Ujambazi Mlimani City

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,800
34,189
UJAMBAZI MLIMANI CITY

Wadau, habari za jioni

Hapa maeneo yetu kuna msiba umetokea. Marehemu ameuwawa na majambazi. Alichukua fedha (milioni 10) kutoka Benki mojawapo hapa Mlimani City na kuanza safari ya kuelekea huko Salasala ambako alikuwa na shughuli ya ujenzi inayoendelea. Majambazi walimfuata kwa nyuma, walimpita na kumzuia kwa mbele. Majambazi walimtaka atoe 10M aliyochukua Benki kabla ya kumpiga risasi. Walikuwa wanafahamu kiasi halisi kilichochukuliwa!

Siku kama 5 kabla ya tukio hili, tukio lingine lilitokea eneo la Bamaga (mkabala na Hongera bar). Mtu na mke wake walichukua fedha toka benki hapo Mlimani City (13m). Majambazi walimfuata kuanzia hapo Mlimani city hadi huko Bamaga na kumtaka awape fedha. Kumbe alikuwa amezitenganisha; aliwapa laki 5 lakini walipatwa na hasira na kuhoji fedha nyingine ilikuwa wapi. Walimpiga risasi begani. Mke wake akawaongezea laki 1; naye alijeruhiwa kwa risasi wakidai "tunataka milioni 13 zote". Pona yao ni kuwa fedha walikuwa wameificha kwenye booth. Baada ya kuona muda unapita majambazi wakaondoka. Na kwa bahati nzuri majeruhi walipona. Cha kushangaza ni kuwa majambazi hawakujifunika nyuso zao wala hawakuwa na wasiwasi wa kujificha hata kidogo.

Huko nyuma, jirani yetu mmoja (Mama-Joshua) alichukua milioni 4 hapo hapo Mlimani City. Baada ya kufika kwa Kakobe, majambazi walimpita na kumsimamisha baada ya kujifanya kuwa wanamjua. Baada ya kusimama walimtaka awape "awape mzigo aliochukua benki". Hivyo:
1. Mlimani city ni eneo hatari sana kwa ujambazi;

2. Inaelekea wafanyakazi wa Benki wanashirikiana na majambazi. Hivyo, kitendo cha wewe kwenda kuchukulia fedha ndani ya benki (bulk cash room) hakiwezi kuwa ni cha siri;

4. Epuka kuchukua fedha nyingi benki. Fanya malipo kupitia benki au njia nyingine mbadala;

4. Kama una ujenzi, ni hatari kuwa na kawaida kuwapelekea mafundi fedha kwenye site; tumia M-pesa, tigopesa, nk.

5. Kama umechukua fedha, usikubali kusimamishwa na mtu usiyemjua njiani isipokuwa kama wameku-block na huna jinsi ya kukwepa.

Mjulishe rafiki, ndugu na jamaa kuhusu changamoto hii ya kiusalama.
 
HAYA MATUKIO YANASIKITISHA SANA YAANI PALE PATANGAZWE KUWA NI ENEO HATARISHI NA BANK ZOTE SIJUI ZIFUNGWE MITAMBO GANI KWA SABABU MATUKIO NI MENGI HAYO KAKA NI 1% YA MATUKIO YA WATU KUPOTEZA MAISHA BAADA YA KUCHUKUA PESA HAPO MLIMNANI KWA NN KUSIWE NA CCTV ROOM KUCHUNGUZA WATU WANOKAA PALE SIKU NZIMA ETI WANAPIGA STORI .KWELI SERIKALI IMEWEKA PAMBA MASIKIONI MPKA NANI AFE NDO WASIKIE HICHI KILIO
 
Heavy parking ile ni maficho ya majambazi yenye mitego ya kila kona washirika wao wa kuingia pale kuchota pesa, na wahudumu nao ni vibaraka bila shaka iweje uthibitishe kiasi halisi cha kupora, hesabu hiyo umeipataje!? Cashier wanahusika sna.
 
hawa watu ( majambazi ) wawekewe mtego wa kukamatwa alafu wawataje wanaoshirikiana nao. maana sasa uhuru na amani kwa wateja wa hizo bank hapo umepungua. huu ni ushahuri wangu kwa vyombo vya ulinzi
 
Mmmmh hiii hatari. Nashauri usibebe kiasi kiasi kikubwa cha fedha,
Ni vema ufanyie biashara yako bank.
Mfano, kama unanunua kiwanja mshauri muuzaji apokelee pesa bank kwa usalama wenu wote
 
Wahudumu wa bank ni wahusika wakubwa wa matukio ya wizi pale mlimani city. Haiwezi tokea mtu frm no where akaja akakuambia toa kiasi flan kma hajaambiwa na mtu aliyekukabidhi hiyo hela. CASHIA WA BANK ZA MLIMANI CITY NI JIPU KUBWA LINALOSUBIRIA KUTUMBULIWA.
 
Katika uchunguzi wa juu juu hii inaonekana kwa asilimia 100 wafanyakazi wa mabenki wana mtandao unaohusika na huu ujambazi. Mimi nitaenda mbali kidogo kuwalaumu Benki kwa kuwa wazembe kwenye kuchukua hatua za kiusalama na kulinda wateja wao. Kuna kifaa kinaitwa HPMPJ (High Power Mobile Phone Jammer) ni kifaa kinachotumika kukata network ya simu au kifaa chochote cha mawasiliano unapoingia kwenye range frequency. Kwa watu wanaoenda Bank M watanielewa,maana ukiingia kwenye Bank zao simu huwa inapoteza network. Serikali ingeweka sheria ya lazima kwa Mabenki kufunga vifaa Kama hivi na kuchukua hatua madhubuti kuhakikishia wateja usalama.

Haya matukio yamezidi sana na hatua za msingi zisipochukuliwa Itakuwa mbaya sana siku za mbeleni.
Benki zingepiga marufuku wafanyakazi wake kutumia simu muda wa kazi. Ikiwa wanahitaji kutumia simu watumie za mezani/ ofisini ambazo ziko monitored na Benki.
Wafanyakazi wa Benki wanatakiwa kufanyiwa extensive Backgroung check for security clearance. Na nyendo zao zifuatiliwe kwa ukaribu.
Nafikiri pia muda umefika kwa serikali yetu tukufu iruhusu ( Private Investigators) kwenye taasisi za fedha.
Kwa Leo nitaishia hapa.
 
Nice thoughts
 
Kuna sehemu tatu hapa, mfanyakazi wa benki, mteja aliyechukua pesa na jeshi la police (serikali).

Mfanyakazi wa benki sio mwaminifu. Ni jambazi anayetumia ofisi yake kuua watu kwa tamaa ya pesa. Benki ziangalie namna zinavyoajiri watu hasa fresh graduates. Na pale na limit ya kutumia private phones kwa wafanyakazi muda na eneo la kazi.

Aliyechukua pesa benki anatatizo. Na technology yote hii ya mobile money, cheques kuna sababu gani ya kumlipa mtu cash? Kama ni pesa nyingi lipia benki. Kama ni hizi za kawaida tumia mobile money. No reason kubeba milion zaidi ya 10 cash. No reason. Ni risk.

Police (serikali) haijawajibika vya kutosha kudhibiti ujambazi wa bei rahisi kiasi hiki. Armed robbery inakuwa organised. Sasa tulisajiri simu za nini kama bado watu wanasajiri simu na wanazitumia kufanya uhakifu bila wasiwasi wowote?

Mwisho, usalama unaanza ma mtu binafsi. Siri iwepo kuhusu miamala yako. Kama una fundi site mlipe kwa simu na si cash. Hao ndio wanaochoma kuwa unatembea na cash.
 
UJAMBAZI MLIMANI CITY

Wadau, habari za jioni

Hapa maeneo yetu kuna msiba umetokea. Marehemu ameuwawa na majambazi. Alichukua fedha (milioni 10) kutoka Benki mojawapo hapa Mlimani City na kuanza safari ya kuelekea huko Salasala ambako alikuwa na shughuli ya ujenzi inayoendelea. Majambazi walimfuata kwa nyuma, walimpita na kumzuia kwa mbele. Majambazi walimtaka atoe 10M aliyochukua Benki kabla ya kumpiga risasi. Walikuwa wanafahamu kiasi halisi kilichochukuliwa!

Siku kama 5 kabla ya tukio hili, tukio lingine lilitokea eneo la Bamaga (mkabala na Hongera bar). Mtu na mke wake walichukua fedha toka benki hapo Mlimani City (13m). Majambazi walimfuata kuanzia hapo Mlimani city hadi huko Bamaga na kumtaka awape fedha. Kumbe alikuwa amezitenganisha; aliwapa laki 5 lakini walipatwa na hasira na kuhoji fedha nyingine ilikuwa wapi. Walimpiga risasi begani. Mke wake akawaongezea laki 1; naye alijeruhiwa kwa risasi wakidai "tunataka milioni 13 zote". Pona yao ni kuwa fedha walikuwa wameificha kwenye booth. Baada ya kuona muda unapita majambazi wakaondoka. Na kwa bahati nzuri majeruhi walipona. Cha kushangaza ni kuwa majambazi hawakujifunika nyuso zao wala hawakuwa na wasiwasi wa kujificha hata kidogo.

Huko nyuma, jirani yetu mmoja (Mama-Joshua) alichukua milioni 4 hapo hapo Mlimani City. Baada ya kufika kwa Kakobe, majambazi walimpita na kumsimamisha baada ya kujifanya kuwa wanamjua. Baada ya kusimama walimtaka awape "awape mzigo aliochukua benki". Hivyo:
1. Mlimani city ni eneo hatari sana kwa ujambazi;

2. Inaelekea wafanyakazi wa Benki wanashirikiana na majambazi. Hivyo, kitendo cha wewe kwenda kuchukulia fedha ndani ya benki (bulk cash room) hakiwezi kuwa ni cha siri;

4. Epuka kuchukua fedha nyingi benki. Fanya malipo kupitia benki au njia nyingine mbadala;

4. Kama una ujenzi, ni hatari kuwa na kawaida kuwapelekea mafundi fedha kwenye site; tumia M-pesa, tigopesa, nk.

5. Kama umechukua fedha, usikubali kusimamishwa na mtu usiyemjua njiani isipokuwa kama wameku-block na huna jinsi ya kukwepa.

Mjulishe rafiki, ndugu na jamaa kuhusu changamoto hii ya kiusalama.
6.Kila ambaye ameibiwa kwa style hii atengeneze matangazo kumi ya jinsi walivyoibiwa na kwamba wafanyakazi wa hiyo benki ni suspect then hayo matangazo yabandikwe maeneo mbalimbali jijini ikiwemo hapo mlimani city ili ulimwengu ujue.
 
Back
Top Bottom