Mtoto wa RUGE amuombea samahani Baba yake

Utaanzaje mpa mkono wa kushoto mkuu wa nchi halafu umkate jicho?,hata kwa trump haiko hivyo refeer mwandishi wa CNN alinyanganywa kibali cha kutia mguu ikulu kwa kukosa heshima mbele ya mkuu wa nchi

Sasa imetokea. Wewe hukuona?
 
Ukabila (ukanda) na chuki. Watoto kule Arusha hawakuthaminiwa, pengine walikuwa wakiishi jimbo la upinzani.
Wamefariki Watu zaidi ya 200 kwa Ajali ya kivuko wameenda Baadhi ya Viongozi(Mkuu wa Nchi hakwenda) , ila Msiba huu Serikali yote iko kanakwamba ni Msiba wa Kitaifa ,CCM Wanafki sana..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: prs
Kwani kampeni za ndani ya chama zimeanza, naona amejipanga kuendelea na ufalme wake wa uenyekiti, nendeni kwenye pointi moja kwa moja acheni kuzunguka. Mmsheanza kumuonea wivu marehem sifa anazopewa na nyie mnazitamani dah! Wakifanana so what
Waswahili wanasema anataka kutembelea nyota ya Ruge .
 
Kuna kitu kinaitwa funeral behavior watu wanatakiwa kufundishwa kuwa ukifiwa you need to behave yourself.Sio sehemu ya Ku misbehave ile.Taabu wengine wakifiwa hunywa pombe Kali au kuvuta Bangi eti apate steam ya msiba matokeo yake aweza misbehave.Kama kweli kufanya hivyo ita mcost labda asiwe na deal yeyote na serikali au ajira serikalini wataondoka na hiyo video na kuiweka kumbukumbu for years ya Kula naye sahani moja
Aisee,
Am speechless,
Are you crazy?????

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Mbunge wa jimbo la Hai na Kiongozi wa upinzani Bungeni kwa sasa yupo gerezani Segerea.

Ruge Mutahaba, Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji, Meneja wa Clouds Entertainment Company zamani kabla ya kuwa Clouds Media Group, Muanzilishi wa Tanzania House of Talent (T.H.T), amefariki Jumanne 26/2/2019 Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu.

Mbowe na Ruge watu hawa ukiwafuatilia na kuchunguza tabia na maisha yao kwa karibu, utagundua hawana tofauti kubwa sana, kuanzia wanavyoishi na watu, wako simple na sio watu wa kujikweza kabisa hata siku moja, wote wakisisitiza muda wote mlango wangu uko wazi, hupenda kusikiliza kuliko wao kuongea.

Nilianza kufanya kazi na Ruge Mutahaba nikiwa na miaka 22 tu, nikiwa kijana mdogo, kwenye interview mbele ya watu wenye Digrii na Diploma nikiwa na elimu ngazi ya cheti tu, alitizama uwezo wangu wa kazi na commitment na sio ukubwa wa elimu yangu, ndipo nilipoanza kufanya nae kazi kwa karibu mpaka mwaka 2013.

2014 nilikutana na Freeman Mbowe nikiwa kama mwandishi wa habari tukiwa field kanda ya kati, tukiwa tunaruka kwa chopa kwenye operesheni "delete ccm" niliachana na genius nikakutana na genius, how luck i was.

Kwa jicho lile lile aliloniona Ruge, Mbowe nae aliniona, nikaanza kufanya kazi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Mbowe na Ruge kwa kuwa nimewahi kukaa nao sijaona tofauti kubwa sana walizo nazo, wote ni watu wa watu, wanapenda watu na kujichanganya sana, ili wajifunze mambo mapya na kusikiliza watu.

Wote wamefanikiwa kupewa dhana ya ushawishi mkubwa katika jamii kwa yale wanayoyaamini na kufanikiwa kupendwa sana kila kona wanayopita, pia wamebahatika kupewa hekima na busara nyingi katika maisha yao, ni watu wanaoamini katika vipaji vya watu, wenye macho ya kugundua watu wenye uwezo mkubwa na kuwachukua na kuwalea katika kile wanachokiamini na kutaka wafikie ndoto zao pale wanapowaamini, hukuacha huru uendelee kupepea na ataendelea kukusaidia wakati wowote utakapohitaji msaada kutoka kwake.

Ni watu wasiopenda kushindwa, hawapendi kuona watu wanashindwa pia katika yale wanayoyaamini katika kufikia ndoto zao, wako tayari kujitoa kwa lolote katika kusimamia wanachokiamini, hawakati tamaa, wapambanaji na wenye kupenda kusaidia watu, waliopata kukaa na Mbowe wanaweza wakawa mashuhuda na waliobahatika kukaa na Ruge pia ni mashuhuda pia ni watu wenye kaliba moja na maono sawa.

Ukimfuatilia Mhe Freeman Mbowe ni mtu ambae ameamini katika rika zote hususani vijana ambao kupitia yeye amewapa nafasi na kuwalea na kwa sasa ni wanasiasa na mastaa wakubwa nchini Tanzania.

Maisha ya Freeman Mbowe kusafiri nje ya nchi toka akiwa kijana mdogo sio ishu ana-exposure ya kutosha ni mtu ambae amefika Marekani akiwa kijana mdogo angeweza kubaki huko aendelee kula maisha yake kwa mrija lakini akaona hapana lazima nirudi Tanzania na kulitumikia taifa lake, vile vile ilivyo kwa Ruge amezaliwa Brookkyn New York Marekani lakini aliamua kurudi Tanzania akiamini Tanzania inamuhitaji sana.

Kupitia Mbowe wamesaidiwa watu wengi unaposoma hili andiko kichwani kwako majina ya waliofanywa na Mbowe wajulikane yanakuja mengi, na amefanikiwa kubadilisha siasa za Tanzania kwa asilimia kubwa akifungua akili za Watanzania waliokuwa wamelala bado (In deep slumber), ameleta utoafauti sana na ilivyokuwa awali kwa miaka 20 iliyopita akiwa shujaa wa kwenye siasa za upinzania,Sugu hupenda kuita "Siasa za Mars" yani za level za juu sana kupata kutokea.

Kupitia Ruge wamesaidiwa watu wengi na unaposoma hili andiko majina ya waliyosaidiwa na Ruge yanaanza kuja kichwani na amebadilisha tasnia ya burudani kwa asilimia kubwa hapa Tanzania.

Mfano Joseph Mbilinyi mbunge wa Mbeya mjini, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema (Sugu), Joseph Haule mbunge wa Mikumi (Professa Jay) hawa walipita mikononi mwa Ruge akafanya nao kazi katika sanaa na baadae kuibukia mikononi mwa Mbowe akawaamini akawapa nafasi na sasa anafanya nao kazi katika siasa, ukiacha changamoto ambazo zilitokea awali kati ya Sugu na Ruge na Profesa Jay misuguano ya hapa na pale Nukuu "Kama hakuna changamoto katika unachokifanya fahamu kuna mahali unakosea" Ruge.

Lakini mwisho wa siku yote yalikwisha wakafanya kazi kwa pamoja hadi mauti yanamkuta Ruge, Sugu na Profesa Jay walikuwa wakishirikiana vizuri kwa pamoja kwa masuala ya muziki huku wasanii hawa wakiwa wanamuziki na wanasiasa Wabunge wa Chadema chini ya M/kiti wao kiongozi wa mapambano ya kuleta mabadiliko ya kweli usawa na haki hapa nchini Tanzania Kamanda Freeman Mbowe.

Mbowe wakati akimiliki Club Billicanas kabla ya kuvunjwa mwaka 2016 na utawala wa awamu ya 5, ameshirikiana na Ruge na Joseph Kusaga Mkurugenzi wa Clouds Media Group wamekuwa ni wafanyabiashara walioungana (Business Partners) katika burudani na kuinua vijana katika muziki kupitia club hiyo ya kisasa iliyopata kutokea Tanzania na kwa asilimia kubwa ya wasanii wa Tanzania wamefanya shows pale wao ni mashahidi.

Wasanii wengi walikuwa wakifanya shows zao pale ikiwa ni club ya kisasa nchini iliyojulikana pande zote za Dar es salaam, Tanzania yote na Áfrika Mashariki, wageni wengi walipofika Tanzania walipenda kutembelea Club Billicanas na Much More Restaurant kupata vyakula, vinywaji, burudani na kukutana na wasanii mbalimbali ikiwa ni sehemu yenye usalama mkubwa, parking kubwa ikiwa ni club pekee ambayo haikuwahi kupata kashfa yoyote wala majanga huku viongozi wengi wa kiserikali wakipenda kufika hapo wakiamini ni sehemu salama sana.

Kupitia Club Billicanas na kupitia Mbowe na Ruge asilimia kubwa ya wasanii wamefanya kazi ndani ya Club Billicanas, Ruge na Mbowe walikuwa ni ndege wanaofanana ndio maana waliruka pamoja ingawa mmoja ni mwanasiasa/mfanyabiashara na mwingine alikuwa ni mfanyabiashara 100% katika tasnia ya habari, burudani na michezo.

Kwa ufupi wanasiasa waliopitia mikononi mwa Mbowe akawaamini na kuwaacha wafanye kazi na leo ni wakubwa, kwa kuwataja wachache ni pamoja na Zito Kabwe, Halima Mdee, John Mnyika, Joseph Mbilinyi (Sugu), Joseph Haule (Profesa Jay) John Heche, Ester Bulaya, Godbless Lema, Peter Msigwa, Meya Boniface Jacob, Ester Matiko na wengine wengi sana ambao ni matunda yake ambao ni wengi siwezi kumaliza nikianza kuwataja hapa.

Baadhi ya Wasanii waliopitia mikononi mwa Ruge nakufanya nao kazi ni Sugu ambae mara ya mwisho alifanya show ya Fiesta Mbeya akiwa kwa karibu kabisa na Ruge.
Profesa Jay, Lady Jaydee, Ray C, Mwana FA, AY, Lina, Ruby, Nandy, Mwasiti, Amin na wengine wengi ambao siwezi kumaliza leo nikianza kuwataja hapa.

Hawa ni watu ambao wanaomiamini katika uwezo wa mtu binafsi hawaamini sana katika vyeti ingawa wanasisitiza sana elimu na kusaidia kulipia watu wasio na uwezo ada za shule, wakisisiti kwamba elimu ni muhimu itakusaidia kureason na kupambanua mambo hivyo usiache elimu iende zake, ila wakati wanafanya kazi na wewe hawaangalii elimu sana, bali wanaangalia uwezo wako kwenye kufikisha ulicho nacho kwa watu na jinsi utakavyotumia uwezo wako kuisaidia jamii yako kupitia kipaji chako, unaweza ukaona kuna wasomi maprofesa lakini kupitia elimu zao kubwa wamekuwa ni mizigo kwa taifa badala ya faida ndani ya jamii, hapo ndipo unapoona unaweza ukawa na elimu ukashindwa kuitumia na mwenye elimu ya kawaida akakuzidi kureason mambo na kutatua jambo kwa manufaa ya wengi.

Mbowe na Ruge ni watu ambao ukicgunguza ukafanya utafiti wako mdogo utagundua ni watu ambao wanapendwa sana na watu wakiwemo wale wanaoamini katika mambo wanayoyafanya miongoni mwa jamii kwa ushawishi wao.


Ni watu ambao kwa hali zao za kifedha na kwa kuwa sio wabinafsi, pasipo na shaka wangeweza wakakaa na kuendelea kutumia pesa zao bila kubugudhiwa na kuacha kutaka kuisaidia jamii kutoka sehemu moja ama nyingine.

Mbowe amekuwa mpigania usawa na haki katika Taifa hili atakaebisha au kukataa hata mawe yatasema hata Yesu na Mtume Muhammad walihubiri neno la Mungu lakini walipingwa, kupingwa kupo kote duniani, na watakaopinga ni opponents sababu hata Ruge huyu kuna ambao wanampinga, sio lazima upendwe na wote au uchukiwe na wote, tenda wema nenda zako life is too short .

Tumsifu kabla hajaondoka, sio aondoke ndio tumsifu, ambapo hatoweza kuona wala kusikia.

Ruge amesaidia jamii husasani vijana kwa kuwafungulia dunia kama alivyokuwa akisema katika kauli mbiu mbalimbali za fursa, leo ameondoka anapewa sifa ambapo hawezi kuona wala kusikia.

Hivi ndivyo navyoweza kuwalinganisha Mbowe na Ruge katika maisha yao.

Namsifia Mbowe leo, kwa kusaidia watu wengi, najua akitoka Segerea atasoma ujumbe huu nakuona sifa hizi, isije ikatokea kama ilivyo kwa Ruge nilishindwa kumpa sifa zake hata kwa kumtumia ujumbe kwa simu yake huku nikiwa na namba yake, amefariki ndio naona umuhimu wa kumpa sifa zake lukuki, kwa sasa nikiwa chini ya Boss mwingine mwenye kaliba kama ile ile ya Ruge nampa sifa zake.

Mbowe is so kind, very intelligent, hero of this good fight, sent from heaven to start this war against lawlessness in the country.

Watajaribu kukata miti lakini mbegu zishadondoka chini katika udongo wenye rutuba na kuota tena, you changed people's mind sets, you sow the right seeds in us, prints are in our hearts no body can see from outside, you did the right thing in your life time though you are behind bars by now but i will never be a snitch and turn my back on you.

Salute Kamanda Mbowe. Aluta Continues....
Umemsahau Lowassa!
 
Ukabila (ukanda) na chuki. Watoto kule Arusha hawakuthaminiwa, pengine walikuwa wakiishi jimbo la upinzani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Chuki za hatari Mkuu, hata Waliojitokeza Kusaidia kama Nyalandu nao wamaonekana wanatafuta Kiki za Kisiasa, Yani Watoto wanapoteza Maisha hata huruma hakuna, Watu wanakufa kwa Tetemeko unasema Serikali haijaleta tetemeko!! Badala ya Kuwafariji!! tena hiyo ni baada ya Miezi kupita ..Tulipofika kuna Watu ni Watanzania kuliko wengine.Ubaguzi na Chuki.
 
Haitusaidii waTanzania wote.sisi tunaendelea na maisha
Angalia vizuri tukio mubashara la kuaga mwili wa marehemu pale ukumbini. JPM alikuwa wa kwanza. Baada ya kuaga na kusali kidogo, alienda kuwapa Mikono ndugu wa marehemu na baadaye viongozi. Kama umeona vizuri ndugu mmoja mdada hakumaindi kabisa Pole ya JPM na akampa JPM mkono wa kushoto na kumkatia jicho la chuki. Hamkuona wakuu hilo?!?

JAH Rastafari Morning Africa.Trust JAH respect nature
 
WakureaTE="share, post: 30609059, member: 12643"]Angalia vizuri tukio mubashara la kuaga mwili wa marehemu pale ukumbini. JPM alikuwa wa kwanza. Baada ya kuaga na kusali kidogo, alienda kuwapa Mikono ndugu wa marehemu na baadaye viongozi. Kama umeona vizuri ndugu mmoja mdada hakumaindi kabisa Pole ya JPM na akampa JPM mkono wa kushoto na kumkatia jicho la chuki. Hamkuona wakuu hilo?!?[/QUOTE]
Alikuwa amebeba mtoto kama uliona vizuri na mtoto alikuwa amelalia mkono wakulia tazama vizuri
 
Aliyoyafanya Ruge kwenye jamii kama normal corporate person, yalitakiwa kufanywa na upinzani!

Ruge zaidi ya mpinzani, hata huyo kidomo washa bwana Lissu hana na haji na hawezi mfikia Ruge kwa impact ya mtu mmoja mmoja


Sugu is realy trying lakini sio kwa magnitude ya Ruge

naona unatamani sana sana sana Ruge angekuwa mwenyekiti wa chadema!...hakuwa, hajawa..Mliye naye hawezi hana na hatakuja kuwa kama Ruge

Umeandika waraka mrefu wa kuaminisha watu uongo.Mbowe anajulikana kwako ila sio katika jamii

Juzi kafungwa, yuko ndani...sijui hata kama ulienda kula nae xmass na mwaka mpya..haukwenda mwanahizaya wewe!!

usimfananishe Ruge na huyo muhuni

Projects za Ruge zaidi ya 20, zipo, zimezaa matunda...nenda jukwaa la celebrity kazione list yake

kisha rudi, futa utumbo huu
Kweli mkuu! Ila ruge alikuwa inspirational kwenye issue za kihuni huku mwenzake Mbowe akipigania haki na usawa kwa wote!! Hilo umeliona? Ruge analaumiwa kwa kula jasho la watu wanyonge ambao Mbowe amekuwa akiwapigania miaka yote! Mambo ni mengi mkuu! Alale kwa amani Ruge Mutahaba!
 
Back
Top Bottom