Mtu akifa anaenda wapi?

Mtu akifa anaenda wapi?

unazungumziaje waumini kuwa waovu na wasio waumini kutokua waovu -- unaonaje mkuu?
Huna sababu ya kuwa na wivu nao.!

Mtu anaposhikamana na imani maana yake anahitaji kulishwa kitu, si mbaya

Wewe usie na sababu ya kushikamana na hivyo, ndio tuendeleze tulipoishia, shida nini.?
 
Vita vipo ,mauaji kila kona , ukatili bado umejaa mpaka makanisani, ufisadi wa kutisha , na wanaofanya ndio wana hizo hofu za jehanam ,je imesaidia kitu gani ? Nchi ambazo hawaamni hizi mambo kwa kiasi kikubwa kuna utulivu mkubwa, unajua hilo?
Nafahamu kwa kiasi chake ila ningependa unifahamishe siri yao
 
Nafahamu kwa kiasi chake ila ningependa unifahamishe siri yao
Ukishakua nnje ya imani una kuwa na fikra huru , imani nikama gereza la matumizi sahihi ya akili ,hivyo unaweza fanya upumbavu wowote for the sake of so called imani.
 
Ongezeko la maji ya bahari ndio uelekeo wa kupotea ufu wa mtu, na kuendelea ktk maisha mapya! Mimi mwenyewe sijui lkn kwa Imani ya budha
 
Ukishakua nnje ya imani una kuwa na fikra huru , imani nikama gereza la matumizi sahihi ya akili ,hivyo unaweza fanya upumbavu wowote for the sake of so called imani.
Haya tutoke gerezani, na upuuzi wote

Tuwe huru kwa Dunia inayozalisha wajinga kila kukicha

Unadhani wakiachwa jinsi walivyo kwa dunia hii matendo yenye ukomo, lipi litakuwa na manuufaa.!?

Tumfanye binadamu awe huru ashibe aendekeze nyege, Baada ya muda anapambana na ongezeko lake na kuona hilo ni tatizo wakati Ufahamu wake unahusika zaidi.!

Kumfanya binadamu kuwa na hofu kwa asicho kifahamu Kuna faida zaidi kuliko maisha yake halisi
 
Ni sawa vitabu vimeandika kweli. Maneno ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli. Ila nakushauri pia usome na Quran yenyewe imeelezea kwa ufasaha sana safari ya roho na maisha baada ya kufa.
Quran imeelezea hata pale mtu anapokufa anaona nini na anapokuwa kaburini anakutana na nini.

Haya maisha baada ya kifo ni maisha ambayo sisi wanaadamu hatuyazingatii kabisa. Hatuyapi umuhimu wowote. Lakini kwa hakika kuna majuto makubwa sana baada ya kifo kwani mtu atayaona yale alyoyafanya hapa duniani na malipo yake ataonyeshwa.

Tujitahidi kutenda mema kwani hatujui siku wala saa
 
Swali hili limekuwa ni kitendawili kwa wanadamu wote: Mtu akifa, anaenda wapi?

Maandiko ya kale ya Henoko 22:18–26 yanatupa picha nzito ya safari ya roho baada ya kifo. Hebu tusome kwa pamoja:

18 Kutoka hapo nikaenda mahali pengine, mlima wa mwamba mgumu.

19 Na ndani yake palikuwa na mashimo manne, makubwa na mapana na laini sana. Mashimo hayo yalikuwa laini mno, makubwa na yenye giza kuonekana.

20 Ndipo Rafael, mmoja wa malaika watakatifu aliyekuwa pamoja nami, akaniambia:
“Mashimo haya yameumbwa kwa kusudi hili, kwamba roho za nafsi za waliokufa zikusanyike humu, naam, kwamba roho zote za watoto wa wanadamu zikusanyike hapa. Na mashimo haya yamefanywa kuyapokea hadi siku ya hukumu yao na muda wao uliowekwa, mpaka hukumu kuu juu yao itakapofika.”

21 Nikaona roho ya mtu aliyekufa ikileta malalamiko, na sauti yake ikaenda mbinguni ikiwasilisha kesi. Nikamuuliza Rafael malaika aliyekuwa pamoja nami:
“Hii roho inayowasilisha malalamiko, ni ya nani? Ni nani ambaye sauti yake inapaza kesi mbele ya mbingu?”

22 Akanijibu akasema:
“Hii ni roho iliyotoka kwa Habili, ambaye aliuawa na ndugu yake Kaini. Yeye anawasilisha kesi dhidi yake hadi uzao wake utakapofutwa kabisa juu ya uso wa dunia, na uzao wake uondolewe kati ya uzao wa wanadamu.”

23 Kisha nikauliza kuhusu hilo, na kuhusu mashimo yale yote:
“Kwa nini shimo moja limetengwa na lingine?”

24 Akanijibu akasema:
“Mashimo haya matatu yamefanywa ili roho za waliokufa zitenganishwe. Na mgawanyiko umewekwa kwa ajili ya roho za wenye haki, ambamo kuna chemchemi yenye maji angavu.

Na mgawanyiko umewekwa kwa ajili ya wenye dhambi wanapokufa na kuzikwa duniani, na hukumu haijatendeka juu yao wakati wa maisha yao.

25 Hapa roho zao zitawekwa kando katika mateso makubwa mpaka siku kuu ya hukumu na adhabu na mateso ya wale wanaolaani milele na malipo ya roho zao. Hapa watafungwa milele.

Na mgawanyiko umewekwa kwa ajili ya roho za wale wanaowasilisha malalamiko, wanaotoa ushuhuda kuhusu maangamizi yao, walipouawa katika siku za wenye dhambi.

26 Mgawanyiko pia umewekwa kwa ajili ya roho za watu ambao hawakuwa wenye haki bali ni wenye dhambi, waliokamilika katika makosa. Hao watakuwa marafiki wa wakosaji, lakini roho zao hazitauawa siku ya hukumu, wala hazitafufuliwa kutoka humo.”

Ufunuo wa Safari ya Roho Baada ya Kifo

Kulingana na Henoko, malaika Rafael alimwonyesha kwamba baada ya kifo, roho za wanadamu haziishi ovyo, bali zinakusanywa na kutenganishwa kulingana na matendo yao. Kuna mashimo manne makuu:

(a) Shimo la Wenye Haki

Roho za wenye haki hupumzika kwenye sehemu yenye chemchemi ya maji angavu.

Ni alama ya faraja, pumziko na tumaini la ufufuo wa uzima.

Yesu alisema: “Na uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.” (Yohana 17:3).

(b) Shimo la Wenye Dhambi Wasiohukumiwa Duniani

Hawa ni wale waliotenda maovu lakini hawakupata hukumu wakati wa maisha yao.

Roho zao zinawekwa kwenye mateso makubwa, zikitazamia hukumu ya mwisho.

Waebrania 9:27: “Na kama vile wanadamu wamewekwa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu.”

(c) Shimo la Waliouliwa kwa Dhuluma

Roho hizi zinatoa malalamiko na ushuhuda juu ya mateso yao.

Mfano ni Habili, ambaye damu yake ilililia haki mbele za Mungu (Mwanzo 4:10).
"Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi."

Hii inatufundisha kuwa Mungu husikia kilio cha wanyonge.

(d) Shimo la Wenye Dhambi Waliojaa Makosa

Hawa walikamilika katika uovu, waliishi maisha ya uasi wa kudumu.

Roho zao hazitafufuliwa tena, bali zitafungwa milele kwenye giza lisilo na tumaini.

Ufunuo 20:15: “Na mtu yeyote asiyepatikana ameandikwa katika kitabu cha uzima alitupwa katika ziwa la moto.”

Mafunzo Makuu kwa Maisha Yetu

1. Kifo si mwisho, bali ni mwanzo wa safari ya milele.

2. Mungu ni wa haki, kila dhuluma huangaliwa na hukumu yake huja.

3. Wenye haki na waovu hutenganishwa.

4. Yesu Kristo ndiye tumaini la uzima wa milele. Yohana 11:25: “Mimi ndimi huo ufufuo na uzima; yeye aniaminiye mimi ajapokufa ataishi.”

Kwa hiyo, mtu akifa haendi mahali pamoja kwa wote. Kuna mgawanyiko:

Wenye haki → pumziko na faraja.

Wenye dhambi → mateso na giza la milele.
usiumize kichwa ni kama ukifuta picha kwenye simu inakwenda wapi
 
Haya tutoke gerezani, na upuuzi wote

Tuwe huru kwa Dunia inayozalisha wajinga kila kukicha

Unadhani wakiachwa jinsi walivyo kwa dunia hii matendo yenye ukomo, lipi litakuwa na manuufaa.!?

Tumfanye binadamu awe huru ashibe aendekeze nyege, Baada ya muda anapambana na ongezeko lake na kuona hilo ni tatizo wakati Ufahamu wake unahusika zaidi.!

Kumfanya binadamu kuwa na hofu kwa asicho kifahamu Kuna faida zaidi kuliko maisha yake halisi
Sheria za nchi mbona zipo? Mtu akishakua na fikra huru hata uwezo wa kujitambua unaongezeka , vipi kuhusu wanatishiwa jehanam ila anajitoa mhanga ili akifa apate peponi?
 
Sheria za nchi mbona zipo? Mtu akishakua na fikra huru hata uwezo wa kujitambua unaongezeka , vipi kuhusu wanatishiwa jehanam ila anajitoa mhanga ili akifa apate peponi?
Kuishi bila Ufahamu ni hatari zaidi ya bomu la muhanga

Mtu akizaliwa bila Ufahamu na chambo cha maisha kikiwa pesa

Anaweza kufanya lolote zaidi ya bomu la muhanga

Kuna watu wanajilipua kwa viuno usiku kucha kutafuta salali na jamii haioni kama ni bomu.!
 
hiki unachosema sio kweli mkuu
 
Kuishi bila Ufahamu ni hatari zaidi ya bomu la muhanga

Mtu akizaliwa bila Ufahamu na chambo cha maisha kikiwa pesa

Anaweza kufanya lolote zaidi ya bomu la muhanga

Kuna watu wanajilipua kwa viuno usiku kucha kutafuta salali na jamii haioni kama ni bomu.!
Noma sana , ngoja nikuulize swali , mtu anaetishiwa mbinguni na jehanam na akafanya matendo mema na mtu anaefanya matendo mema bila ahadi wala vitisho ,yupo yupo real zaidi?
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Nifahamishe

we fungua macho tu --- tathmini kwa makini hiyo model uliyoitaja kama imesaidia lolote , case study rahisi ya wewe kutumia "hapo middle east"
 
Noma sana , ngoja nikuulize swali , mtu anaetishiwa mbinguni na jehanam na akafanya matendo mema na mtu anaefanya matendo mema bila ahadi wala vitisho ,yupo yupo real zaidi?
Hii nimeipenda, Acha ni kujibu kwa maoni yangu usinihukumu

Kwa ninachofahamu dunia haijawahi kuwa sehemu salama kwa waja wapya.!

Hata ukizaliwa eneo lenye makandokando kama TZ bado Kuna namna ya kuwa kitu

Kuwa real ni namna ya kukubali kuchangamana na mazingira husika na kubaki jinsi ulivyo

Kuishi kwa hofu ya kuambiwa au ya kujitengenezea mwenyewe sio kitu kikubwa

Lakini kwa namna gani tutaamua jinsi tulivyo inatuhusu sisi wenyewe zaidi

Tukiamua tujilee kwa kuwa fanya watu wahofu katiba na gerezani Kuwe ndio motoni ni uamuzi wetu, kuliko moto wa jahanam

Lakini suala la msingi kwanini inatupelekea kudhani bila hofu mtu hawezi ishi.!?

Maana hata kama umezaliwa mbumbu Kuna kitu utahisi hakiko sawa kwa wanadamu maana you can feel kuna error kwenye matokeo ya uwepo wa binadamu before udhihiriko.!

Na ndio hapo nadhani walipoanzia wahenga kutafuta sababu ya uwepo wetu
 
Safi, binafsi naona sababu bado haijapatikana na huenda mambo yapo hivi hivi tu bila sababu yoyote ,pia huenda hakuna mwanzo wala mwisho , maisha yapo kwenye cycle tu🤔
 
Back
Top Bottom