Viongozi wa dini waumbuana juu ya uuzaji wa dawa za kulevya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wa dini waumbuana juu ya uuzaji wa dawa za kulevya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by tufikiri, Jun 20, 2011.

 1. t

  tufikiri Senior Member

  #1
  Jun 20, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na Mwandishi Wetu
  Mchungaji wa Kanisa la Full Salvation, Christopher Mtikilla ‘ameifungukia’ kauli ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa, baadhi ya viongozi wa dini nchini wanajihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya, Ijumaa Wikienda linashuka naye.

  Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu Ijumaa iliyopita, Mtikilla alisema tamko la JK ni la kweli kwa vile wapo baadhi ya viongozi wa dini wasiofuata maadili ya kazi yao na kufanya biashara hiyo. Akaongeza kuwa, yeye anamjua mmoja (jina tunalo).

  “Rais alisema kweli, wala wasipinge. Kama kuna kiongozi yeye hafanyi biashara hii, ajue kuna wenzake wanafanya,” alisema kwa kujiamini Mtikilla.

  Aidha, Mtikilla ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha DP, alimtaja mchungaji mmoja wa kanisa la kiroho la jijini Dar es Salaam ambaye ana waumini wengi kuwa, na yeye anafanya biashara hiyo na watu wengi wanajua.

  “Mfano…(akamtaja jina) yule ni mfanyabiashara wa haya madawa, nani asiyejua bwana. Huyu na wenzake wengi ndiyo siri nzito ya kuwa matajiri wakubwa kwa sababu ya fedha haramu.”
  Pia, alisema kuwa, mchungaji huyo alidakwa na madawa miaka ya karibuni, baadhi ya viongozi hao wa dini walisikia, lakini akahoji, “ni kwa nini hawakutoa tamko?”
  Mchungaji Mtikilla aliongeza kuwa, haoni sababu ya viongozi wa Baraza la Maaskofu Tanzania kumkomalia JK kuweka hadharani majina ya viongozi wa dini wanaojihusisha na madawa ya kulevya.

  Akahoji: “Mbona kuna maovu mengi yanayofanywa na viongozi wa dini ikiwemo ubakaji, ulawiti, utapeli na ushirikina lakini baraza halitoi tamko lolote?

  “Kila mmoja ana mapungufu yake, serikali kuna mahali inakosea kwa sababu suala hili siyo la kulizungumzia kwenye majukwaa bali kama wapo wanaotuhumiwa, wakamatwe na uchunguzi wa kina ufanyike ili sheria ichukue mkondo wake.
  “Pia viongozi wa dini wanakosea sana kutoa tamko dhidi ya rais. Hakuna sehemu ambapo maandiko matakatifu yanawataka kutumia jazba kukabili changamoto wanazokutana nazo.
  “Kama kiongozi hafanyi haya, ajue kuna wenzake wanajihusisha na michezo isiyofaa, ikiwemo hili la biashara ya madawa ya kulevya. Tuache kuteteana na kujificha nyuma ya mwavuli wa dini. Siku hizi wengi hawaaminiki, wanajali fedha kuliko huduma ya kuchunga kondoo wa Bwana,” alisema Mtikila.

  Wiki mbili zilizopita, katika hafla ya kumsimika Askofu John Ndimbo wa Kanisa Katoliki, Mbinga, Ruvuma, Rais Jakaya Kikwete alisema kuna baadhi ya wachungaji wanaojishughulisha na biashara ya madawa ya kulevya.
  Alisema watumishi hao wa Mungu wamekuwa wakitumia nafasi zao kwenye paspoti kuingiza au kutoa madawa ya kulevya.

  Ndipo maaskofu wanaounda Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) walipokutana Juni Mosi, mwaka huu mjini Dodoma chini ya Mwenyekiti, Mchungaji Peter Kitula na kumpa saa 48 Rais Jakaya Kikwete kuwataja kwa majina viongozi aliodai wanafanya biashara hiyo haramu.

  Viongozi wengine wa dini wanaounda jumuiya hiyo ni Askofu Valentino Mokiwa (Anglikana, pia ni Kaimu Mwenyekiti), Alex Malasusa (KKKT) na Moses Kulola (EAGT).
  Wengine ni maaskofu kutoka makanisa ya Moravian, African Inland, Baptist Tanzania, African Brotherhood, Church of God na Kanisa la Biblia.
  Makanisa mengine yaliyopo kwenye Jumuiya hiyo ni Mbalizi Evangelist, Mennonite, Presbyterian, Salvation Army na Tanzania Yearly Meeting.
  Miaka ya karibuni, kumekuwa na baadhi ya wachungaji wa kiroho wanaolalamikiwa na baadhi ya waumini wao kwa kuwa na utajiri mkubwa.

  Waumini hao wamekuwa wakiwatuhumu wachunga kondoo wao kuwa, wanamiliki mamilioni ya fedha, magari ya kifahari, nyumba za kisasa huku wao, wakiwa kama kondoo, wanaishi maisha ya ufukara wa kutupwa.

  Hata hivyo, uchunguzi wa kina wa gazeti hili umebaini kuwa, baadhi ya wachungaji nchini, wanashindana kumiliki magari ya bei mbaya huku baadhi ya kondoo wao wakishindwa kulipia kodi ya chumba cha shilingi elfu thelathini (30,000/=) kwa mwezi.
   
 2. Ta Kamugisha

  Ta Kamugisha JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 3,003
  Likes Received: 1,077
  Trophy Points: 280
  Duh! hii kali, ebu mwaga jina la uyo mchunga kondoo. maana wengne wanaendesha hammer.
   
 3. S

  Smarty JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 729
  Likes Received: 149
  Trophy Points: 60
  asante kwa taarifa!!
   
 4. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #4
  Jun 20, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hii nchi tuna kazi sana habari za uzushi utazijua tu, tangu lini EAGT ikawa mwanachama wa cct??
   
 5. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #5
  Jun 20, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,011
  Trophy Points: 280
  kama majina yanatajwa na sheria hazichukui mkondo wake, nani alaumiwe? Huu ni ushahidi wa serikali dhaifu, na kwa kawaida serikali haiwezi kuwa dhaifu ila na yenyewe kuhusika na maovu kwanza. Maovu yake ndio yanayoikosesha ujasiri wa kuzingatia sheria.
  Rais mwenye dola kuweza kuwashughulikia waovu wote naye yupo majukwaani akilalama, kama wafanyavyo wale wasio na dola.
  Hii ni aibu ya karne!.
   
 6. Mkenazi

  Mkenazi Senior Member

  #6
  Jun 20, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 124
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Moses Kulola (EAGT) yuko chini ya PCT (Pentecostal Council of Tanazania) na wala sio CCT
   
 7. VUVUZELA

  VUVUZELA JF-Expert Member

  #7
  Jun 20, 2011
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Huu ndio ujinga wa nchi hii eti majina mnayo lakini hayatajwi.
  Magazetini (jina linahifadhiwa)
  Mtikila(jina ninalo)
  Kikwete (wajitokeze wenyewe)
  This is crap!
  Kama hamuwezi kutaja majina basi mkae kimya
   
 8. Nzowa Godat

  Nzowa Godat JF-Expert Member

  #8
  Jun 21, 2011
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 2,630
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Kwa nini vita na uhalifu
  vimezagaa kila mahali bila
  sababu za msingi ?
  BIBLIA INAJIBU HIVI:
  "Kisha aliwaambia, Taifa
  ...litaondoka kupigana na taifa,
  na
  ufalme kupigana na ufalme".
  Luka 21:10.
   
 9. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #9
  Jun 21, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,011
  Trophy Points: 280
  Sababu za msingi zipo. Hizi hapa 2Timoth 3:1-8.
   
Loading...