Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 576
- 1,626
Wakuu,
Una jirani, rafiki yako au hata ndugu mnaoishi karibu na mtoto wako alikuwa hana mazoea ya kwenda huko lakini ghafla amekuwa habanduki kwa jirani huyo mzazi shtuka. Na kinyume chake vile vile, mtoto wako alikuwa anapenda kwenda sehemu fulani kucheza lakini ghafla haendi huko na unajua kuna rafiki yake mzuri muda wote hucheza pamoja shtuka pia, kuna uwezekano mkubwa kuwa kuna jambo baya limetokea huko ambalo limefanya awe anaenda au aache kwenda sehemu husika.
Badala ya kufurahia mtoto akienda sehemu fulani unapata muda wa kufanya mambo yako, au sasa mtoto wako ameacha kuzurura na kupenda mchezo kila wakati, fuatilia ujue kuna nini.
Watoto wengi wanapitia unyanyaji wa kingono kwa kwa njia hii kutoka kwa watu wazima au hata watoto wenzao, mpaka mzazi unakuja kushtuka unakuta ameshaharibika au ameshafanyiwa vitendo vibaya muda mrefu.
Ni vizuri pia kuweka utaratibu wa kupiga stori na mwanao kila siku jioni, muulize siku yake ilikuaje, amefanya nini, amecheza na nani, amejifunza nini, kwa kufanya hivi itakuwa rahisi kujua nini kinaendelea kwenye ulimwengu wa mtoto wako na kutambua tatizo mapema pale linapotokea.