Mazingira yaliyomzunguka mwanadamu hutupa signals zilizobeba ujumbe

Ivan Stepanov

JF-Expert Member
Apr 22, 2023
4,889
15,939
Wakuu habari za wakati huu. Ni matumaini yangu hamjambo, na wale wenye changamoto (ni sehemu ya maisha japo zinazidiana), basi mwenyezi Mungu awafanyie mlango.

Nimependa tu kuandika hiki kitu japo kinaweza kisiwe kwa ajili ya kila mtu lakini sio mbaya ukisoma kwakua it doesn't cost you a penny.

Kilichonisukuma kuandika hii composition ni baada ya tukio la siku ya jana ambalo limeibuka leo, na ilikua hivi.

Jana baada ya kutoka katika shughuli za kutafuta mkate wa kila siku kama ilivyo ada, nikaona hapa nimechelewa home na nikisema nipande daladala nitakwama kutokana na foleni za jijini hapa zilivyo.

Basi nikakwea boda boda kuelekea home (uelekeo wangu ni Kilwa road) mpaka nilipo hitisha safari yangu na kufika home na maisha mengine yakaendelea na leo nikaingia mzigoni kama kawaida.

Sasa nika post status kwenye moja ya namba zangu kadhaa za whatsapp ambazo ni private zaidi. Na baada ya muda nikapokea comment toka kwa namba ya mshkaji wangu wa zamani sana. Huyu ni home boy na yeye yuko town hapa.

Hatujaonana miaka mingi sana toka tukiwa wanafunzi huko nyanda za juu kusini magharibi. Ile text ikasema "Hii sura nimeiona jana kwenye boda boda". Nikacheka sana kisha tukaongea mambo ya hapa na pale kama unavyojua wanaume hatunaga mambo mengi, tunaongea ya msingi tu.

Nikalazimika kuuliza alinigunduaje maana siku hiz nime badili sana muonekano wangu licha ya utu uzima wa mid 30 now na tumeonana last time tukiwa teenegers (usiulize kuhusu namba yake nilipata wapi na yeye alipata vipi yangu, hii ni stori nyingine)

Mimi: aisee kwanini hukunishtua uliponiona?

yeye: Isingewezekana, maana na mimi nilikua kwenye daladala na wewe ulitupita ukiwa kwenye boda boda.

Mimi: sasa uliweza vipi kuni spoti kisha ukanigundua kama ni mimi maana ni kitendo cha ghafla sana?
(HAPA JAPO ALIJIBU KIUTANI LAKINI JIBU LAKE LIKANIACHA NA FIKRA)

Yeye: ahahahahaah!! nahisi nilipokea signals tu from the universe nikajikuta na concerntrate kutzama dirishana kisha ghafla nikakuona unapita na nikakujua kwamba ni wewe licha ya kwamba ume change sana.

Mimi: ahahaah aisee, that was really the signal vibration from the universe!

Basi tukaendelea na mambo mengine lakini baadae nikajikuta fikra zangu zinarudi sana hapa kwenye sentensi hizi mbili

Yeye: ahahahahaah!! nahisi nilipokea signals tu from the universe nikajikuta na concerntrate kutzama dirishana kisha ghafla nikakuona unapita na nikakujua kwamba ni wewe licha ya kwamba ume change sana.

Mimi: ahahaah aisee, that was really the signal vibration from the universe!

Na katika kutafakari katika namna tofauti tofauti nikajiambia tu kwamba "MAZINGIRA YANATUMA MESSAGE nyingi sana kwa mwanadam lakini si wengi tunao tilia maanani".

Na jumbe hizi toka kwenye mazingira huwa na malengo mengi tofauti tofauti kama kumpa taarifa, kumpa tahadhari, kumpa "way out" ya changamoto fulani fulani anayo kabiliana nayo n.k n.k na hii ni kutokana na "fact" kwamba huwezi kumtenganisha mwanadamu na mazingira ("enviroment is anything that surrounds us"-mwanangu Marry juzi nikakumbuka alichokua ananisimulia walichojifunza huko darasa la pili kuhusu mada ya mazingira)

Kwa kutafakari haya machache kuhusu namna mazingira ambavyo yamekua "benet" na mwanadamu kuwasiliana nae na kumtumia signal mbali mbali ambapo zingine humpa a "plain & clear message" au saa zingine hutuma signal zitakazo "invoke" fikra ili ku "connect dots" na ku "solve puzzle" nikakumbuka mfano huu ambao ni ushuhuda halis katika maisha yangu.

USHUHUDA WANGU-nitaeleza kwa kifupi.

Mwaka 2020 mwanzoni kabisa niliamua kuacha kazi na kuamua kuwa mjasiriamlai kuji engage kwenye project zangu (professionally a software guy). Kama ambavyo inafahamika mwanzo sio mwepesi na pia niliacha kazi sikua nimejiandaa kutoka na mazingira yalionitokea mpaka kuchukua uamuzi huo so sikua na kitu chochote kile kuingia nacho mtaani. Maisha yakanipiga sana but baada ya muda mrefu kidogo nikaomba msaada kwa mshkjai wangu anisaidie ku rescue situation yangu financially maana hali ilikua mbaya personally na familywise. Jamaa akanitafutia kazi maeneo ya Mwenge, na kiukwel ilikua ni kazi tuu bora mradi mkono uende kinywani hakukua na future yoyote nayoiona mbele, si kwamba silipwi,ila sikua naifurahia kazi hata kidogo maana haikua inatatua changamoto zangu za kiuchumi hata kidogo, project yangu nikai "suspend" kwa muda nikiwa napambana na kibarua cha watu.

Kila siku asubuh nilikua napanda daladala za mnazi m1-Mwenge hivyo ni lazima nipite SOKO LA MABIBO. nilikua ni mtu wa mawazo sana sana. Naogopa tu kuacha kazi kwakua ni mshkaji kaniunganisha kwa watu wanaoheshimiana sana na wao wakanipokea bila longo longo sasa nikiondoka nitamuharibia mchizi na yeye hakusita kunisaidia nilipomlilia shida anisaidie kazi, SASA NITAFANYAJE?

ANGALIA SASA CONCEPT YA MAZINGIRA NA SIGNALS ZAKE!.
kila siku napita MABIBO SOKONI nikiwa kwenye daladala na kumbe kuna kitu nilikua na miss sikioni until ONE DAY nilipofungua macho. huwa nafikiriaga kwamba INTENSITY YA SIGNALS FROM THE SURROUND siku hii probably ilikua kubwa sana that I COULDNT IGNORE anymore AU siku hii NILITENGENEZA UTULIVU WA NDANI kwa kiwango ambacho I WAS REALLY ATTACHED TO THE ENVIROMENT AND GIVE THE SURROUNDING A WAY TO CONTACT ME kwa urahisi.

siku hii nilipofika eneo hili la sokoni mabibo, NILIWATAZAMA SANA wale raia, wanawake kwa wanaume, vijana watoto kwa wazee ambao kimsingi walikua busy sana na majukumu yao.
  • wengine wakishuka magunia mazito ya viazi toka kwenye malori na kuyaweka mgongoni
  • wengine wakibeba magunia ya mkaa mazito migongoni toka kwenye malori
  • wakina mama wengine wakipanga mafungu ya viazi chini na kuuza
  • vijana na watoto wengine wakiuza mifuko na vifunganshia kwa wateja wanaonunua mahitaji yao.
  • akina mama wengine na akina dada wako busy na machupa ya chai na uji wakiuza

shughuli zilikua nyingi sana LAKINI KUNA KITU KIMOJA nilikiona katika nyuso za watu hawa ambao kwa picha ya haraka haraka ni WAHANGAIKAJI tuuu, wengi walikua na NYUSO ZA FURAHA, wanafanya yote wakiwa na USO MKUNJUFU wana furahia zile process na harakati zao wengi wakitukanana na kutaniana huku wanacheka katika KUPEANA HAMASA YA kile kila mtu anafanya. WAMEAMUA KUYAFURAHIA MAISHA YAO YA WAKATI HUU HUKU WANAENDELEA KUPAMBANIA KESHO YAO ambayo bado hawaijui ila WAKIONEKANA WANA MATUMAINI na IMANI ndio maana wanafurahi.

SIO KWAMBA walikua wana RAHA KULIKO MIMI. au sio kwamba mimi nilikua na SHIDA KUWAZIDI WAO...HAPANA.

nikawaza hivi mimi nina sababu gani ya kutofurahia maisha. KWANINI NAKATAA UHALISIA KWA WAKAT HUU na huku ndio ukweli wenyewe. KWAMBA kwasasa haya ndio maisha yangu, i should LEARN TO COPE AND ACCEPT while am fighting for better future!! KWANI ININIGHARIMU HOW MUCH KUWA NA MINDSET HII???mbona hawa wanaweza WHY AM I DWELLING IN SADNESS kisa tu nachokitafuta hakija fika?

from that moment on , I CHANGED MY MINDSET.

Nikajiuliza KWANINI SIKUA NA FIKRA HII MUDA WOTE HUU NA NINAPITA HAPA KILA SIKU NA KUWAONA HAWA WATU ?KWANINI NAJIFUNZA LEO KITU AMBACHO I COULD LEARN FROM THE SAME MOTHER NATURE FROM THE VERY FIRST DAY?

Nikagundua kwamba I BLOCKED THE MY HEARING FROM THE SURROUNDINGS, SIGNALS WERE BARRED FROM INVOKING MY BRAIN TO GRASP THE MESSAGE FROM THE ENVIROMENT.

Na hii ilinifanya kupunguza sana FULL TIME KUWEKA EAR PHONES MASIKIONI au KUTUMIA SIMU MUDA MWINGI NAPOKUA KWENYE FOLENI.

Mwisho.
 
Ipo hivyo unapowaza kitu au kumuwaza mtu basi unazalisha signals ndio pale unamtembelea mtu unashangaa wanakwambia leo tulikua tunakuongelea basi kumbe walipokua wanakuongelea walizalisha signal ambazo zili click kwenye subconscious yako na wewe ukajikuta unaenda kwao.

Nadhani hiki ndicho Elon Musk anataka kukifanya kupitia neural Link
 
Ipo hivyo unapowaza kitu au kumuwaza mtu basi unazalisha signals ndio pale unamtembelea mtu unashangaa wanakwambia leo tulikua tunakuongelea basi kumbe walipokua wanakuongelea walizalisha signal ambazo zili click kwenye subconscious yako na wewe ukajikuta unaenda kwao.

Nadhani hiki ndicho Elon Musk anataka kukifanya kupitia neural Link
sure mkuu
 
Back
Top Bottom