Mtoto wa kiume wa mwl. Christopher Mwakasege afariki dunia hospitali ya Agha Khan

In short huyo jamaa hamjui mwakasege,kwa anayemfahamu hawezi kusema maneno ya namna hiyo,Mwakasege si sawa na akina Gwajima,Boniface Mwamposa,Frank Kilawa,GeoDavie,wala Mzee wa upako,Mwakasege ni mwalimu,anafundisha watu wote!

Hana dhehebu/hekalu lake binafsi,anakufundisha ukielewa nenda katafute sehemu itakayokufaa kumwabudu Mungu wako!

Ni miongoni mwa watu wachache sana wenye vipaji vya kuichambua biblia na kukufanya uelewe!!!
Mnooo bonge la mwalimu
Na alishasema Mungu alikataa asiwe mchungaji abaki kuwa mwalimu
Wachungaji wengi hasa Kkkt huwa wanaenda kwenye semina zake
 
MUNGU amtie nguvu mwalimu wetu christopher mwakasege hakika yupo kwenye wakati mgumu kila jaribu linakuja kwa kipimo na size ya imani ya mtu na hakuna mwenye uwezo wa kupangua mipango ya MUNGU jina la bwana libarikiwe
 
najua ni ngumu zaidi ya maelezo, lkn hapa nikipimo chake cha kiwango cha kumjua anayemtumikia
Kama unamfuatilia mwakasege utakubaliana na Mimi kuwa huwa Mara nyingi anafuata maelekezo anayopewa katika utumishi wake.

Wakati mama yake amefariki na akaendelea na semina ya dar, wakati yupo madhabahuni anafundisha usingejua kuwa kuwa maiti ya mama yake mzazi mortuary inayosubiri semina iishe wazike.

So, Me ninamuombea kwa Mungu ampe uvumilivu na utulivu wa kumsikiliza Mungu anasema nini juu yake katika wakati huu.

Nakumbuka alipokuwa anaelezea msiba wa baba yake tangu anapewa maelekezo ya namna atakavyofariki mpaka mazishi, haikuwa kitu chepesi ila Mungu alimuwezesha.

Nakumbuka masomo yake ambayo ni reference katika hili.

1. Uponyaji wa moyo uliovunjika.
2. Ukichoka ufanyeje.

Wakati anapewa taarifa za kifo cha Fanuel Sedekia ilimlazimu kutumia njia nyingine kudhibitisha kifo hicho. Hata sasa Mungu hatamuacha.
 
In short huyo jamaa hamjui mwakasege,kwa anayemfahamu hawezi kusema maneno ya namna hiyo,Mwakasege si sawa na akina Gwajima,Boniface Mwamposa,Frank Kilawa,GeoDavie,wala Mzee wa upako,Mwakasege ni mwalimu,anafundisha watu wote!

Hana dhehebu/hekalu lake binafsi,anakufundisha ukielewa nenda katafute sehemu itakayokufaa kumwabudu Mungu wako!

Ni miongoni mwa watu wachache sana wenye vipaji vya kuichambua biblia na kukufanya uelewe!!!
Analo "dhehebu" la kijanjajanja...ana akili sana. Sadaka anakusanya, mafungu ya kumi anakusanya, utasemaje kuwa hana dhehebu lake binafsi? Semina zake ndio ibada zake, amecheza na akili tu ili asigombane na Lutheran lakini analo kanisa lake linaitwa Mana Ministry!
 
Bwana Yesu asifiwe!

Nasikitika kukufahamisha habari ya msiba wa mtoto wa Mwalimu Christopher Mwakasege. Joshua amefariki.

Alidondoka jana akitoka kazini, akapoteza fahamu na leo amefariki muda mfupi uliopita.

Mwalimu ana Semina mkoa wa Mbeya na ndio mtoto pekee wa kiume. Sio pito Jepesi

Tuwakumbuke kwa maombi.
R.i.p
 
Mhubiri3:1-8

Kuna wakati uliowekwa wa kila kitu,+ hata kuna wakati wa kila jambo chini ya mbingu: 2 wakati wa kuzaliwa+ na wakati wa kufa;+ wakati wa kupanda na wakati wa kung’oa kilichopandwa;+3 wakati wa kuua+ na wakati wa kuponya;+ wakati wa kubomoa na wakati wa kujenga;+ 4 wakati wa kulia+ na wakati wa kucheka;+ wakati wa kuomboleza+ na wakati wa kurukaruka;+ 5 wakati wa kutupa mawe+ na wakati wa kukusanya mawe;+ wakati wa kukumbatia+ na wakati wa kuepuka kukumbatia;+ 6 wakati wa kutafuta+ na wakati wa kuacha kutafuta kilichopotea; wakati wa kuweka na wakati wa kutupa;+ 7 wakati wa kupasua+ na wakati wa kushona,+ wakati wa kukaa kimya+ na wakati wa kusema;+ 8 wakati wa kupenda na wakati wa kuchukia;+ wakati wa vita+ na wakati wa amani.
 
Analo "dhehebu" la kijanjajanja...ana akili sana. Sadaka anakusanya, mafungu ya kumi anakusanya, utasemaje kuwa hana dhehebu lake binafsi? Semina zake ndio ibada zake, amecheza na akili tu ili asigombane na Lutheran lakini analo kanisa lake linaitwa Mana Ministry!
Mana ministry siijui mkuu,inawezekana ukawa sahihi coz sijawahi kusikia hilo dhehebu,na mara zote kwenye semina zake hana kawaida ya kujipambanua au kutangaza dhehebu lolote!

Kwa hiyo kama kuna dhehebu analimiliki mwenyewe basi anapaswa kuliweka wazi,hana sababu ya kuacha kulitangaza!

Ila ninachojua mpaka sasa,Christopher Mwakasege ni mwalimu,na sio Mchungaji!
 
Back
Top Bottom