Mtumishi wa umma mbaroni kwa kuchana na kuchoma Quran, Waziri Jafo aagiza asimamishwe kazi

Hii ni mihemko isiyokuwa na maana ktk utumishi wa umma. Amemsimamisha kazi kwa kutumia kifungu kipi cha sheria za kazi? Kuna mahali pameandikwa kuwa mtumishi wa umma akichana kohorani asimamishwe kazi? Aache hizo. Analogia Malenga,

Sent using Jamii Forums mobile app
Mtumishi wa Uma anatakiwa kuwa na haiba na Mfano Bora katika jamii Jambo ambapo litaleta umoja, upendo, amani na mshikamano katika jamii, ukitafakari kiasi kidogo tu, utaona amevunja "Code of ethics" bila Shaka amefanya kitendo hicho bila kutafakari hatma yake, kitu ambacho so sahihi kwa Mtumishi wa Uma kufanya alichofanya.
 
Mtumishi wa Uma anatakiwa kuwa na haiba na Mfano Bora katika jamii Jambo ambapo litaleta umoja, upendo, amani na mshikamano katika jamii, ukitafakari kiasi kidogo tu, utaona amevunja "Code of ethics" bila Shaka amefanya kitendo hicho bila kutafakari hatma yake, kitu ambacho so sahihi kwa Mtumishi wa Uma kufanya alichofanya.
Sasa kama hoja ni hiyo si jeshi la polisi tayari limemkamata na watamfungulia mashtaka kwa mujibu wa katiba? Kusimamishwa kazi kunakujaje? Kwani amevunja sheria za kazi?
 
MIMI NILIVYOONA HAPA KUWA HUYU ALIKUWA ANATAFUTA NJIA YA KUHAMISHWA KAZI NA KUPELEKWA SEHEMU NYENGINE, SASA AKAONA HII ITAKUWA SAWA KABISA KUFANYA ALIVYOFANYA.
AU HUENDA IKAWA MAISHA YA TANZANIA YAMEMSHINDA AKAONA ATAFUTE NJIA YA KUJIRIPUA NCHI YOYOTE ILE AMBAYO ITAMSAIDIA KWA KUWA NA USHAHDI, KWA HIVYO AKAONA BORA ACHUKUE QURAN AICHANE, NA HUKU ANAJUA KUWA ANARIKODIWA APATE RIKODI ZAKE, IKISHA IKIWA TAYARI KUSEPA, ATOE SABABU YA KUWA USALAMA WAKE UPO HATARINI KWA WAISLAM KWA SABABU AMECHOMA KITABU CHAO, KWA HIVYO ANAHOFIA IKIWA ATAREJESHWA NCHINI HUENDA ATAUAWA.
VITIMBI VITIMBI VITIMBI,
YUPO MBORA ZAIDI YA VITIMBI.
 
Hiyo JUZUU si ni maandishi tu kwani ina nini cha mno sana!?

Ni kweli kijana kakosa busara lakini hili sio kosa la kusimamishwa kazi.

Kukosa busara sio jinai wala sio kosa la kimaadili.

JUZUU ni ya kwake mwenyewe ana uamuzi hata wa kuinyea na kuikojolea!



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii Mh. Jaffo kachemka, hakuna sheria inayo sema hivyo.
Serikali wajiandae kulipa fidia pesa ndefu.

Sema yule mangi nae sifa zimezidi.
Mkuu japokuwa hajuani lakini unatakiwa ujue kwamba kuna sheria na kuna order, sheria atakama haipo haiwezekani mtu ana hatarisha amani ya inchi alafu unazungumzia sheria. Ebu sema hapa wapi umewahi kuona waislam wanachana bibilia? Kama ameweza kuchana Qur'an manaake ata kuua anaweza na kama ameweza kufanya hilo jje ukimukuta ofisini na wewe niwa imani nyingine ataweza kukupa huduma?
 
SURA YA KUMI NA NNE
MAKOSA YANAYOHUSIANA NA DINI NA MAZISHI
125. Mtu yeyote ambaye atavunja, kuharibu na kuchafua mahali popote pa kuabudia au kitu chochote kinachoitwa kitakatifu na watu wa aina yeyote kwa madhumuni ya kufedhehesha dini ya kundi lolote la watu au kwa kufahamu kuwa kundi lolote la watu linataka kufanya uharibifu, hasara au uchafuzi kama fedheha kwa dini atakuwa ametenda kosa.

126. Mtu yeyote ambaye kwa hiari yake ataleta fujo kwenye mkusanyiko wowote ambao umekusanyika kihalali kufanya ibada au sherehe za dini ametenda kosa.

127. Mtu yeyote ambaye, kwa madhumuni ya kuumiza imani za mtu yeyote au kufedhesha dini ya mtu yeyote, au kwa kufahamu kuwa imani ya mtu yeyote inaweza kuumizwa, au dini ya mtu mwingine iko hatarini kufedheheshwa, ametenda kosa la kuingia kwenye eneo la kuabudia bila ruhusa eneo la makaburi matakatifu au kwenye eneo lolote ambalo limetengwa kwa ajili ya mazishi au kama bohari ya mabaki ya maiti, au atafanya dhuluma yeyote kwa maiti ya binadamu au atafanya fujo kwa watu wowote waliokusanyika kwa ajili ya mazishi, atakuwa ametenda kosa.

128. Mtu yeyote ambaye bila halali anazuia mazishi ya mwili wa mtu yeyote aliyekufa au mtu ambaye, bila mamlaka halali kwa niaba hiyo au vinginevyo kulingana na kanuni iliyowekwa na Waziri anayehusika na afya (ambayo unamuongoza Waziri aliyepewa mamlaka kufanya) anafukua kaburi, anapasua, au anafanya uharibifu wowote kwenye mwili wa mtu yeyote aliyekufa au ambaye, anawajibika kufanya maiti ya mtu yeyote izikwe, kwa hiari yake na bila kupewa idhini na mamlaka halali anapuuza kutimiza wajibu wake kwa makusudi , atakuwa ametenda kosa.
129. Mtu yeyote ambaye kwa dhamira ya kuudhi imani ya mtu yeyote ya dini yake akatamka maneno yeyote au akafanya sauti yeyote itakayosikiwa na mtu huyo au akafanya ishara mbele ya macho ya mtu huyo atakuwa ametenda kosa.

ᴸᵉᵍᵉⁿᵈᵃʳʸ
 
Back
Top Bottom