Mtoto wa Mke wangu: Sheria inasemaje?

Mtoto wa Mke wangu: Sheria inasemaje?

mi nimeskitika sana ulivyomuhusisha mtoto kwenye ugomvi wenu. toka miaka mitatu mpaka hapo alipofika mbona umejitahidi sana, huwezi jua huyo mtoto akawa msaada mkubwa kwako na kwa wadogo zake hapo baadae. muombe msamaha mkeo kwa kauli chafu uliyomtolela.
 
Chanzo cha yooote haya ni umaskini, mke angekuwa na kijihela cha kumtunza mwanae aah, maisha poa kabisa.
 
Napenda wenye ufahamu wanisaidie kuhusu hili.
Nina mke wangu wa ndoa ambaye kabla sijamuoa nilimkuta na mtoto wa kiume wa miaka mitatu, mtoto huyo sasa hivi mkubwa na ameingia form one sekondari.
Mtoto huyu ana baba yake ambaye ni mtu mwenye uwezo mkubwa tu, lakini kutokana na jeuri ya mama yake (mke wangu) hataki kumshirikisha mtoto upande wa babake kwa jambo lolote, yaani hataki hata mtoto ajue kuna babake. Ada ya shule silipi mimi ila mjomba wa mtoto yaani kaka wa mke wangu.
Chakula, mavazi, uniform, nauli ya kwenda shule ya boarding na matumizi ya shule vyote natoa mimi.
Katika kukorofishana baada ya yeye kukataa kunipigia pasi nguo zangu kwa madai kupiga pasi ni option tu hufanyika akipenda yeye sio lazima na mimi nikamjibu ku supply education materials kwa mwanao ni option tu sio lazima kwani mtoto huyo ana baba yake aliye hai , labda asingekuwa naye (amekufa) ndo ingekuwa lazima!
Niliongeza kuwa wajibu wangu kwa mtoto wake huyo ni kumpa chakula ale na kumpa malazi alale tu na sio vitu vingine.
Swali langu sheria inasemaje kuhusu wajibu wetu kwetu sisi akina baba wenye watoto wa aina hii?

Ndugu yangu si vyema kabisa kumhusisha mvulana huyo na matatizo yako na mkeo. Kama ulishaamua kumhudumia kijana, haileti picha nzuri kuanza kuhoji huduma zako kwa kijana huyo hivi sasa, eti kwa sababu mamake kagoma kukupigia pasi! Mbona suala la pasi ni dogo sana brother? Tafadhali jitahidi kudhibiti hasira zisikutoe ndani ya busara!!
 
Kutokupasi mkeo hakuhusiani na mtoto,ww shida zako na mkeo unamuingiza vp mtt?umelazimishwa kumuhudumia?huko ni kumnyanyapaa mtt,na unavyoonekana unataka mtt either apelekwe kwa baba ake au ahudumiwe na baba ake,hujui madhara ya mkeo kua na mawasiliano na mzazi mwenzie,shukuru mkeo hataki mawasiliano na huyo baba,ulipenda boga babu penda na ua lake,yako na mkeo hayamhusu mtt!
Passion Lady, nilidhani huyu jamaa anastahili kupewa pongezi kwa kukaa na mtoto wa kufikia ili hali baba wa mtoto yupo na ana uwezo tu kipesa kama alivyotwambia, well hapa imeingia issue ya mtoto huyo kwasababu kulikua kuna vitu vya Options, kama your fellow lady ameaanza kuleta hizo story za option ni kwanini na men nae asitafute issue nyingine ambayo nae kwake ni option? kumbuka Ada sio gharama kubwa sana kama matumizi mengine ya shule, so by any means huyu jamaa ana toa gharama kubwa sana kwa mtoto kuliko hao wajomba zake, hilo moja lakini issue ya pili hapa ni hi, huyu mtoto bila shaka wajomba zake wameisha mwambia kua huyo sio baba yake mzazi, hata kama hawajasema, ipo siku siri hiyo itavuja na kumfikia huyo mtoto, mtoto huyo huyo ataanza process za kumtafuta babaye and mind you, akifanikiwa usije shangaa akaanza kumjali baba yake mzazi na sio baba wa kufikia, hili lazima huyu mwanaume mwenzangu limuume tu.
Sorry, msaidie sasa hapo kwenye vifungu vya sheria kama alivyo omba!
 
mtoto aliingiaje kwenye issue ya kupigiwa pasi? matatizo mengine mnayaanzisha wenyewe halafu vikilipuka mnataka kushauriwa. umekaa na mtoto asiye wako all these years, halafu leo unataka ushauriwe only kwa sababu mke kakataa kukupigia pasi, sioni uhusiano hapa.
Sina hakika kama kuna sheria inayohusiana na mwanaume kuishi na mtoto asiye wako, ila ninachoweza kukuambia ni kua sheria ni nyie wenyewe mnaiweka i.e. wewe na mkeo mtakavyolichukulia. maadam ulimuoa mke wako ukijua ana mtoto asiye wako na ukamu accept, sioni kwanini ghafla uanze kumuingiza kwenye matatizo yenu ambayo hayamhusu.
Ukipenda boga, basi penda na ua lake....
 
..Katika kukorofishana baada ya yeye kukataa kunipigia pasi nguo zangu kwa madai kupiga pasi ni option tu hufanyika akipenda yeye sio lazima...
Kwa nini aliamua ku-opt kutokukupigia pasi (kama mwanzoni alikuwa akifanya hivyo)? Ni nini kilitokea? Unajisikiaje kama ukinyoosha nguo zako mwenyewe?

.. mimi nikamjibu ku supply education materials kwa mwanao ni option tu sio lazima ...
Ungejaribu kutafuta sababu halisi ya yeye kukataa kunyoosha nguo zako, badala ya kutoa jibu kama hili. Halijengi.

.. Swali langu sheria inasemaje kuhusu wajibu wetu kwetu sisi akina baba wenye watoto wa aina hii?
Umesema ulimkuta huyo mkeo akiwa na mtoto wa miaka mitatu. Je nini yalikuwa makubaliano yenu juu ya malezi na mustakabali wa huyo mtoto? Kabla ya wewe kumuoa huyo mkeo, baba wa mtoto alikuwa anatimiza wajibu wake? Kwa nini mkeo hataki kumshirikisha mzazi mwenzie katika kumlea huyo mtoto wao?

Kimsingi, wajibu wa malezi ya watoto upo chini ya walezi/wazazi wote wawili. Huyo baba wa huyo mtoto anaowajibu wa kumlea mwanae ingawa umegusia kuwa mkeo (mama wa huyo mtoto) kwa namna fulani hataki kumshirikisha baba wa mtoto katika malezi.
 

jamani jamani,huyu mama akipewa nafasi ya kua
karibu na huyo mzazi mwenzie sijui?!!labda huyo baba
hana wivu na mke wake,na kama mwanamke hataki ukaribu
na huyo baba kuna sababu,wala si ujeuri wake!!
 
Ndo maana inashauriwa usioe mwanamke aambaye keshazaa tayari
Mkuu si busara kusema hivi kwani mtoto anahusiana nini na mapenzi yenu. Isitoshe wengi wa hawa wanawake sio kwamba walipenda kuwa na hawa watoto kabla ya ndoa. Mshukuru mungu kama unao wazazi wote wawili katika maisha yako.
 
Back
Top Bottom