MALUNGU
JF-Expert Member
- Jun 2, 2011
- 250
- 97
Nguvu hizi zinazotumika ni kiashirio cha ukomo wa kufikiri.Mjadala wa Gesi au Rslimali za taifa kwa ujumla hauwezi kuzimwa kwa nguvu.Dikteta Dhalimu Wa Nigeria General Sani abacha alitumia Nguvu nyingi kuwanyamazisha Akina Ken Saro Wiwa kule Niger Delta akishirikiana na makampuni ya kibepari ya Shelly,CHEVRON,BP n.k katika kuhujumu raslimali ya Mafuta dhidi ya watu wa Ogun lakini mwisho wake haki ilishinda na yeye alikufa vibaya.
Hapa Tanzania watawala wanatuelekeza kufuata njia ya Ken,Daima tutashinda!
Wananchi wamechoka mpaka basi, ila kwa kuwa watawala wetu wanasubiri taarifa za hao wanaotaka kuwasifia tu, mwisho wake watakuja kuuona siku ikulu ikiwa imezungukwa na watu. Wakiwa wanataka nyumba yao wamweke wanayemtaka. Sipendi umaskini ila hawa wanaonisababishia ipo siku watajutia haya wanayoyafanya.