NADHARIA YA KWANZA
:-MTU MWEUSI NDIYE MJENZI MKUBWA WA USTAARABU HAPA DUNIANI
A: ASILI YA MAJINA YA JAMII ZA WATU NDANI YA NADHARIA.
Kuna maneno ambayo yatatumika hivyo ili kuweka mambo sawa na kutowachanganya wasomaji ngoja nielezee chimbuko lake katika historia. Jambo muhimu kabisa kukumbuka ni kwamba majina mengi ya sehemu, taifa au jamii ya watu fulani mara nyingi hutokana na asili ya eneo lile (kama tabia ya nchi), jina la baba wa jamii ile au mtu aliyekaa katika lile eneo husika. Mfano, taifa la Israeli limetokana na Yakobo ( 2006-1859 K.K) ambaye anaaminika kuwa ndiye Baba wa jamii ya Waebrania: au neno Ethiopia, wanahistoria kama Herodotus wa Ugiriki(484-425 K.K) na Flavius Josephus wa Rumi ( 37-100 B.K) walilitumia kutoka kwenye lugha ya kigiriki "
Ethiopos" ambalo linamaanisha mtu ambaye ngozi yake imeungua na jua. Hivyo Basi nchi ya Ethiopia ambayo zamani iliitwa Abyssinia imelichukua neno ambalo linaelezea sifa ya watu wanaokaa nchi hiyo: Au Bara la Ulaya ambalo ni Europe limetokana na jina ambalo linaelezea sifa ya eneo ambalo linahusishwa na mwanamke Europa ambaye kwa lugha ya Kigiriki jina lake lina neno "
Eurus" na "
ops/op-lopt". Ambapo "
Eurus" linamaanisha Pana na "
ops/op-lopt" linamaanisha sura au uso. Hivyo Ulaya maana yake uso mpana kwasababu Wagiriki pamoja na watu wa zamani waliamini ni eneo kubwa sana.
Neno Afrika limegubikwa na utata mwingi kama ambavyo historia ya watu wake ilivyogubikwa na utata. Mpaka sasa watu tofauti wamejaribu kuelezea chanzo cheke kila mtu akivutia kwake. Baadhi ya wasomi wameelezea neno Afrika lilitokea baada ya Jemedari wa jeshi la Rumi aitwae
Scipio Africanus ambaye alishinda vita dhidi ya Ufalme wa Karthago (Carthage) mnamo mwaka 146 K.K. Ambapo dola la Karthago lilikuwepo sehemu ambapo ipo Tunisia leo, hivyo basi Afrika likapewa jina hilo la huyo jemedari. Wengine wakasema neno la Afrika asili yake ni Kigiriki ambapo neno "
Aphrike" linalomaanisha Baridi ndiyo asili yake. Wengine wakasema neno la kilatini "
Aprica" linalomaanisha hali ya jua kali ndiyo asili yake. Mwanahistoria wa Kigiriki Leo Africanus alisema Afrika asili yake ni neno "
Aphrike" linalomaanisha sehemu yenge baridi kali na ya kutisha. Lakini wasomi wengi wanadai kwamba neno Afrika asili yake ni lugha mbili za Kifonike (Phoenecian) na kilatini. Katika lugha ya Kifonike ambayo ilikuwa ni ya watu walioijenga Karthago neno "
Afri" kwao ilikuwa ni Vumbi na neno "Ica" limetoholewa kwenye lugha ya Kilatini kumaanisha Ardhi,nchi. Hivyo basi neno Afrika linamaanisha "Nchi/Ardhi yenye vumbi.
Neno Uarabuni nalo lina asili pana katika muktadha wake. Kwanza kabisa wanahistoria manguli wanalihusisha na maneno ya majigambo ya dola la Kiashuru (Assyria) yaliyoandikwa mwaka 853 K.K. Hili lilitokana na kitendo cha mfalme Shalmanasi kumpiga kivita moja ya machifu wake walioasi. Jina la huyo chifu ni Gindibu Mwarabi. Wanahistoria wengi walitumia kuwaelezea watu wa Shamu ambao walikaa katika ghuba ya Uarabu. Lakini wanahistoria kwa upande mwingine wanahusisha neno "
Arabu" na lugha za watu wa mashariki ya kati hasahasa Waebrania. Ambapo ziliezea sifa za neno na watu wenyewe. Neno la Kihebrania "
Arav" linamaanisha jangwa, ambapo zaidi zaidi kuna lugha zinawealezea zaidi kama watu wanaohamahama au wafanyabiashara. Ukisoma kwenye Biblia kitabu cha pili cha Mambo ya Nyakati 17: 11 kwenye lugha ya Kihebrania utaona kwa mara ya kwanza linatumika kuwaelezea Waarabu kama jamii ya wafugaji. Lakini kwasababu sehemu kubwa ya Elimu ya dunia ya leo imepata ushawishi kutoka kwa nchi za Kigiriki basi Wanafalsafa na Wanahistoria wa Kigiriki walitumia neno Uarabuni kuelezea sehemu yote ya Rasi ya Uarabuni pamoja na nchi kama Misri.
Neno Ethiopia Wagiriki wamelitoa kwenye neno lao "
Ethiopos" ambalo "Aitho" linamaanisha naungua na neno "ops" linaamnisha Uso. Hivyo Ethiopia ni mtu aliyeungua uso kwa maana nyingine ni mtu mweusi, na katika historia ya kale watu walioandika sana kama Herodotus, Appolodorus, Marcellinus na Josephus wanasema kuwa watu weusi walikaa mashariki ya kati, Misri, Sudan, Ethiopia, Visiwa vya bahari ya meditteranea na Afrika Kaskazini. Haya yote yalizungumzwa na wanahistoria katika kikao cha UNESCO ambapo tamati haikufikiwa. Japo kwenye Biblia kitabu cha Yeremia 13:23 Mungu aliuliza kwamba Je, Mkushi/Ethiopia anaweza kubadili rangi yake ya mwili? Hili linathibitisha kwamba katika historia kulikuwa na watu weusi na walikuwa wana mchango mkubwa sana kwenye dunia. Herodotus katika maandishi yake aliwaelezea wanaume weusi "Ethiopians" kama watu warefu, wazuri wa sura na wenye nywele ngumu. Lakini leo kuna nchi ya Ethiopia ambayo watu wake wamijiita hivyo kutokana na mandhari ya kihistoria.
Neno Misri katika historia linaonyesha kutumika kimakosa. Kwanza Katika dunia ya kale Wamisri waliita nchi yao "
Kemet" ambalo lilimaanisha ardhi nyeusi ya mto naili na pia eneo la watu weusi. Mwanahistoria Flavius Josephus ndiye aliyeelezea Historia ya Malkia wa Sheba ambaye alienda kumtembelea mfalme Suleimani. Huyu malkia wengi wanamuita Mekeda lakini pia katika lugha ya Amhara kuna kumbukumbu inayotoa jina lake jingine kama Birkis. Daktari wa Historia Windsor Rudolf anasema wafalme wengi japo siyo wote walikuwa na majina zaidi ya moja. Mfano Suleimani alipewa jina Yededia alipozaliwa lakini alipokuwa mkubwa aliapishwa kama Suleimani, au Mtoto wa mfalme Suleimani Menelik wa Kwanza alivyoenda kuapishwa Yerusalem alipewa jina Daudi kama babu yake. Hivyo isichanganye mtu kama Josephus alitumia Mekeda na Wengine wakamuita Birkis.
Tukirudi kwenye neno Misri, Wagiriki walilichanganya na jina la mji mkuu wa Kibiashara Misri kipindi hicho ulioitwa "Thebes" ambapo jina lake la pili uliitwa "Aigyptos" hivyo wafanyabiashara wengi waliuita Aigyptos na hivyo jina likakaa hadi kuitwa Egypt. Mfano wa haya mambo hata leo hii upo, katika historia ya Tanganyika hatujawahi kuwa na kabila la Wahehe lakini kutokana na Wajerumani kukosea kabila la Wahehe likazaliwa mpaka leo hii lipo. Au Sehemu kama Tosa-Maganga mkoani Iringi kumtokana na makosa ya wageni kuandika kile walichokisikia wenyeji wakisema. Hivyo Dola la Kale la Misri liliitwa KEMET (Nchi ya Nile Nyeusi au nchi ya watu weusi)
MUHIMU: Tujifunza kitu muhimu, kwamba katika historia siyo kila mtu ambaye alikuwa ni Mwarabu alikuwa ni mwarabu mweupe wa leo hii, na pia siyo kila Mwafrika alikaa hapa Afrika, tukifika huko mbele tutona jinsi ambavyo kulikuwa na muingiliano mkubwa katika hivi vizazi. Mfano mzuri ni kwamba Misri ya leo hii siyo Misri ya zamani kwasababu imetawaliwa na watu wengi tofauti kwa vizazi vingi. Daktari Ivan Van Sertima anasema kwamba kama ilivyo leo Marekani ambayo ilikuwa nchi ya Wahindi wekundu ndivyo ilivyo leo Misri. Kwamba Wenyeji ambao ni Wahind wekundu ni wachache kuliko wahamiaji kutoka barani Ulaya. Hivyo naomba tuvumiliane maana mwishowe nitaweka kila kitabu nilichokisoma na kukifanyia kazi ili wale wanaopenda kusoma wapitie wenyewe na wachambue kipi ni kweli na kipi siyo ukweli.
TUTAENDELEA HIVI PUNDE.................................................
B: MWANZAO WA VIZAZI VYA BINADAMU KUTOKA KWA NUHU.
CC: KENZY , Hoshea , R Mbuna , binjo , Luggy