Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,820
- 4,573
JOPO la Madaktari katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Kusini, Mtwara wamefanya upasuaji wa kuondoa damu kwenye ubongo wa mtoto wa miaka tisa kwa mafanikio makubwa baada ya kutumia vifaa vya kisasa kufanya uchunguzi na kubaini tatizo hilo.
Akizungumza Kwa njia ya simu na chombo kimoja cha habari kuhusu upasuaji uliofanyika jana, Dk Hashimu Titto wa hospitali hiyo amesema kuwa wamefanya upasuaji wa kwanza kwa mafanikio makubwa kwa mtoto wa miaka tisa aliyegongwa na pikipiki.
“Zoezi la kutoa damu iliyovilia kwenye ubongo wa mtoto mdogo baada ya kupata ajali limefanyika kwa utaalam mkubwa na kwakweli limefanikiwa, awali tulifanya vipimo na uchunguzi na ikagundulika kuwa na damu kwenye ubongo iliyovilia baada ya kupata ajali ya kugongwa na pikipiki,”amesema.
Credit: Nipashe