Toba yarabi,yamekuwa hayo?
...........halafu ndo ukweli sasa.
Hiyo inaitwa killing me softly......ni utaratibu mzuri tu Kaunga unazuia watu wasinywe sumu.
Nimepokea ombi maalum toka kwa mama chanja wangu mtarajiwa ,anasema kuna mtu kamwomba ushauri,katika hili naye anaomba mchango wenu.
Ni hivi:
Kuna mdada mmoja (tumwite Cindy), Cindy aliolewa na akaachika.Alipata watoto wawili kwenye ndoa yake na anaishi mwenyewe na wanae.Majuzi kuna baba mmoja aliingia kwenye ofisi ya dada yake Cindy (tumwite Brenda) na hapo ofisini huyo baba aliona picha ya Cindy na akamtunuku. Alijitahidi kuomba contact za Cindy lakini Brenda akawa anakataa.Jamaa king'ang'anizi pamoja na Cindy kumwambia dada yake asitoe contact zake lakini tokana na presha yajamaa mwisho Brenda alimpa jama namba ya Cindy.Zikanza simu na sms zisizoisha mpaka Cindy akakubali akutane na jamaa.Wakakutana,wakala,wakanywa,in the process Cindy akamweleza jama ukweli kuwa yeye ni divorcee with two kids.Kuanzia siku hiyo hajamsikia wala kumwona jamaa tena.
Cindy anajiuliza hivi jamaa kakimbia kisa ana watoto? Au kisa ni u divorcee?apparently dada yake kumbe hakumweleza jamaa kuwa cindy aliwahi kuolewa na ana watoto.
Hivi wanaume mnakerwa kuwa na mwanamke mwenye watoto/divorcee,kwa nini?
Na wewe unaamini?
Dark City naomba nikuulize swali ila mtu yoyote anakaribishwa kulijibu. Hivi wewe kama mwanaume ukiwa unamtaka mwanamke(na huna uhakika kama hana bwana) ukawa kila ukimpigia simu yuko home hata iwe late(yani mida yoyote,after working hrs)hana cha weekend wala nini. Huyo mwanamke utamfikiriaje???anafaa au anaogopesha kupelekea ww uchanje mbuga lol......nataka kujua wanaume in general(ama wengi wenu)huwa mnamuonaje mtu kama huyo.
Watu wanatofautiana,na si kila mtu anaweza kuwa na guts za kusema kila kitu kilichoko moyoni mwake. Ndiyo maana kuna watu wanajua sana kupepesa mdomo wakati wengine wanongea kwa vitendo. Kila njia ina madhara yake!
Babu DC!!
Hivi wanaume mnakerwa kuwa na mwanamke mwenye watoto/divorcee,kwa nini?
mwambie cindy hasihofu ni upepo tu utapita, atapata anayempenda,japo wanaume weng hawapendi wanawake wenye watoto, ukiongezea na kuachika huo ni upepo mkubwa.
Babu heshima yako.....na pia huwa tunaamua kukaa kimya na kuondoka ili kutoumiza as sometimes if not always......truth hurts.....sasa kuliko kumuumiza mtu its better kukaa kimya na haswa kama ukweli hautabadilisha the status quo
Kaunga my sis..how are you
Lakini mko tofauti mind you as wengine ukimpa ukweli aweza lia mpaka ukaanza kujisikia vibaya.....sasa its better to quit than telling it at the opening and leave a psychological scar and a permanent attitudinal depression......
Hili kwa mwanaume yeyote mwenye busara ni kukaa kimya unless the second side atake maelezo na pia inabidi kupima sana kbla ya ku burst open kwa sababu tajwa hapo juu
Bishanga hili swali ni wewe umelianzisha yule njemba hakutoa sababu ya kwanini kakimbia. Kumbuka ya kuwa alilia simu ya Cindy kutokana na taswira ya picha tu aliyoiona na alipokutana naye na kukaa naye kitako hatujui alipata picha ipi.................yawezekana majukumu tajwa yalimtibua au aliona hawataeza kuelewana na Cindy.............
Now nimejua namna wanawake wenye watoto wanavyoteseka na jamii kuwanyanyapaa kwa sababu wana watoto,jambo hili litaongeza maumivu sana kwa wanawake ambao tayari wako kwenye ndoa zenye mateso!Watahofia kuondoka kwa kujua after that hakuna mwanaume atakua anashida nae kwa sababu ya watoto au mtoto unless awe na vitu vya kuwavuta wanaume kama fedha n.k.To my opinion mwanamke wa aina hii ni mwanamke bora kuliko asiyekuwa na mtoto!
Babu DC,ni kweli wanateseka sana tena sana,bahati mbaya sana sisi wanaume ndo tunaosababisha tatizo hili kwa njia zote.Sisi ndo tunaowatia mimba,sisi haohao tunawaacha halafu hatuwataki tena kuwaoa,balaa kubwa!