Mtoto Tuntufye Mwakasaka alitutoka February 2010

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,499
86,037
Ndugu wadau, nachukua fursa hii, kuwajulisha na kuwashukuru kwa mchango wenu wa kuandika Habari za mtoto Tuntufye Julius Mwakasaka.

Nikiwa kama mjomba wa Tuntufye na ambae nimeishi nae tangu kuzaliwa kwake, nawiwa kusema kua Tuntufye Julius Mwakasaka alitutoka tarehe 17 mwezi wa Pili 2010 kule KCMC Moshi ambapo alipelekwa kwa uchunguzi zaidi wa afya yake.

Mazishi yalifanyika Lushoto- Kialilo kwa bibi yake mzaa mama; Mwalimu Esther Mshana na baadae kilio kupelekwa Mbeya.

Tulimpenda sana, alikuwa Mcheshi na mtundu sana, alikuwa rafiki wa wote ( si kwa unafiki bali kwa hali halisi) Mchokozi ili kutafuta maana na urafiki lakini pia mpole kwa mambo ambayo alikose kama Mtoto. Ninampenda kwa Binasfi yangu.

Ameacha vilio na simanzi kwa wote ZAIDI AMEWAACHIA UPWEKE Ndugu zake; Tunosye na Alice. Nakumbuka sana maneno aliyoandika Tunosye ( 10) kwenye chumba chao wakati mdogo wake huyu anaumwa, maneno haya ambayo yalikuwa faraja kwangu na kwao yalisomeka hivi : TUNTUFYE IS OUR HERO huku mengine yakisomeka kwa kifupi tu Surprise pengine waliamini baada ya ndugu yao kuzunguka na kuhangaika huku na kule angerudi na kucheza nao na pengine kwao ingekuwa kama Surprise!!
Tunaamini ameenda kupumzika baada ya shida na mateso mengi aliyoyapata.
Taarifa zaidi na picha bofya hapa: http://servetanzaniacommunity.blogspot.com/2010/03/if-tomorrow-starts-without-me.html

Nawapenda wote sana na MUNGU AWABARIKI

Elli
 
OOhhh..broda, this is so much paining!
Poleni sana broda wangu, na inapofikia hatua hii, ni lazima tuyakabidhi yote kwa Mungu, maana akili za binadamu zinakoma mahala fulani!
NARUDIA tena...SURPRISE
 
jamani machozi yamenitoka kwa uchungu
RIP Tuntufye tulikupenda lakini mungu kakupenda zaidi
 
Elli, muwe na Moyo Mkuu. Mungu ndiye anafahamu kilichomuondoa Tuntufye duniani. Kama shairi linavyosema muwe na Imani kuwa yu pamoja nanyi kiroho ijapokuwa kwa macho ya nyama hamumwoni. R.I.P Tuntufye.
I read the story and despite being a man, I could not resist pooring my tears around my face. Especially, when I figured out some of the experience of loosing someone dear to you!!
 
R.I.P Tuntufye,

Kama mzazi imeniuma sana. Na inapotokea kuwa binadamu anaumwa maradhi ambayo hayaonekani kisayansi.Oh lord, have mercy on us.
 
Poleni sana. He has gone back to be among the angels. I hope you can draw some comfort ( I know it is difficult) from the presence of his siblings.
 
Asanteni wadau, I have gone through all your comments na maneno mazuri. Thank you but we have to make sure that, in future, tunazuia vifo vya aina yoyote kwa kadiri iwezekanavyo, leave alone Mapenzi ya MUNGU.

Thank you, Ninawapenda
 
Ndugu wadau, nachukua fursa hii, kuwajulisha na kuwashukuru kwa mchango wenu wa kuandika Habari za mtoto Tuntufye Julius Mwakasaka.

Nikiwa kama mjomba wa Tuntufye na ambae nimeishi nae tangu kuzaliwa kwake, nawiwa kusema kua Tuntufye Julius Mwakasaka alitutoka tarehe 17 mwezi wa Pili 2010 kule KCMC Moshi ambapo alipelekwa kwa uchunguzi zaidi wa afya yake.

Mazishi yalifanyika Lushoto- Kialilo kwa bibi yake mzaa mama; Mwalimu Esther Mshana na baadae kilio kupelekwa Mbeya.

Tulimpenda sana, alikuwa Mcheshi na mtundu sana, alikuwa rafiki wa wote ( si kwa unafiki bali kwa hali halisi) Mchokozi ili kutafuta maana na urafiki lakini pia mpole kwa mambo ambayo alikose kama Mtoto. Ninampenda kwa Binasfi yangu.

Ameacha vilio na simanzi kwa wote ZAIDI AMEWAACHIA UPWEKE Ndugu zake; Tunosye na Alice. Nakumbuka sana maneno aliyoandika Tunosye ( 10) kwenye chumba chao wakati mdogo wake huyu anaumwa, maneno haya ambayo yalikuwa faraja kwangu na kwao yalisomeka hivi : TUNTUFYE IS OUR HERO huku mengine yakisomeka kwa kifupi tu Surprise pengine waliamini baada ya ndugu yao kuzunguka na kuhangaika huku na kule angerudi na kucheza nao na pengine kwao ingekuwa kama Surprise!!

Tunaamini ameenda kupumzika baada ya shida na mateso mengi aliyoyapata.
Taarifa zaidi na picha bofya hapa: If Tomorrow Starts without Me: For Tuntufye Mwakasaka a.k.a Mzee Mshana

Nawapenda wote sana na MUNGU AWABARIKI

Elli
Huzuni sana.

Kilio kilipelekwa Mbeya, nimekumbuka zamani sana nikiwa Mbeya, msiba uliitwa kilioni.
 
Aisee sijaelewa japo ni msiba sijui huyu Tumtufye alikuwa nani nakàfaje
 
Mimi natamani tu kufahamu maendeleo ya Tunosye! Halafu wewe Bwana PGO ulibadili username, au! Maana hili neno PGO limekuzwa sana kipindi hiki cha karibuni na akina J4 Malangahe!

Sasa wewe umeuandika huu uzi 2010, na PGO, wapi na wapi!! 🤔
 
Back
Top Bottom