Mtu kapigwa risasi Mlimani City Dar es salaam

Huu mtindo wa kushika bahasha za hela waziwazi wakihisi hawahulikani ndio unao waponza wabongo wengi,hata pale posta huwa nawaonaga wengi sana na vibahasha vyao nabaki kunichekea tu...

Mtu hivyo alikuwa anakiita kifo haina hja ya kumuonea huruma...

Kova alishachanganyikiwaga na hizo Boxer hataki hata kuzisikia

Mkuu ujue mm hua naogopa tu kutoa lawama kwa marehemu wanao uwawa kwa kubeba hela kizembe then wanalaumu polisi eti hawafanyi kazi.
Tuwe watu wa kuelewa jamani ingawa kifo kipo tu but wengine tumezidi uzembe. Acheni unafiki watu wengine wanajitakia kufa. Utabebaje 18m kwenye kibahasha dunia ya leo?
Ni mazoea au kujisahau ila vyovyote vile kama mpaka leo hujui ujambazi na hatari ya kubeba hela nyingi ovyo or routinely basi subiri kifo anytime na u silaumu mtu.
 
Mkuu yawezekana uko sahihi lakini tatizo ni kwamba wanakuwa na wewe tokea bank, hivyo hata uzibandike gundi mwilini wao watazitaka. Wafanyakazi wa mabenki wengi siyo waaminifu kabisa wanashirikiana na majambazi, ukiwa unadraw pesa nyingi kisha ghafla teller anashika simu yake anambeep jambazi kuwa kuna mteja "mkubwa". Ukitoka uko nao hadi wazipate.

Jambo la msingi inapotokea hali hii ilitakiwa teller aliyemhudumia simu zake zichunguzwe. Pia iwe ni marufuku teller kuwa na simu awapo counter. Hizi counter ziwekewe tinted hata kwa mteja ili wateja wengine wasijue kiasi anachochukua yule aliyepo counter.





Anatoka mkoa wa Mbeya

Huyu hakutoka bank. Ametoka kuzichukua sehemu ya biashara yake. Kimsingi ukiwa unatabia au upo mazingira ya kubeba hela ndefu lazima ujue precautions zote za uchujuaji hela hizo kuanzia kwa mkeo mpaka wafanyakazi wako na marafiki.
Vinginevyo utapigwa risasi tu cku moja.
 
Dah hii ni noma kwakweli, polisi sijui wanafanya nini??

Polisi kazi yake ni kukulinda wewe na mali zako.

Je,alikwenda kituoni kuomba ulinzi azifikishe pesa zake benk salama bila kupigwa risasi na kufa?!.....HAPANA hakwenda kwasababu anajiamini ona sasa kilichomkuta
 
Wapo mkuu na wanafanya kazi kweli kweli!
Nilikuwa nafuatilia clips ya ITV habari jana ikimuonyesha kamanda Kova alivyojipanga kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama kuhakikisha ukaaji wa wazee wastaafu wa mpira kutoka Ulaya na Ufaransa wanakula holiday yao kwa amani bila bugudha.

Atafadhali, atakayetuwekea hiyo clip nitampatia 'like' 10,000.

Ngoja niitafute
 
Nyerere alipambana na kuwaacha Maadui watatu kaongezeka huyu wa nne ujambazi. Kinachonisikitisha ni kuwa huyu ni zao la umasikini. Hii nchi inaelekea wapi bandugu?
Bandugu, Maadui wanaongezeka kwa kasi, Takwimu inadhihirisha kuwa hulka ya wa Tanzania ni watu wanahofu kifo(woga) lakini wamekubuhu katika uhuni,wizi,umjambazi,mkahaba,ulevi wa kupindukia !! Kazini hawadumu zaidi ya saa 3 hadi 4 kuwajibika.!!
Chunguza na utafiti utahakikisha ukweli huu !! Mungu tusamehe Tanzania.
 
18mils ndogo?!u cant be serious kibongobongo?!!
watu wamepinda asa hv wanaua kwa milioni 2.....!!!
mi nahisi deal limeanzia kwa watu wake wa karibu from nowhere haiwezekani tu wamfate na kumuua only him
Sasa fanya dili limeanzia kwa watu wake wa karibu,
Inamaana huo mgao utakua na watu wengi tayari,unakwenda jela maisha kwa pesa mbuzi namna hiyo,na mara nyingi huwa wanadhulumiana.
 
RIP ADSON.
Kupata ajira ni ngumu sana, ukisema ujiajiri kihalali mazingira yake magumu, na wasomi Kila siku wanaongezeka, mwisho wake watu wanajiajiri kwa njia haramu kama Hizi. Kuaminiana kwenye jamii kunapungua Kila siku.....
 
Ni nyingi kwao hizo. Tukisema bongo si salama tena hamtaki,
Jamaa anaonekana smart sana. Imekuaje kahatarisha uhai wake kutembea na bahasha yenye pesa?
Vifo vingine vinazuilika bana

Mkuu ni ulimbukeni tu,hizo sio pesa nyingi za kugharim maisha ya mtu,Kuna wamama Wacongo na Wazambia wanatembea na pesa cash mpaka zaidi ya dola laki na nusu na mtu huwezi kuwadhania,
Itakua ni mtu wake wa karibu mwenye akili fupi ndio kamchoma,na ata kamatwa tu kama ndugu wataamua kufwatilia.
 
Acha kuilau serikali hata kwa uzembe wa makusudi, unabeba hela nyingi kwenye bahasha unategemea nn? Na je ni gani ina usalama kwa asilimia zote? Niambie ni inchi gani haina matukio ya uhalifu duniani, maisha unayoyataka kwa duniani huwezi ata, labda ufe Wacha 1
 
Last edited by a moderator:
Halafu wakikamatwa wakachomwa moto kuna mijitu inajifanya kuwatetea! RIP Cheyo!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Mkuu, kuna madai kuwa eti polisi wanakuwa "well adviced" na hawa maharamia!Yaani ni "deadly brutal combination of two frontiers- the bandits and the police.

This combination is very scary and dangerous.

Hata ishu ya millenium towers inasemekana wako well informed.malalamiko ya baadhi ya wanausalama kushirikiana na wahalifu ni mengi.unakuta ndani ya mtandao unahusisha staff wa benki,polisi,walinzi,madereva magari na boda boda.umezingirwa kila kona.jeshi letu lijipange kupambana na organized crime.ni wizi mbaya na mgumu kuzuia.inabidi hadi polisi wenyewe wajichunguze.hao polisi jamii na sungusungu ndio kabisaa.wamegeuka wachora rada kwa wahalifu.
 
Acha kuilau serikali hata kwa uzembe wa makusudi, unabeba hela nyingi kwenye bahasha unategemea nn? Na je ni gani ina usalama kwa asilimia zote? Niambie ni inchi gani haina matukio ya uhalifu duniani, maisha unayoyataka kwa duniani huwezi ata, labda ufe Wacha 1

Wewe hufikiri nje ya box... hivyo huwezi kuona correlation kati ya UJAMBAZI na SERIKALI DHAIFU! Hata kama hakuna ''inchi'' (nchi) nje usalama kwa asilimia mia moja lakini vilevile HAIKUBALIKI watu wauawe kama wadudu..... Serikali ipo KUWALINDA raia wake BILA KISINGIZIO. Wewe unafikiri hata watu wakiacha kubeba fedha nyingi kwa hali ilivyo hapa Tanzania (jeshi la polisi lilivyooza na serikali ilivyojaa wavivu na wezi)ndio ujambazi utaisha? Sana sana watatafuta targets nyingine, ikibidi kuteka nyara na kudai ransom kwa nguvu.
 
uombe escot ya police kwenda bank wkt kuna police wanasaliti jeshi?unaweza kuhisi uko salama kwa ulinzi kumbe wenzio wanakulia ramani.wanakuwa washawasiliana na wazee wa boxer kitambo.kifupi kwa ss hakuna police Bali kuna wasaliti
 
polisi wa pikipiki niko nae hapa ananiuliza leseni na tri angle ahahaaa kashika bunduki wanaume wanaua watu.hivi tukiulizana hawa polisi wenye pikipiki wameshawahi kukamata jambazi hata mmoja?
 
Back
Top Bottom