Kuna baadhi ya wachangiaji wanatumia kigezo cha hali ya hewa kuwa ni factor mojawapo ya sisi waafrika kuwa weusi, kwamba tulipigwa sana na jua kiasi kwamba rangi zetu zikabadilika.
Hilo mimi napinga, kwa sababu ukizungumza kigezo cha hali ya hewa utagundua kwamba hapa tanzania kuna baadhi ya maeneo hususani kwa miaka hiyo ya nyuma karibu mwaka mzima ni baridi, kwa mfano maeneo ya lushoto,mafinga,makambako. Sasa kwa nini watu wa huko angalau wasiwe wana rangi ya kizungu kama kigezo mojawapo ni hali ya hewa?