Nyakijooga
Senior Member
- Dec 9, 2018
- 123
- 202
Ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam Machi 25, 2024 katika Mkutano wa Kimataifa wa wataalamu wa ubongo,mishipa ya fahamu na uti wa mgongo ulioandaliwa na MOI kwa kushirikiana na Chuo na Hospitali ya Well Cornel iliyopo nchini Marekani
Aidha akieleza kuhusu mkutano huo unaofanyika kwa siku nne, amesema unatoa mafunzo ya tiba inayotokana na ajali zinazoumiza ubongo na kuwa yatawasaidia wataalamu kuwatibu watu walioumia kwa ajali zilizoathiri ubongo na mgongo.
“Wataalamu wanajengewa uwezo kuwatibu kwa umahiri na kupunguza matatizo yanayotokana na ajali tumekuwa tukishirikiana kwa muda wa miaka 12,” amesema.
“Pia tunapata wataalamu kutoka Marekani ni ushirikiano wa faida kwa pande zote mbili kila mwaka tunakutana,” amesema.
Licha ya hivyo Prof. Makubi amesema idadi ya wataalamu hao bado ni ndogo, ambapo ameweka wazi kuwa MOI kuna madaktari bingwa 12 na nchi nzima wako 23 ikilinganishwa na idadi ya Watanzania.
Kwa upande wa Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo, Uti wa Mgongo na Mishipa ya Fahamu, Dk Hamisi Shabani amesema kabla upasuaji wa uti wa mgongo wagonjwa walikuwa wanapelekwa nje lakini sasa wote wanatibiwa ndani.
“Sasa imepatikana hamasa ya madaktari kujifunza, mimi nilikuwa daktari wa tatu walipokuja sasa wako 23, ila sio somo gumu ambalo watu wanatakiwa kukimbia imekuwa rahisi kwetu kuongeza ujuzi tofauti na awali,” amesema.
Amesema wana wanafunzi sita kutoka nje ya nchi na wanne wa ndani ya nchi na kwamba watatumia teknolojia mpya baada ya vifaa kuletwa vya endoscopy, ambapo mgonjwa atakaa saa chache hospitali.
Ameongeza kuwa bado kuna uhaba wa madaktari bingwa, ambapo kwa viwango vya Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa nchi zinazoendelea daktari mmoja anatakiwa kuhudumia wagonjwa 100,000 kwa mwaka, huku kwa sasa nchini daktari mmoja akihudumia wagonjwa milioni 1.2 kulingana na idadi ya Watanzania .
Pia Prof Roger Hartl kutoka Chuo cha Well Cornel amesema amejifunza mbambo mengi baada ya kuja Tanzania ambayo yamemsaidia kuhudumiwa wagonjwa wake huko Marekani.
“Tumetengeneza mfumo wa kufundisha wataalamu kwa kubadilishana ujuzi wanakuja kwetu na sisi tunakuja kwao ili kuhakikisha tunahudumia wagonjwa kwa namna ya kufanikiwa ,”ameeleza.