Mtoto wa nje ya ndoa

Mkulu hiyo hapo imenifanya nipate picha kama vile unamCROSS EXAMINE mshtakiwa.

Mkulu unafaa zaidi kuwa Lawyer kama siyo Lawyer.

Nimeipenda.

Respect.
 
Aisee hii issue inaonekana ngumu sana lakini mwisho wa siku ni ukweli tu unaotakiwa kwa mmeo na mtoto. Maana ukiacha harafu jamaa yule akaja kudai mtoto itakuwa tatizo kubwa hivyo ni vema hilo likafanyika mapema ili mtoto naye aamue kama atamchagua baba mlezi au kuamua kurudi kwa baba mzazi.

Baba mzazi hawezi laumiwa kwani inawezekana kwakuwa yuko kwenye ndoa na huyu dada yuko kwenye ndoa hivyo kila mmoja inawezekana alikaa kimya kwa upande wake. Lakini kuna siku jamaa atamwambia mke wake kuwa huwa ana mtoto na hapo ndiyo kasheshe itakapokuja.

Makosa kama haya hutokea lakini huwa ni lazima yasemwe vinginevyo matatizo huwa ni makubwa na yenye kuumiza sana.
 

Aisee huyu jamaa anatia huruma. Yaani baada ya kumyima haki yake siku zote hizo leo hii amejua tena kutoka kwa mtu mwingine then wanamtenga? Kwakweli dunia hii watu wabaya sana. Mimi ningekuwa mimi ningetimua nikaenda kuanza maisha mapya maana huu unafiki ni ngumu sana kuuvumilia. Makosa niya wakubwa siya kijana tena hasa mama yake inabidi amsaidie kijana wake kuliko kumwacha anateseka bure. Kwani yeye ndiye alimwambia huyo mama awe na uhusiano na huyo baba. Pole yake sana.
 
arrrg wewe maindamainda unaudhi sana......ulikubalije kupanua miguu wakati umeolewa?

.....haya mambo ndio yanayosogeza goal yangu...bado kidogo nitaungana na akian Icadon no kuoa.Kama kuoa kwenyewe upuuzi ndio huu wanawake mnawafanyia waume zenu its better niwe nakamata ma striper najimegea......
 
wanaume hufanya hivyohivyo ila bahati nzuri wakiishazalisha wanaacha aliyezaa apambane,
mwanamke inakuwa issue kwakuwa mahusiano ya mama na mtoto ni makubwa toka tumboni hadi kuzaliwa, wazalishao wake za watu ni waume za watu......
 
Bibi Kizee,
Asante sana. Kuna wakati huwa siwaelewi wanaume kabisa, kwa jinsi wanavyokuwa na double standards.
 
Bibi Kizee,
Asante sana. Kuna wakati huwa siwaelewi wanaume kabisa, kwa jinsi wanavyokuwa na double standards.
Huwezi kuwaelewa kamwe......

Iweje utoke nje ya ndoa ilihali una mume wako? usiniambie ni shetani....ujue unanizidishia hasira
 
ukisoma posts nyingi humu, ni vigumu kuona wanaume wakikubali kuwa wanachangia katika kuparaganyisha familia na kumomonyoa maadili.
Utakapojaribu kuibua maswala utasikia ohh ulifanya research! Bahati mbaya sana kwa vile hatutaki ku disclose identities zetu tunashindwa kuleta takwimu zenye uhalisia na hivyo kuonekana kama tunaoleta hadithi za saloon kama wanavyopenda kusema Yoyo,Ngwaninyami A.K.A...A.K.A......na Masanilo- the trio ( mnaniboa sana!).The bottomline is - men put ur act together kama mnataka mabadiliko!STOP BLAMING WOMEN - ACCEPT THE FACT THAT YOU TOO HAVE UR OWN SHARE IN IT! U WANT CLEAN RELATIONSHIPS - MAKE SURE U R CLEAN.
 
Aisee hii issue inaonekana ngumu sana lakini mwisho wa siku ni ukweli tu unaotakiwa kwa mmeo na mtoto. Maana ukiacha harafu jamaa yule akaja kudai mtoto itakuwa tatizo kubwa.

Subutu yake! Hawezi kudai mtoto kwa mke wa mtu na kama anaipenda ndoa yake, au kama mkewe hazai basi watakubaliana. Vinginevyo ni hadithi.
 
naungana mkono na wadau waliopita ya kuwa "only truth shall set U free. Kumbuka hata kama baba mzazi halisi hana uthibitisho kuwa mtoto uliyenaye ni mwanawe but DNA inaweza kuthibitisha dada angu.

The earlier the better labda mzee akiujua ukweli atakasirika kwa muda na hata kukufukuza but if he really loves U na kama utampigia magoti ukakili kwa moyo wako wote, atakutafuta and U'll enjoy the marriage again

Piga moyo konde mwite umwambie....ikiwezekana shirikisha wazazi pia katika jambo hilo... kumbuka unavyochelewa ni hatari zaidi..

But make sure it doesn't happen again, mean kumcheat...maana utakuwa unatonesha kidonda.
 

Ni jambo ngumu sana ukweli ni kwamba wapo watu wengi wa jinsi yako lakini hawana ujasiri wakuliweka wazi.Kwa mtu wa kawaida ni gumu kulipokea japokuwa inaonyesha fadhaiko kubwa ulilonalo moyoni. Inaniashilia kuwa jambo hilo lilitokea kwa bahati mbaya jambo ambalo humtokea mtu yeyote maana tumewahi kuona mtu akitembea na mtu ambaye akijiuliza baadaye anasema hivi ilikuwaje?Kuteleza siyo kuanguka kama ungeweza kukili kwa mumeo na kuhakikisha kwamba kosa hilo hulitendi tena kwa vyovyote hiyo ndo ingekuwa zawadi pekee kwa mumeo yaani uaminifu.
Wahenga walisema Kitanda hakizai haramu msemo huo uchukulie kuwa wapo wengi na haikuanza leo. Ziko siri watu wanaingia nazo mpaka kaburini lakini kitendo chako cha kuswuta na hilo ni kwamba unataka kutoa ile hali yakusutwa na nafsi yako.Basi kama unaweza mwambie mumeo uwetayari kulipa gharama ya tendo hilo na gharama yake itakuwa na ahuweni kwako maana utaona kama umetuwa mzigo fulani.Kila action ina Impact yake.
 
Nimewaambia jamaa zangu wa4 wakapime DNA j3 yawezekana huyu mahindamahinda akawa mke wa mmoja wao....
 
Nimewaambia jamaa zangu wa4 wakapime DNA j3 yawezekana huyu mahindamahinda akawa mke wa mmoja wao....

Usiwapandishe presha wenzio, kwanza usikute na wao wana watoto nje kwa kujijua/kutojijua!..
Ukimchunguza sana bata hautamla nakwambia!..Wakina maindainda wapo wengi kwenye jamii sema ujasiri wa kusema ukweli hawana vile wamekosea na wataaibika pia kuogopa talaka na vitu kama hivyo!
 
acha kabisa kauli hizo ndio zimenifanya nizidi kusogeza goal....

yaani waendelee kuhudumia watoto wasio wao? mambo ya Saleh wa clouds Fm noma.....ushaolewa kwanini uzini nje?
 
acha kabisa kauli hizo ndio zimenifanya nizidi kusogeza goal....

yaani waendelee kuhudumia watoto wasio wao? mambo ya Saleh wa clouds Fm noma.....ushaolewa kwanini uzini nje?

Siku hizi unalea mimba mtoto akishazaliwa tu basi unahakikisha unafanya DNA kuhakikisha mtoto aliyezaliwa ni wako hasa kama anafanana na bibi au babu wa Babu wa Mke wako ambao si ajabu wewe hujui hata wanafananaje. Akili mkichwa!!!!
 
acha kabisa kauli hizo ndio zimenifanya nizidi kusogeza goal....

yaani waendelee kuhudumia watoto wasio wao? mambo ya Saleh wa clouds Fm noma.....ushaolewa kwanini uzini nje?

Usisogeze goal mbele kisingizio kubambikiwa mtoto labda kama hujadhamiria kuoa kutokana na mambo mengine.
Kuna haja ya kuwa mkali(siyo cris brown style) kwa mamaa kuwa kuna DNA na akikubambikia mtoto utapata ukweli ili ajue mumewe moto chini!
Hakuna haja ya kuzini nje wakati umo kifungoni ila mambo yanatokea sana kwenye mazingira tunapoishi!..
Make sure unaoa hiyo 2010, eti mwanaJF Yo Yo bwanaharusi mtarajiwa!..I can imagine maana utakuwa unawaza DNA DNA tu! Haitokei kwa kila mtu pia usimcheke mtu kesho yakakukuta halafu uelewe vizuri kashkash za maisha!..
 

kuacha mke siyo suluhisho, kosa la kwanza halimwachi mke huyu dada ameteleza angekuwa ni mtu wa makusudi asingehudhunishwa na nafsi yake,Tatizo kubwa hapa siyo kumweleza mume wake bali ni jinsi gani ataaminika tena kwa mumewe(Trust) hicho ndicho ninachoona kinamsumbua.
Pendo la kweli halifi kama bwana ana mapenzi na mkewe hilo linaweza kutatulika kwanza kwangu kama mwanaume kitendo cha mke wangu kuniambia hilo japo kuwa litaniuma sana lakini litanipa heshima kuwa hakika huyu mama ananipenda na kuniheshimu kwani hakuwa na sababu yakuniambia
amenihurumia (huruma ni moja ya vigezo vya mapenzi ya dhati) Dada yangu napenda kukupa pongezi kwa jinsi ulivyo na huruma na pendo la dhati kwa mumeo.Mwambie mumeo naye umuone pendo lake liko vipi.
 
Siku hizi unalea mimba mtoto akishazaliwa tu basi unahakikisha unafanya DNA kuhakikisha mtoto aliyezaliwa ni wako hasa kama anafanana na bibi au babu wa Babu wa Mke wako ambao si ajabu wewe hujui hata wanafananaje. Akili mkichwa!!!!

hii discussion is quite revealing!
So the prob seems to be real and big.Im just thinking out loud..hivi tuseme mume atakapoanza kumwambia mkewe... hebu tukapime DNA tujue kama mtoto ni wangu au la, halafu wakipima ikaonekana mtoto ni wa mume, huko nyumbani kutakalika?Binafsi mimi nikifikishwa kwenye situation hiyo sijui kama hiyo ndoa itakaa tena.
 
Siku hizi unalea mimba mtoto akishazaliwa tu basi unahakikisha unafanya DNA kuhakikisha mtoto aliyezaliwa ni wako hasa kama anafanana na bibi au babu wa Babu wa Mke wako ambao si ajabu wewe hujui hata wanafananaje. Akili mkichwa!!!!

Maana utasikia kucha kama za bibi au mjomba, kha! hapo mimi nachoka mtoto kazaliwa hata mwezi hana anafanana kucha na mtu halafu akifika mwaka kucha zinafanana na mtu mwingine!..
Bora mfanye DNA zenu mapema ili mlee watoto vizuri badala ya kuwa na wasiwasi kila siku wakati kama baba unatakiwa ushiriki kwenye malezi ya mwanao na mkeo/partner!
 

Maindainda, damu siku zote ni nzito kuliko maji,ni afadhali kama huyo jamaa angekuwa hajui kwa hiyo siyo rahisi ifutike hata kama angekuwa hana watoto wa jinsia moja chako ni chako.you never know hivi huyu mtoto akija kuwa maarufu na baba yake anajua itakuwaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…