Mkurugenzi wa vipindi na uendeshaji wa Clouds aliyefariki dunia hivi karibuni anatoa funzo kubwa sana kwa vijana. Funzo hilo ni kutengeneza network halisi katika maisha.
Ruge hakuwa na accounts zenye followers wengi instagram, twitter au kwingineko na badala yake alikiwa na wafuatiliaji halisi katika maisha halisi kupitia yale aliyoyafanya wakati wa uhai wake.
Juzi nilipita katika vijiwe mbalimbali ambapo nilikutana na mijadala mingi kutoka kwa watu wa kawaida wakihoji kwani Ruge ni nani hasa, mbona msiba wake umegusa watu wengi sana hasa viongozi wakuu wa taifa letu?
Nilichojifunza kwenye maisha ya Ruge ni kuwa alitumia muda wake mwingi kufanya mambo ambayo yaliigusa jamii iliyomzunguka moja kwa moja pia alifanya mambo mengi kwa ajili ya taifa lake. Na hili limejidhihirisha katika kipindi hiki akiwa hayupo nasi tena, kwa namna watu walivyoubeba msiba wake kama shujaa.
Ujumbe wangu vijana tuache kuchapisha mambo yasiyoeleweka kwenye mitandao ya kijamii na badala yake tufanye kazi zitakazotuletea followers halisi wenye kuguswa na maisha yetu na michango yetu chanya.
Rest in Peace Ruge your Legacy will remain forever!