Mtoto uleavyo ndivyo akuavyo

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,720
215,775
Jon ni mtoto wa pekee katika familia yao huyu ni kifupi cha Jonathan si Faru John, wazazi wake waliona wote wawili wakiwa 30+, baba alishafikisha 35 mama alikuwa bado kwenye 31, baba na mama Jon walisomea nje ya Tanzania na wato walirudi nyumbani kuendeleza gurudumu, walikutana katika seminar za kikazi, wote walijikuta wana mengi ya kufanana, na urafiki wao ulikuwa mkubwa kufikia mapenzi hatimae ndoa.

Baada ya harusi haikuchukua hata mwaka mmoja, mama Jon alishika ujauzito, alijifungua salama mtoto wa kiume mwenye afya njema. Jitihada za baba na mama kupata mtoto wa pili zilianza kuyeyuka Jon alipofikisha umri wa miaka 9 wakati huo mama alishagonga 40 basi aliamua tu kumshukuru Mungu.

Wakati akihangaika kutafuta mtoto, mama Jon alihudhuria ibada za makanisa yote, kama ni kufunga alifunga mpaka akawa kimodel. Tangu siku Jon anazaliwa baba Jon alishaamua kuwa baba bora. Aliacha kunywa pombe mbele ya Jon, kwani hakutaka Jon awe na mawazo kuwa pombe ni kitu kizuri mbona hata baba alikunywa.

Alipokuwa baba tu, baba Jon aliomba kubadilisha masaa yake ya kazi, aliingia kazini li saa moja kabla ya wengine ili awahi kutoka li saa moja kabla ya wenzake. Nia ya kufanya haya ni kuwahi kucheza na mtoto nyumbani, kumwogesha, kumlisha na kumsomea bed time stories. Jon na baba Jon walikuwa best friends.

Jon alipotoka jino la kwanza tu, baba yake alianza kulisafisha jino lile, mpaka meno yanaongezeka, baba Jon alimfundisha Jon kusafisha meno yake, kuvaa mwenyewe pyjama zake na vingine vingi. Jon alifundishwa kuwa kupumua mbele za watu si maadili, ukitaka kupumua unakwenda msalani, si haja tu hupeleka watu msalani.

Jon alipoanza shule, baba yake aliporudi nyumbani jioni alikagua madaftari, na kama kuna makosa waliyafanya pamoja kati kati ya wiki ama J'mosi. Kila J'mosi kuanzia saa nane Jon na baba yake walikuwa na darasa la nusu saa, hakutaka kumkomaza sana Jon akiwa mdogo, aliamini baada ya nusu saa concentration inapungua kwa watoto wadogo.

Akiwa na umri wa miaka 7, Jon alifundishwa kutandika kitanda chake na kufua nguo zake za ndani pamoja na socks kwa mkono. Jon akiwa na umri wa miaka 14 wakati huo kijana wa secondary, darasa halikuwa la baba Jon tena bali alikodi mwalimu mmoja kutoka Uganda ambae anafundisha private school, mwalimu yule alilipwa shilingi 50,000 kwakila somo alilomfundisha Jon, masomo yalikuwa English, Science na Hesabu.

Baba Jon alimpangia Jon majukumu yake, kila J'mosi kwakuwa hakwenda shule, aliachwa alale kidogo, lakini ikifika saa nne awe ameshasafisha chumba chake cha kulala, amefua nguo zake za ndani na baada ya chakula cha mchana alikuwa na masaa mawili na mwalimu nyumbani, baada ya hapo anapumzika kidogo na kuanza kupiga pasi nguo za baba, dada wa kazi aliambiwa afue tu lakini kupiga pasi nguo za baba Jon ilikuwa ni shughuli ya Jon.

Kutokana na kusali sana kwa mama Jon akiomba mtoto, alitokea kuwa mcha Mungu sana, basi yeye alimfundisha Jon upendo kuwa ndiyo amri kuu Yesu aliyoiacha duniani, hakuna silaha inayomuumiza adui yako kama kumsaidia akiwa na shida.

Mama Jon alimfundisha Jon kumshukuru Mungu kwa kila alichonacho, wapo watoto wengi ambao wamefiwa na wazazi na wanaishi kwa kwashida, pia kumshukuru Mungu kwa kusaidia wasionacho hapa duniani. Birthday zote za Jon alifundishwa kuwanunulia watoto yatima zawadi. Mama Jon mwenyewe kila mwaka alishonea watoto 10 uniform katika nyumba za yatima, na kuwanunulia vifaa vya vyote vya shule.

Jon alikuwa nyota inayowaka si shuleni, mtaani wanapoishi hadi kanisani. Wasichana wengi walimtamani Jon awe boyfriend, nani ambae hakumpenda yule mtoto kipanga? Mafundisho aliyofundishwa na mama yake kuwa usiwe na adui duniani, hata ukigombana na mtu usilale bila kuyamaliza, yalimsaidia sana Jon, kwani vijana wengi walimchukia kwakua alipendwa na vimwana.

Jon na baba Jon walikuwa wapenzi wa Arsenal na si wakati wote ulikuwa vitabu tu, hapana waliangalia mpira pia na wote wawili walikuwa na namba katika timu ya mtaani. Sherehe ambayo baba Jon atakua na familia yake hakugusa pombe kabisa, na akiwa na hamu ya bia alinunua na kunywea chumbani kwake kwa siri. Jon mpaka anakua mkubwa ukimwambia baba yako anakunywa pombe atabisha mpaka asubuhi.

Uamuzi wa Jon kusomea udaktari ulitoka moyoni kuwa ni kazi itakamsaidia kusaidia wengine, matokeo yake ya form VI yalikuwa ya kuhadithiwa, jina la Jon lilitoka mpaka kwenye magazeti na wazazi wa Jon walitafutwa na kuulizwa walimlea vipi mtoto wao?

Jon akiwa medical school alikutana na Liz ambae ni Mwingereza alikuja Tanzania kwenye elective module kuangalia huduma za afya katika nchi zinazoendelea. Liz alimpenda sana Jon, kuanzia usafi wa mwili wake, chumbani kwake, maakili ndiyo usiseme.

Liz ni mtoto wa kike peke yake katika familia ya watoto watatu, kaka zake Liz wawili ni Robert na Richard. Baba yake Liz ana pesa ndefu, si ya kumfikia Donald Trump ila next door neighbour wao ni Elton Jon. Baba yake Liz ana contract ya kusupply catering equipment kwa jeshi la Uingereza.

Liz na kaka zake wanapewa allowance kwa mwaka na baba yao ili wasimsumbue, kila January watoto wote waliwekewa £30,000 kwenye account zao. Liz alikuja Tanzania hakufikia kwenye student accommodation, alifikia Kempinsinky, Jon mwenyewe alishafahamu kuwa mtoto Liz ni maji marefu, lakini Liz ndiye alionyesha mapenzi yake yote kwa Jon.

Robert kaka wa Liz ni teja, ameshaharibiwa kabisa na madawa ya kulevya, baba yao alishatumia pesa nyingi sana kumpeleka Robert rehab katika nchi mbali mbali, lakini Robert hajawahi kuweka kitu cha kuoccupy ubongo wake, akiboreka tu yeye anawaza kuwa high, anautafuta. Hii allowance anayopewa na baba yake haikai hata miezi mitatu inakuwa imekwisha.

Richard ambae anamfuatia Robert kuzaliwa, yeye ni mtu wa totoz, pesa ikiingia January hakawii kutafuta toto la kwenda kuenjoy nalo kwenye cruz, anaweza kuzunguka dunia miezi mitatu akirudi nyumbani account iko kwenye overdraft.

Wakiwa na matatizo ya pesa baba yao anaweza kuwakopesha lakini hii inamaana allowance yako ya January itakatwa kulipia deni, utaratibu huu ulimshinda baba kwa bwana Richard, kama ni kukopa ameshakopa pesa ya miaka minne mbele.

Liz ndiye mtoto anaempa faraja baba yake, yeye starehe yake kubwa ni kwenda Ibiza summer na wanafunzi aliosoma nao A-level. Baada ya kukutana na Jon, mwaka uliofuatia Liz alikatisha holiday yake ya Ibiza, baba yake aliuliza kwanini, alimjibu hiyo pesa ninaona ni heri niitoe charity isaidie watu wenye matatizo, baba hakuamini anachosikia, kwani hiyo holiday ya Ibiza ilikuwa ni lazima kwa Liz.

Baba yake Liz alitaka kufahamu sababu hasa ya Liz kubadilika hivyo, Liz alimueleza baba yake kuwa alipokuwa Tanzania alipata boyfriend aliyemueleza maana ya kusaidia wasionacho na yeye amejiona ana umuhimu wa kujinyima kwaajili ya wengine, hata asipokwenda Ibiza haimpunguzii kitu. Baba alikuwa na hamu sana ya kumuoana huyo kijana.

Liz alifanya maandalizi ya Jon kwenda kumtembelea, Liz aliishi mwenyewe kwenye flat yake wakati huo akiwa junior doctor. Walipanga weekend ya kwenda kuwasalimia wazazi wa Liz, weekend ilifika, walifika huko, nyumba ya wazazi wa Liz ina vyumba 8 vya kulala, kuna butler na maid ambao wanaishi kwenye servant quarter.

Maid wa kina Liz ni mama wa ki-Portuguese ambae alipatwa na dharura hivyo ilimbidi aende kwao. Tangu alipoondoka shughuli nyingi za ndani zilizorota, Jon amefika anakuta wazazi wanalalamika jinsi ya kumpata mtu wa kuwapigia pasi, wiki ya pili sasa hakuna mtu wa kupiga pasi.

Jon alikunja shati na kuingia mzigoni, Liz mwenyewe hakuamini, kwa masaa mawili kijana akiwanyooshea nguo nyingi sana, baada ya masaa mawili baba Liz alimwambia hakuja kufanya kazi amekuja kuwaona, anaomba aachane na shughuli hiyo.

Waliongea mengi sana, general knowledge really, baba yake Liz alitamani sana kufahamu wazazi wa kijana huyu na jinsi walivyomlea, alitamani vijana wake wangekuwa kama huyu kijana. Baada ya holiday ya Jo kuisha, alirudi Tanzania, si muda mrefu baba na mama Liz walikuja kutembea kwa mapenzi waliyokuwa nayo kwa kijana Jon.

Urafiki wa Jon na Liz uliendelea kufikia engagement na baadae ndoa, Liz uzazi wa kwanza alipata watoto mapacha, kabla hajakaa vizuri aliinua mimba nyingine ya watoto mapacha, kulea watoto wanne wadogo haikuwa shughuli ndogo, mama Jon alihamia kabisa nyumbani kwa Jon na Liz kuwasaidia kulea, aliwaambia ni matokea ya maombi aliyofanya kuomba watoto,

Mungu hakumpa watoto wale yeye direct lakini wamekuja kupitia kwa Jon, kwakweli mama alifurahia kila sekunde ya kukaa na wajukuu na baba ilibidi awe anakuja kusalimia lakini hakai sana aliondoka. Baada ya miaka mitano ya uzazi wa mwisho Liz alipata ujauzito wa mapacha tena, jumla Jon na Liz walipata watoto sita wenye afya njema.
 
Sijaelewa mengi
Ila nimeona baba jon alikosea katika malezi kwani alimfanya mtoto wake ashabikie Arsenal, hapo alikuwa ana mfundisha vibaya mtoto.

Halafu jon alimaliza form 4 mwaka gani!? Nataka niangalie kama kweli alitoka kwa news paper
 
Sijaelewa mengi
Ila nimeona baba jon alikosea katika malezi kwani alimfanya mtoto wake ashabikie Arsenal, hapo alikuwa ana mfundisha vibaya mtoto.

Halafu jon alimaliza form 4 mwaka gani!? Nataka niangalie kama kweli alitoka kwa news paper
Hahaha, mkuu ngoja nilitafute hilo gazeti nitaliscan niliweke hapa.
 
Back
Top Bottom