Mtoto wa JK aula Etihad Airways

Mtoto wa JK aula Etihad Airways

Jiulizeni swali moja tu kasoma shule gani mpaka kafikia hapo??? Alafu leo unashangilia kitilya kuwa rumande swali je watoto wa kitilya wanafanana na wako??? Au wameshaanza kuomba mjini???

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Sina wivu.Ningekuwa na wivu nisingefundisha vijana wote hao niliofundisha na kuwakuza katika Industry hii.Iwe ndani ya Tanzania au nje ya Tanzania,wengine tupo toka enzi za East Africa Airways,uje umuonee wivu mtoto mdogo kama huyu?

Mimi nilitaka kuweka sawa tu,kuwa huyu si rubani wa Etihad,bali ni mwanafunzi wa chuo cha Urubani cha Etihad..yaani Etihad Flight College.Na akimaliza hapo sio lazima apate ajira hapo,inategemea na ufaulu wake na uhitaji wa shirika.

Sina wivu mama LadyRed
Sawa baba...
 
Hongera capt khalfan kikwete!
Najua huo urubani haujaja kirahisi rahisi bali ume-struggle! Hongera sana!
 
....mzalendo kama JAKAYA,mpaka anaingia IKULU hajasomesha mtoto ULAYA....baba Tunda
 
View attachment 538554
Moja ya darasa la wanafunzi wa urubani wa Chuo cha Etihad....

View attachment 538553
Moja kati ya ndege zao za mafunzo wakiwa chuoni.

View attachment 538552 Huyu kijana wa JK sidhani hata kama atakuwa amefikia level ya kama huyu kijana ya kuwa "Solo Pilot".Na ukiangalia begani kwa wote wawili,wana "bar" moja kuashiria bado wapo "darasani" au wapo tu chuoni kusoma na si kwamba wameajiliwa(Nipo tayari kusahihishwa ndani ya mjadala kama kaajiliwa)


Hongera sana kijana,hivi huyu ni Rashid au Khalfan!?Huwa ninawachanganya.
Hivi amepata ajira au yupo "Training" kwa ajili ya kupata masaa?Maana kwa pesa ya baba yake,sio kazi kulipa "Etihad Flying School" ili apate masaa ya kuwa rubani kamili baada ya kuwa darasani.

Maana hata ukiangalia begani ana bar moja tu,ili uwe "Pilot in Command" hapo begani lazima uwe na "Four bars".Sasa huyu dogo atakuwa ametoka tu shule huko Marekani then "field" anafanyia Etihad na mzazi akawa analilipa shirika ili mtoto apate masaa(Rating Hours) then anarudi bongo tu kurusha Boeing za ATCL.

Au anaweza akawa kwenye shule ya marubani iliyo chini ya kampuni ya ndege ya Etihad.Wakuu kuinua dude kama Boeing 737-800,Boeing 777,Boeing 787 au Airbus 380 au ile mpya A350 siyo kwa bar moja begani.Utauwa watu dakika moja tu.

Kitu kingine wazazi tunachopaswa kujua,a pilot is just a mere driver.Urubani ni kama udereva tu,training yake ni miezi sita baada ya hapo unaanza sasa kuruka ili upate masaa ya kuweza kukupa uzoefu wa kurusha ndege,unaanza kupata leseni ya kuruka ukiwa solo,then ya kuruka na abiria na baadae ndege za kibiashara.

Tatizo ni ada ilivyo ghalama.Kitu kilicho kigumu ni kuwa Engineer wa ndege na sio rubani.Ndio maana zile ndege pale nyumbani terminala one,vijana wengi waliishia kidato cha nne,sababu baba zao wana pesa,wakaenda course South Africa na USA na sasa wanarusha.

Mzee Mwinyi ana mwanae rubani,sema ile sio familia ya facebook na Instagram.

NB:Isionekane nina wivu
Well said Mkuu

Sent from my SM-N910V using JamiiForums mobile app
 
Sitakaa nipande Etihad tena....

(jok)

Hongera sana kiongozi ndoto yako soon itakuwa true,
 

kafanikiwa kupata elimu bora, matokeo yake kazi nzuri kafukuza umasikini. Watoto wetu wanaenda kwenye shule hazina vyoo na masomo uchwala, hawana matumaini ya kuuvuwa umasikini. Rais Magufuli kapigilia msumali elimu ya teens mothers kawasaliti kuwa masikini na watoto wao. Tutawashangilia watoto wao tu. Viwanda haviwezi kujengwa na watu wachache bali na taifa zima. Sasa is who you are.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Back
Top Bottom