Mtumishi wa umma mbaroni kwa kuchana na kuchoma Quran, Waziri Jafo aagiza asimamishwe kazi

SURA YA KUMI NA NNE
MAKOSA YANAYOHUSIANA NA DINI NA MAZISHI
125. Mtu yeyote ambaye atavunja, kuharibu na kuchafua mahali popote pa kuabudia au kitu chochote kinachoitwa kitakatifu na watu wa aina yeyote kwa madhumuni ya kufedhehesha dini ya kundi lolote la watu au kwa kufahamu kuwa kundi lolote la watu linataka kufanya uharibifu, hasara au uchafuzi kama fedheha kwa dini atakuwa ametenda kosa.

126. Mtu yeyote ambaye kwa hiari yake ataleta fujo kwenye mkusanyiko wowote ambao umekusanyika kihalali kufanya ibada au sherehe za dini ametenda kosa.

127. Mtu yeyote ambaye, kwa madhumuni ya kuumiza imani za mtu yeyote au kufedhesha dini ya mtu yeyote, au kwa kufahamu kuwa imani ya mtu yeyote inaweza kuumizwa, au dini ya mtu mwingine iko hatarini kufedheheshwa, ametenda kosa la kuingia kwenye eneo la kuabudia bila ruhusa eneo la makaburi matakatifu au kwenye eneo lolote ambalo limetengwa kwa ajili ya mazishi au kama bohari ya mabaki ya maiti, au atafanya dhuluma yeyote kwa maiti ya binadamu au atafanya fujo kwa watu wowote waliokusanyika kwa ajili ya mazishi, atakuwa ametenda kosa.

128. Mtu yeyote ambaye bila halali anazuia mazishi ya mwili wa mtu yeyote aliyekufa au mtu ambaye, bila mamlaka halali kwa niaba hiyo au vinginevyo kulingana na kanuni iliyowekwa na Waziri anayehusika na afya (ambayo unamuongoza Waziri aliyepewa mamlaka kufanya) anafukua kaburi, anapasua, au anafanya uharibifu wowote kwenye mwili wa mtu yeyote aliyekufa au ambaye, anawajibika kufanya maiti ya mtu yeyote izikwe, kwa hiari yake na bila kupewa idhini na mamlaka halali anapuuza kutimiza wajibu wake kwa makusudi , atakuwa ametenda kosa.
129. Mtu yeyote ambaye kwa dhamira ya kuudhi imani ya mtu yeyote ya dini yake akatamka maneno yeyote au akafanya sauti yeyote itakayosikiwa na mtu huyo au akafanya ishara mbele ya macho ya mtu huyo atakuwa ametenda kosa.

ᴸᵉᵍᵉⁿᵈᵃʳʸ
Tafuta wanasheria wakusaidie Bwana mdogo. Sheria hazisomwi namna hii ya kupesti maandishi na kukariri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilikuwa nasikia ukichana hio unakuwa chizi, kumbe fix tu!
.Nawewe unaweza jaribu, mbona nyote mumetoka kwenye mti mmoja mnafundishwa chuki badala ya kuelewa biblia
kumbe hii ndio elimu ya kwenda shule lakini sio kuelimika!
 
HEKIMA NA BUSARA ni kitu mhimu Sana,......usifanye tu chochote unachojisikia ,fikiria kwanza unachofanya kina umhim gan kwako na kwa upande mwingine kina athari gani
Hiyo JUZUU si ni maandishi tu kwani ina nini cha mno sana!?

Ni kweli kijana kakosa busara lakini hili sio kosa la kusimamishwa kazi.

Kukosa busara sio jinai wala sio kosa la kimaadili.

JUZUU ni ya kwake mwenyewe ana uamuzi hata wa kuinyea na kuikojolea!



Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani hata picha yake unamwona Yuko sawa? Kikubwa kilichonifurahisha Mimi Ni kuwa kwa waislamu kumpeleka katika mamlaka husika, hii Ni hatua nzuri Sana na ndio Msingi mmojawapo wa Imani hiyo, Kitendo Cha kukamatwa na kusimamishwa kazi kwake huyu jamaa Ni adhabu Tosha tu, Binafsi ninamwomba Allah amwongoze kijana huyu aweze kuijua haqi na kuifuata na amuepushe na mihemko itakayoleta mitafaruku katika jamii si tu ya Kitanzania Bali iwe kwa ulimwengu kwa ujumla.
Nilikuwa nasikia ukichana hio unakuwa chizi, kumbe fix tu!
 
Huyu
Hajaichana Quraan,Bali ameichana heshima yake

Waislam
Wanatakiwa watulie juu ya tukio kama hili,Wasifanye chafuko au fujo ya aina yoyote

Quraan bado katika maisha yetu
Kama angetaka kuichana,Basi angechana Vifua vyetu

Waislam tusomeni Dini yetu
Kuiwacha Dini,ni mbaya zaidi kuliko aliechana karatasi zilizoandikwa ndani yake Quraan

Tusomeni Dini yetu
Tusomeni Dini yetu
Tusomeni Dini yetu
Mtumishi wa Serikali aliyechana Quraan Tukufu asimamishwa kazi, Taarifa hiyo imetolewa leo na Waziri wa TAMISEMI Mhe. Suleiman Jaffo.

RPC Morogoro Wilbroad Mutafungwa amethibitisha kukamatwa kwa kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Daniel Maleki, kwa kosa la kuchana na kuchoma moto kitabu cha Juzuu Amma ambacho ni sehemu ya Quran Tukufu.

“Maleki ni Afisa Biashara wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, alionekana akichana na kuchoma kitabu hicho Kitakatifu cha dini ya Kiislamu, kitendo ambacho kiliwakasirisha Waumini wa dini hiyo na wananchi waliokuwa maeneo hayo na kuamua kutoa taarifa kwa Polisi” RPC Mutafungwa.

Muheshimiwa Jafo amesema, Mtumishi huyo yuko chini ya ofisi ya Rais na jambo alilofanya halileti afya kwa jamii. Muheshimiwa Jafo amemtaka mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilosa kumsimamisha kazi mtumishi huyo pia afanye uchunguzi na kamati au mamlaka yake ya nidhamu iweze kuchukua hatua kadiri atakavyoona inafaa mara baada ya uchunguzi huo


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa kama hoja ni hiyo si jeshi la polisi tayari limemkamata na watamfungulia mashtaka kwa mujibu wa katiba? Kusimamishwa kazi kunakujaje? Kwani amevunja sheria za kazi?
Mimi nafikiri kama mtumishi wa serekali kuna ethics za utumishi ukiachana na hizo sheria wenzetu wanazo ulizia, lakini pia nikitendo cha uchochezi nakusababisha uvunjifu wa amani inchini kwahiyo anasitahili kuchukilia hatua pamoja na futwa kazi.
 
Mimi nafikiri kama mtumishi wa serekali kuna ethics za utumishi ukiachana na hizo sheria wenzetu wanazo ulizia, lakini pia nikitendo cha uchochezi nakusababisha uvunjifu wa amani inchini kwahiyo anasitahili kuchukilia hatua pamoja na futwa kazi.

OK
 
Watu walimlaumu samatta kujenga msikitini kwa kuwa anashabikiwa na watu wa dini zote,wakadai angejenga hospitali ingesaidia jamii bila kubagua dini,
Sasa huyu mtumishi wa umma anaonyesha chuki zake hadharani kwa dini flani ambayo waumini wake wanatakiwa kupata huduma kutoka kwake wale wale waliomkosoa samatta wanaunga mkono tukio hili.....inasikitisha sana ndugu zangu,hata kama muislamu akifanya tukio la kudhalilisha dini ya kikristo au kitabu cha dini hiyo haifai.
 
Sasa kama hoja ni hiyo si jeshi la polisi tayari limemkamata na watamfungulia mashtaka kwa mujibu wa katiba? Kusimamishwa kazi kunakujaje? Kwani amevunja sheria za kazi?
Jeshi la polisi Ni chombo kingine na Wizara anayoitumikia mtumishi Ina mamlaka yake dhidi ya Hiki alichofanya kwakuwa kimetia doa taswira ya watumishi kifupi imeshusha hadhi ya mtumishi wa Uma.
 
Hiyo JUZUU si ni maandishi tu kwani ina nini cha mno sana!?

Ni kweli kijana kakosa busara lakini hili sio kosa la kusimamishwa kazi.

Kukosa busara sio jinai wala sio kosa la kimaadili.

JUZUU ni ya kwake mwenyewe ana uamuzi hata wa kuinyea na kuikojolea!



Sent using Jamii Forums mobile app
You wrote like alearned person but the context of your statement exposes your ignorance in both you yourself and your family and funny enough your family, community and clan might be depending on you as their Wiseman of the century.
 
nimeitazama vizuri sana ile clip. nimeitazama huku nikiwa katika tafakari ya hisia ya sita.

nilichogundua, tukio linaloonekana ni la kutengenezwa na walioratibu zoezi lile wamelifanya kwa ustadi na kwa dhumumi maalum.

kuna ajenda fulani fulani wenye mamlaka wanataka kuzififisha kwa kupitia tukio lile. na nahisi watafanikiwa.

kila mtu ajaribu ku-connect dot kwa namna anavyojua yeye, bila shaka mtaelewa nazungumza nini.
 
Back
Top Bottom