Askofu Mwamakula: CHADEMA na CCM ni kama wapenzi wawili waliongia kwenye mahusiano bila kufuata taratibu

Precious Diamond

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
397
993
Akiwa kwenye mahojiano na mwandishi wa waandishi wa habari, Askofu Mwamakula amesema anafananisha mazungumzo ya CCM na CHADEMA kama wapenzi walioingia kwenye mahusiano bila kufata utaratibu, sasa hivi mambo yameharibika kila mmoja analalamika.

Akisema Mazungumzo ya CHADEMA na CCM yalikuwa siri, hakuna anayejua waliongea kitu gani, wengine tukiwa tunafahamu tu mambo yalikuwa yanaendelea bila kujua nini hasa kinajadiliwa, na kwamba walikiuka kanuni za mazungumzo kwani hakuna taasisi yoyote huru ilisimamia mazungumzo hayo, sasa wameumizana malalamiko yao ndio wanakuja kuyatoa nje.

CHADEMA wanalalamika mapendekezo yao yote kupuuzwa huku CCM wakisema wamewafanyia CHADEMA hisani na kuwatoa gerezani.

Askofu Mwamakula amesema wanachopendeza ni kuwa, haijalishi yale mazungumzo waliumizana kiasi gani, kwakuwa hili ni jambo la kitaifa, pande zote mbili zikae, lakini iwepo taasisi huru pembeni ya kusimamia mazungumzo yao.

Akaongeza kuwa endapo mmoja atakuwa mbabe na kumshinda mwenzake demokrasia itakuwa nyonge, lakini kama watu wanaoheshimiana wakiwa na misimamo tofauti wakiwekwa meza moja wakatoa nyongo, mwishowe wakasuluhiswa mpaka kufikia muafaka likitoka jambo pale kila mmoja atakitunza na kusema hichi ni chakwetu, na mmoja; upande wa serikali na upinzani wataheshimika!
 
Akiwa kwenye mahojiano na mwandishi wa waandishi wa habari, Askofu Mwamakula amesema anafananisha mazungumzo ya CCM na CHADEMA kama wapenzi walioingia kwenye mahusiano bila kufata utaratibu, sasa hivi mambo yameharibika kila mmoja analalamika.

Akisema Mazungumzo ya CHADEMA na CCM yalikuwa siri, hakuna anayejua waliongea kitu gani, wengine tukiwa tunafahamu tu mambo yalikuwa yanaendelea bila kujua nini hasa kinajadiliwa, na kwamba walikiuka kanuni za mazungumzo kwani hakuna taasisi yoyote huru ilisimamia mazungumzo hayo, sasa wameumizana malalamiko yao ndio wanakuja kuyatoa nje.

CHADEMA wanalalamika mapendekezo yao yote kupuuzwa huku CCM wakisema wamewafanyia CHADEMA hisani na kuwatoa gerezani.

Askofu Mwamakula amesema wanachopendeza ni kuwa, haijalishi yale mazungumzo waliumizana kiasi gani, kwakuwa hili ni jambo la kitaifa, pande zote mbili zikae, lakini iwepo taasisi huru pembeni ya kusimamia mazungumzo yao.
Kifupi CCM na chadema wametufanya wananchi wajinga!!

Tunataka katiba mpya sio maridhiano ya siri kama hakuna katiba na uchaguzi usiwepo!!

Ccm ikabidhi madaraka Kwa Dola kwasababu imeshindwa kufuata taratibu walizowekewa kwamba katiba ipatikane kwanza ndio uchaguzi ufuate!!

Kama hakuna katiba hakuna uchaguzi mpya!!
 
Back
Top Bottom