Habarini za mchana bandugu, natumaini nyote wazima wa afya telee.
Nadhani mutakuwa mmeelewa head inavyosomeka.
Kwanini, mtu mweusi hususani mtanzania hupenda kuongea kiswahili na kupitishia kiingereza, wakati anaeongeanae ni mtanzania mwenzie ama mswahili mwenzie!! Kwanini Mzungu anaongea lugha yake bila ya kupitishia kiswahili ambacho sisi wenyewe waswahili wenye lugha yetu hatukithamini na kuthamini lugha ya kiingereza! Hii kitu inakera sana bandugu, mtu anacomenti kisha anachomeka na Kiingereza wakati mzungu hana huo ujinga., tusiende mbali, humu humu tunao wengi.
Sasa sijajua, je ni ushamba unamsumbua mtu huyu? Au aonekane anajua kiingereza, ama ujinga ndio unampelekea kufanya ivyo!
Kwa staili hii tutaendelea kuwa watumwa wa mabeberu.