Mtu binafsi anaweza kumiliki nyumba ya ibada?

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,214
3,587
Kwanini Mkristo anaweza kumiliki Kanisa/Huduma lakini Muislamu hawezi kumiliki Msikiti, Mhindu hawezi kumiliki Jamatini, M-Bahai hawezi kumiliki Hekalu wala Myahudi hawezi kumiliki Sinagogi?

Kuna nini kwenye Ukristo? Mitume wa Nyakati za Biblia wala Wanafunzi 12 wa Yesu Kristo hawakumiliki Hekalu wala Kanisa. Sisi leo tumetoa wapi hii kitu?

Nadhani serikali ibadili sheria ili Makanisa yasisajiliwe na Msajili mmoja huyo huyo wa kusajili NGOs.

Lakini pia kusiwepo na mtu binafsi au familia au ukoo kumiliki Kanisa/Huduma ya MUNGU.

Mke wa TB Joshua anaendelea kukalia kiti cha mumewe.

Margaret mke wa Bishop Benson Idahosa (Baba wa Upentekoste Nigeria) ameendelea kumiliki Church of God Mission International.

Elizabeth Moses Kulola hajamiliki EAGT.

Evergrace Emmanuel Lazaro kabla ya kutwaliwa nyuma ya kutwaliwa mumewe hakumiliki TAG.

Mazonge kwenye kazi ya MUNGU ni kushindwa kupeleka waumini Mbinguni.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Unauliza jibu mkuu, ukiona mtu kama Masanja Mkandamizaji na macomedian wengine wana makanisa juwa hapo kuna uwalakini tu. Kanisa la mtu binafsi ni changa la macho tu na bahati mbaya waumini wao nao wamefungwa macho na akili.
 
Hakuna na hakutakuwa na kanisa la mtu binafsi. Kwenye usajili wa makanisa ni lazima kuwe na "board of management" hapa ndipo tunapata "board members". Hiki kuita kanisa la Masanja ni just identification ya Kanisa lakini Masanja au Lusekelo hajawahi kuwa wala kumiliki kanisa. Kuna timu ya watu ndani ya kanisa wanaosimamia Kanisa.

Mfano, suala la TB Joshua, baada ya mauti yake Kanisa lilikuwa chini ya board member na mkewe hakuwa miongoni mwa board member so kwa kuwa kulikuwa na waumini wengi na kanisa lilikuwa na ukwasi, mama akapambana ili awe kiongozi wa kanisa na sio mmiliki.

Makanisa yote ya kimfumo from TAG hadi Roman kuna hiyo board member. Hata hizi huduma za sasa ili zisajiliwe kisheria lazima ziwe na mebers of the board au management team mkuu ila hao wachungaji/mitume/manabii n.k wao wanakuwa viongozi wa madhabahuni tu na ndio maana WRM ya Suguye ilifungwa kwani alikosa "board of trustee"
 
Eti dini ya haki, kwamba kuna majini wazuri na majini wabaya, ukifa unapewa mabrikra 72
Screenshot_20230830-084424.jpg
 
Back
Top Bottom