Mtoto wako amewahi kukuaibisha mbele za watu?

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
Wakuu kwema?

Kama tunavyojua watoto walivyo, hawana aibu, wanafanya kile wanajisikia kwa wakati huo, japokuwa kuna wengine wananya kukukomesha. Wanajua mama/baba huwa hataki kuninunulia kitu fulani mkifika supermarket anapiga kelele duka zima wanasikia analilia mdoli😂😂.

Ama unajua mtoto wako huwa hali kitu fulani, unakaribishwa umpe mtoto, unasema mwanangu huwa halagi hivi, picha linaanza mwanao alaililia na kula kitu!

Vipi mdau, ni tukio gani mtoto wako aliwahi kukuabisha mbele za watu?
 
Binti yangu alimwambia mgeni suruali yako imetoboka. Mbaya zaidi ilikuwa imetoboka pakubwa makalioni na jamaa hakuwa anajua kabla.

Binti alisema innocently maana alikuwa ana miaka 2 tu ila jamaa pozi lilikata saa hiyo hiyo.

Nilihadithiwa mimi mwenyewe nilishawahi muuliza mgeni kama haoshi viatu maana vinanuka, mimi mwenyewe sikumbuki. Inasemekana jamaa alikuwa ananuka kweli miguu.
 
😂 😂 😂 😂 daaah, nimecheka sana ya suali kutoboka
 
Wakuu kwema?

Kama tunavyojua watoto walivyo, hawana aibu, wanafanya kile wanajisikia kwa wakati huo, japokuwa kuna wengine wananya kukukomesha. Wanajua mama/baba huwa hataki kuninunulia kitu fulani mkifika supermarket anapiga kelele duka zima wanasikia analilia mdoli.

Ama unajua mtoto wako huwa hali kitu fulani, unakaribishwa umpe mtoo unasema mwananguhuwa halagi hivi, picha linaanza mwanai alaililia na kula kitu!

Vipi mdau, ni tukio gani mtoto wako aliwahi kukuambisha mbele za watu?
Jamii Forum Kila mtu ana mtoto
 
Kuna dada mmoja rafiki yangu, alinitembelea home, siku hiyo nilikuwa nipo na kabinti kangu, kana miaka mitatu.

Tukawa tupo mezani wote watatu wakati wa chakula cha mchana .

Baada ya kumaliza kula binti wa watu kabakiza chakula , akadai kashiba.

Kabinti kangu kakaropoka" icho chakula unamwachia nan? , unadhani baba yangu anapesa za mchezo" .

Duh niliona aibu sana, sijui hayo maneno kayatolea wapi.
 
Mwanangu amekulia sehemu ambayo hakuna Waislamu hajawahi ona mtu akiwa amevaa yale sijui majuba au hijabu manguo meusi ya kufunika uso na mwili mzima.

Nilienda naye Morogoro kwa wazazi, asubuhi akakutana na mama wa kiislam Jirani yetu amevaa yale manguo. Naona mtoto kaja ndani spidi analia na kumuita Mama yake. Mamaaaaa kuna jini linakuja. Kidogo tunaona yule mama anakuja nyumbani. Dogo yupo chumbani amejifunika blanket. Ikabidi tuombe msamaha kwa yule mama maana alisikia na akawa amekasirika. Tukaanza muelekeza mtoto kwani alikuwa mtoto wa miaka 4 kipindi hiko.
 
Kuna dada mmoja rafiki yangu,alinitembelea home, siku hiyo nilikua nipo na kabinti kangu , kana miaka mitatu .

Tukawa tupo mezani wote watatu wakati wa chakula cha mchana .

Baada ya kumaliza kula binti wa watu kabakiza chakula , akadai kashiba.

Kabinti kangu kakaropoka" icho chakula unamwachia nan? , unadhani baba yangu anapesa za mchezo" .

Duh niliona aibu sna ,sijui ayo maneno kayatolea wapi.
Aisee!!!!!
 
Back
Top Bottom