DED Uvinza asimamishwa kazi na Waziri Mkuu kwa kuchelewesha miradi ya Serikali

Rusumo one

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
3,079
3,610
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Uvinza mkoani Kigoma, Zainab Mbunda na Mweka Hazina wa Halmashauri hiyo Majid Mabanga ili kupisha uchunguzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU), kwa madai ya kuchelewesha utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambayo tayari Serikali imekwishatoa fedha.

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa uamuzi huo mkoani Kigoma mara baada ya kukagua ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Uvinza na jengo la halmashauri hiyo ambayo licha ya Mkurugenzi kukiri kuwepo kwa fedha za utekelezaji wake toka mwaka 2021 ujenzi wake bado haujakamilika.

TBC

IMG-20230921-WA0066.jpg
 
Huyu mkurugenzi bwege sana, fedha ipo na anakiri hivyo sasa anachelewesha kwa nini!

Uzembe, mazoea, akili ndogo haiwezekani yeye analipwa posho na mshahara ila ikifika kwenye utekelezaji ana chelewesha.
 
Kuna wadada wengine bora warudishage vijiti tu kwa president, coz hata muonekano wao usadiki yakuwa majukumu waliyopewa ni mazito kwao!!
Kazini hawana utendaji wa ubunifu, wametulia wakingoja kuelekezwa nini cha kufanya toka juu
Huo mwonekano inaonesha majukumu kidogo yamekuwa makubwa

Ama wazee wa Uvinza washa mpiga juju hakumbuki majukumu yake
 
Kfuatia maelekezo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa ya kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma Zainab Mbunda na Mwekahazina wa Halmashauri hiyo Majid Mabanga, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mohamed Mchengerwa (Mb) amemwelekeza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI kutekeleza maelekezo ya Waziri Mkuu mara moja kwa kuwasimamisha kazi Mkurugenzi na Mwekahazina huyo kuanzia leo tarehe 21, 9, 2023 ili kupisha uchunguzi.

Uamuzi huo umefikiwa mkoani Kigoma mara baada ya Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa kukagua ujenzi wa hospitali ya Wilaya na Jengo la Halmashauri ambayo licha ya Mkurugenzi kukiri kuwepo kwa fedha za utekelezaji wake tangu mwaka 2021 ujenzi wake bado haujakamilika.
 
Kuna wadada wengine bora warudishage vijiti tu kwa president, coz hata muonekano wao usadiki yakuwa majukumu waliyopewa ni mazito kwao!!
Kazini hawana utendaji wa ubunifu, wametulia wakingoja kuelekezwa nini cha kufanya toka juu
mwacheni, yeye si amesema anataka ajaze wanawake ili twende sawa?
 
Mimi nilifikiria pale kigezo cha kuteua watu kutokana na uzoefu wao kazini kukoma, basi wateule wapya kwa kigezo kikuu cha ukada wataleta mabadiliko! Kumbe urasimu na ubabaishaji ndiyo umetawala kuliko wakati mwingine wowote ule.
 
Back
Top Bottom