Mtu mwenye Sura mbili ni yupi?

Mtu mwenye Sura mbili ni yupi?

realMamy

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2024
Posts
7,335
Reaction score
18,424
Mtu wa Sura Mbili ni nani?

Ni mtu mwenye maisha ya aina mbili. Uso mmoja wa kuonyesha watu, na uso mwingine wa kweli anaouficha.

Mbele ya watu ni malaika. Maneno yake ni kama asali. Anaweza kukushika mkono na kusema "mimi niko nawe 100%".
Lakini nyuma yako ndio shetani halisi anayekumaliza taratibu.

Huo huo mkono unashika kisu. Anapanga jinsi ya kukutoa, jinsi ya kuchafua jina lako, na jinsi ya kujenga mafanikio yake.

Na watu hawa hupatikana kila sehemu.
Mbele za watu hujifanya ni watu bora na wanyenyekevu,Lakini ndani ya kuta za nyumba ni dhalimu na wanyanyasaji.

Ofisini anapiga kelele za "tufanye kazi pamoja". Lakini usiku anapanga fitina za kuwamaliza wenzake.

Kwenye biashara anacheka nawe vizuri akisema "tuungane". Wakati huo huo anaenda kwa wateja wako kuwaambia wewe ni mwongo na bidhaa yako ni mbovu.

Lakini kumbuka hili: Kila mwenye sura mbili ana mwisho wake.

Kila mask ina tarehe ya kuisha. Kila uongo una saa yake. Siku moja mask itaanguka yenyewe. Siku moja watu watajua ni nani kweli.

Siku ikifika, hakuna cheo,pesa, wala hakuna unafiki utakaoweza kukuficha. Utaanguka kwa aibu kubwa mara mbili.

Chagua leo. Kuwa mtu Mkweli.
Kuliko kuwa watu wawili wa uongo ambao mwishowe utabaki peke yako.

Je Umewahi kukutana na mtu wa aina hii wapi? Nyumbani, kazini au kwenye biashara?
 
Nimekutana na mtu wa aina hiyo hapa hapa JF,
Anaitwa Binti wa zamani
Siamini kama hii jumapili takatifu mimi nimeitwa shetani.

reality tv shade GIF by Big Brother Canada.gif
 
Back
Top Bottom