Mtoto wa miaka 13 aomba msaada wa matibabu kutokana na majeraha aliyopata kwa kupigwa risasi October 29

Mtoto wa miaka 13 aomba msaada wa matibabu kutokana na majeraha aliyopata kwa kupigwa risasi October 29

Traxtion

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2021
Posts
5,895
Reaction score
11,788
Mtoto wa miaka 13, Angel Wariael Noel, ambaye alipata madhara kutokana na tukio la Oktoba 29, kwa kupigwa risasi ya bega iliyomuathiri uti wa mgongo na kumsababishia ulemavu wa miguu. Familia yake inawaomba wadau na watu watakaoguswa kuchangia ili kumsaidia kumudu gharama za matibabu na mahitaji. Ikiwezekana pia hata kupata msaada wa matibabu zaidi nje ya nchi ili kumsaidia Angel kurejea katika hali yake ya kawaida.

Yeyote atakayeguswa na hali hii, tafadhali wasiliana na mama yake mzazi kupitia namba: +255 763 747 599 (HAPPINESS MELEA).

Source:
View: https://www.instagram.com/reel/DUvgKyojKQ6/


View: https://youtu.be/3CY0AIZrKJE?si=XOD0wmVs_uXXWX_f
 
Samia mshenzi sana.Muungano usingekuwepo TUSINGEPATA haya mauaji.
 
Mwenye upendo na hekima akitawala, nchi huneemeka, na watu wake hupata amani na furaha. Dhalimu akitawala, masikitiko, mateso na machozi hutawala miongoni mwa watu.
Tunaomba Mungu alisaidie Taifa letu siku moja lipate watawala wanaojali uhai wa binadamu, wenye utu na hofu ya kutenda maovu dhidi ya wanadamu wenzao.

Ushauri:
Huyu mama wa mtoto badala ya kuchangisha mwenyewe, aombe msaada kutoka taasisi zinazoaminika na kuheshimika na wananchi kama vile taasisi za dini au TLS, zenyewe ziitishe michango kutoka kwa wananchi, nina hakika michango itapatikana ndani ya muda mfupi, na mtoto ataweza kupata matibabu ya uhakika nje ya nchi.
TAHADHARI:
Kuchukuliwe tahadhari zote, yale majitu yaliyotaka kumwua, yakijua kuna aliyenusurika, yanaweza kumwua huyo mtoto na hata mama yake, maana yanataka kusiwepo na mtu anayeweza kutoa first hand information juu ya mauaji ambayo waliyafanya. Mama na mtoto walindwe sana. Tupo katika zama za shetani, ambapo kwao kuua mwanadamu ni tendo dogo sana.
 
Wakati Watanzania wanaendelea kuumia na kumwaga machozi Samuya yupo busy kutuchamba.
Simpendi sana huyu mama. Ni binadamu katili mno
 
Back
Top Bottom