Mtu Mweusi ataendelea kuwa mtumwa wa Mabeberu, huu ndio ukweli wenyewe

Sol de Mayo

JF-Expert Member
Sep 10, 2016
6,194
5,781
Habarini za mchana bandugu, natumaini nyote wazima wa afya telee.

Nadhani mutakuwa mmeelewa head inavyosomeka.

Kwanini, mtu mweusi hususani mtanzania hupenda kuongea kiswahili na kupitishia kiingereza, wakati anaeongeanae ni mtanzania mwenzie ama mswahili mwenzie!! Kwanini Mzungu anaongea lugha yake bila ya kupitishia kiswahili ambacho sisi wenyewe waswahili wenye lugha yetu hatukithamini na kuthamini lugha ya kiingereza! Hii kitu inakera sana bandugu, mtu anacomenti kisha anachomeka na Kiingereza wakati mzungu hana huo ujinga., tusiende mbali, humu humu tunao wengi.

Sasa sijajua, je ni ushamba unamsumbua mtu huyu? Au aonekane anajua kiingereza, ama ujinga ndio unampelekea kufanya ivyo!

Kwa staili hii tutaendelea kuwa watumwa wa mabeberu.
 
...shule ya msingi kiswahili
... o'level na A level kingereza
....Chuo english & swahili

Acha tuu tuwe machotara wa lugha hivihivi..
 
Mkuu, huna sababu ya kulaumu mtu, shida ipo hapa; elimu zetu zote za juu watu tunatumia kiingereza sasa utakuta mtu anazoeshwa maneno ya kiingereza, hii ni tofauti na wazungu ambao wengi hutumia lugha zao za asili katika kufundishia, au wewe umesikia muingereza au muanerika akitumia lugha nje ya kiingereza katika kufundishia?? au mjerumani au mjapani, mrusi nk, wote hao hutumia lugha zao kufundushia.

Shida ipo katika mifumo ya elimu zetu na shida hii ipo kwa wahindi nk, ambao nao hutumia kiingereza katika kufundishia, ni ngumu kumsikia Muhindi akiongea kihindi pekee bila kuingiza kiingereza kidogo.

Dawa yake ni; tuachane na kiingereza kama lugha ya kufundishia na tutumie kiswahili toka chekechea hadi vyuoni.

Je jambo hilo linawezekana??!;
 
Sasa mzungu lini kajifunza Kiswahili Hadi achomekee akiongea..Kwani wazungu wote wanaongea Kiingereza?
 
Kwanza lugha ya kiingereza ni lugha kuu duniani kama ilivyo kiswahili kuwa lugha kuu Tanzania wakati kuna lugha za makabila,watu wanaongea lugha za makabila yao huku wanachomekea na kiswahili.Si utumwa kuchanganya lugha mbili mara moja wakati mwingine huwa ni msisitizo zaidi
 
Badala Magufuli angeteua kwanza mawaziri wa Kilimo na Elimu. Anakimbilia wazir wa fedha na mambo ya nje hili tu kurahizisha kuombaomba mikopo na msaada
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom