Makanyaga
JF-Expert Member
- Sep 28, 2007
- 11,738
- 7,536
Napenda wenye ufahamu wanisaidie kuhusu hili.
Nina mke wangu wa ndoa ambaye kabla sijamuoa nilimkuta na mtoto wa kiume wa miaka mitatu, mtoto huyo sasa hivi mkubwa na ameingia form one sekondari.
Mtoto huyu ana baba yake ambaye ni mtu mwenye uwezo mkubwa tu, lakini kutokana na jeuri ya mama yake (mke wangu) hataki kumshirikisha mtoto upande wa babake kwa jambo lolote, yaani hataki hata mtoto ajue kuna babake. Ada ya shule silipi mimi ila mjomba wa mtoto yaani kaka wa mke wangu.
Chakula, mavazi, uniform, nauli ya kwenda shule ya boarding na matumizi ya shule vyote natoa mimi.
Katika kukorofishana baada ya yeye kukataa kunipigia pasi nguo zangu kwa madai kupiga pasi ni option tu hufanyika akipenda yeye sio lazima na mimi nikamjibu ku supply education materials kwa mwanao ni option tu sio lazima kwani mtoto huyo ana baba yake aliye hai , labda asingekuwa naye (amekufa) ndo ingekuwa lazima!
Niliongeza kuwa wajibu wangu kwa mtoto wake huyo ni kumpa chakula ale na kumpa malazi alale tu na sio vitu vingine.
Swali langu sheria inasemaje kuhusu wajibu wetu kwetu sisi akina baba wenye watoto wa aina hii?
Kwani hapo mwanzo wakati mnaoana mlikubalianaje kuhusiana na huyu mtoto? Naanza kupata picha kuwa umeshaanza kumchukia mtoto kwa makosa ya mama yake. Swala la kupiga pasi nguo haliwezi kuwafikisha hadi kwenye maswala ya msingi ya mtoto, hadi ije ipelekee hatimaye mtoto mumuathiri kisaikolojia halafu aharibike aache kufanya maswala ya msingi na hatimaye aanze kuvuta bangi. Achilia mbali mtoto wa mke wako, hata kama angekuwa mtoto mwingine tu ambaye hata huwajui ndugu zake ila umeamua kukaa naye, kumsaidia na kumsomesha, haiingii akilini ukija kumtelekeza katika latter stage kama hii. Halafu kitu cha msingi unapokuwa unatoa msaada kwa mtu, katika hali ya kawaida na ubinadamu, huwa tunachukulia kuwa huko mbele atakuja kukupa tafu kwa aina moja ama nyingine, ila sasa ninachoshauri hapa ni kuwa ni vizuri ukachukulia kuwa unatoa msaada ambao hautakuja kukurudia kwa namna yeyote ile huko mbele, ili kusudi ikitokea huyo uliyemsaidia akakukumbuka, basi uchukulie kama "previledge" kwako. Ukimsaidia ukiwa na malengo ya wewe kuja kusaidiwa pia, utajenga akilini kuwa una "rights" fulani kwake (wakati siyo) ambazo siku ukija kuzikosa, unafrustrate na unaweza kumfrustrate yeye pia. Sasa hivi naona kama unataka kuwa discouraged kumsaidia mtoto kwa sababu unaona mama yake anakuwa na kiburi na unaanza kujiuliza maswali, huyu mtoto atakuja kunijali kweli huko mbele? Una "assumed rights debts" kwake ambazo unadhani lazima aje azilipe na asipofanya hivyo hutaelewa.
Halafu huyu mwanamke naye amepata wapi maneno ya kijinga ya kuwa anamjibu mme wake namna hiyo? Fanya uchunguzi ila tahadhari kubwa, usi-link matatizo ya mama na attitude yako ya kumsaidia mtoto, yaani anatakiwa mama asibadilishe kabisa attitude yako kwa mtoto.