Mtoto mwenye karama za ajabu aibuka jijini

Mtoto mwenye karama za ajabu aibuka jijini

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,087
Reaction score
34,884
Sheikh%20Shariff.jpg

Mtoto Sheikh Sharif Yusufu Mohammed

Maelfu ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, jana walipigana vikumbo kugombea kupata huduma ya mtoto mwenye umri wa miaka 12 anayeaminika kuwa na karama ya uponyaji kutoka kwa Mwenyezi Mungu dhidi ya magonjwa yote yanayomsumbua mwanadamu.

Nipashe ilifika jana asubuhi katika Mtaa wa Luponda, ulioko Magomeni Makuti, Wilaya ya Kinondoni na kushuhudia maelfu ya watu wa rika na jinsia tofauti wenye maradhi tofauti wakiwa wamefurika ndani na nje ya nyumba inayotumiwa na mtoto huyo kutolea huduma zake, wakisubiri kuhudumiwa.

Mtoto huyo, Sheikh Sharif Yusufu Mohammed, ambaye ni mwanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi ya Kiembesamaki, visiwani Zanzibar, amekuwa akitoa huduma yake kwa njia mbalimbali, ikiwamo kuwaombea dua (maombi) wagonjwa ili kupona maradhi yanayowasumbua.

Dua hiyo husomwa na Sheikh Sharif kwa awamu mbili tofauti; moja ikiwa ni kwa watu wote, ambayo huisoma kwa kushirikiana na wasaidizi wake na nyingine humsomea mgonjwa mmoja mmoja, huku akiwa amemuwekea mkono kichwani.

Wasaidizi wengine wa mtoto huyo ni Sheikh Salim Khamisi, maarufu kama "A'inan Mardhwiyyah", Sheikh Maulana Habshiy na Sheikh Sultan Khamisi (bwana dawa).

Njia nyingine inayotumiwa na mtoto huyo katika kuwahudumia wagonjwa, ni kuwapatia maji kwa matumizi ya kunywa kwa masharti, baada ya kuyaombea maji hayo.

Baadhi ya wagonjwa waliozungumza na Nipashe, walidai wanaamini huduma inayotolewa na mtoto huyo ni ya uhakika kwa vile kila aliyebahatika kuhudumiwa naye, alipona, wakiwamo watu waliokuwa wakisumbuliwa na maradhi sugu na yasiyotibika.

Mmoja wa wasaidizi na kaka ya mtoto huyo, Sheikh Salim Khamisi, alisema miongoni mwa wagonjwa waliokwishahudumiwa na mdogo wake, ni pamoja na mama mjamzito, mkazi wa Mabibo, jijini Dar es Salaam aliyedumu na ujauzito kwa miaka minne.

Alisema baada ya kuhudumiwa na Sheikh Sharif, hivi sasa mama huyo yuko hospitali na kwamba, uchunguzi wa kidaktari umethibitisha kuwa ana ujauzito wa watoto mapacha na anatazamiwa kujifungua wakati wowote kuanzia hivi sasa.

Kwa upande wake, Sheikh Sharif alisema karama aliyonayo, amejaliwa na Mwenyezi Mungu na kwamba, kwa karama hiyo kamwe hawezi kuthubutu kujiita yeye ni Nabii wala Mtume kwa vile anaamini kuwa Nabii Muhammad (S.A.W.) ndiye Mtume wa mwisho.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
 
Wasaidizi wengine wa mtoto huyo ni Sheikh Salim Khamisi, maarufu kama "A'inan Mardhwiyyah", Sheikh Maulana Habshiy na Sheikh Sultan Khamisi (bwana dawa).
How come Funky Sheikh Alhadj Ndjabr El Duder hayumo?
 
Hivi huyu mtoto hakuwi au ni mwingine; na kwa nini wa miaka 12. Maanake kuna mmoja naye aliwahi kuzunguka baadhi ya mikoa akiwa na umri huu! Kwa nini anatoa masharti katika kutumia hayo maji ya kunywa kwa hao wagonjwa? Shetani ndio maarufu kwa kutoa masharti!!!
 
Mkisikia yupo kondeni msiende
mkisikia yupo milimani msitoke
Aliye shambani asirudi kufuata koti lake nyumbani
......
 
hawa Shekh Sharif wapo wangapi? mbona zamani alikuwapo mwingine akihubiri hadi huko Kongo na akamsirimisha Kabila Sr.
 
Kwani hiki cheo cha sheikh hata watoto wanapewa tu? kinatokana na nini?kusomea?
 
duh! Hii kali maana hata muhamad hakuwahi kuponya magonjwa kwa jina la mwenyezi mungu...huyo dogo inakuwaje yeye apewe uwezo huo !! Hii ni noma....
 
duh! Hii kali maana hata muhamad hakuwahi kuponya magonjwa kwa jina la mwenyezi mungu...huyo dogo inakuwaje yeye apewe uwezo huo !! Hii ni noma....
 
Hata shetani naye hujigeuza na kujifanya malaika wa nuru. Asomaye na afahamu...
Kwa maana hapana jina lingine walilopewa wanadamu, litupasalo sisi kuokolewa kwalo isipokuwa JINA LA YESU.
 
uyo kaingiwa na mapepo tu. ukifika pale, taja jina la Yesu kama haujaona amekuwa chali chini anatoa mapovu. kama shetani ameweka magonjwa kwenye miili ya watu, anao pia uwezo wa kuyatoa hayo magonjwa ili kuwapiga upofu wanaofuata njia hiyo waone kama wanamfuata Mungu kumbe siyo. Mkitaka idhihirike kama kweli uyo mtoto anatumiwa na huyo mnayemwita mnyazimungu, tajeni Jina la Yesu, ataruka mashetani hadi akome...manake mashetani kiboko yao ni Jina la Yesu tu.
 
Ha ha haaaaaaaaaa.... Noted mkuu

duh! Hii kali maana hata muhamad hakuwahi kuponya magonjwa kwa jina la mwenyezi mungu...huyo dogo inakuwaje yeye apewe uwezo huo !! Hii ni noma....

Dalili za mwisho wa dunia

Hata shetani naye hujigeuza na kujifanya malaika wa nuru. Asomaye na afahamu...
Kwa maana hapana jina lingine walilopewa wanadamu, litupasalo sisi kuokolewa kwalo isipokuwa JINA LA YESU.

uyo kaingiwa na mapepo tu. ukifika pale, taja jina la Yesu kama haujaona amekuwa chali chini anatoa mapovu. kama shetani ameweka magonjwa kwenye miili ya watu, anao pia uwezo wa kuyatoa hayo magonjwa ili kuwapiga upofu wanaofuata njia hiyo waone kama wanamfuata Mungu kumbe siyo. Mkitaka idhihirike kama kweli uyo mtoto anatumiwa na huyo mnayemwita mnyazimungu, tajeni Jina la Yesu, ataruka mashetani hadi akome...manake mashetani kiboko yao ni Jina la Yesu tu.

Na nyinyi walokole si mnae Mchungaji Kakobe na mchungaji rwakatare Wanaye watowa watu Mapepo Wachafu? Mchungaji Kakobe na mchungaji rwakatare ni Manabii wa Uongo hao wanaotowa Watu Mapepo Wachafu.

Mathayo/ Chapter 24

4Yesu akawajibu, "Jihadharini msije mkadanganywa na mtu.

5 Maana wengi watatokea na kulitumia jina langu wakisema: `Mimi ndiye Kristo,` nao watawapotosha watu wengi.

11 Watatokea manabii wengi wa uongo watakaowapotosha watu wengi.
 
siku za mwisho tutasikia mengi...........BIBLE IMESEMA na hilo ni moja tu bado mengi yaja kaeni mkao wa kula
 
ukisoma matendo ya mitume some where utaona kuna mtu alikuwa akifanya miuziza kwa kutumia uchawi wake na kutibu wagoinjwa lakini alipo kuja Filipo mtume wa Yesu alim- BREACH huo uchawi wake ukadispappear halafu watu wengi wakaponywa kwa jina la Yesu. then wakaja Petro na mwanafunzi mwingine kuombea Ujazo wa Roho Mt. wale ambao walikuwa wamempokea Yesu, wote wakajazwa na matedno ya Mungu yakaonekana. yule mtu naye akaenda kwa Petro akitaka ampe pesa ili naye Petro ampe hizo karama za Roho Petro akamtimua.
 
Ndiye yule yule wa miaka ya 1990's au ni mwingine?
 
kaingiwa na majini huyo, anahitaji msaada wa haraka. akikataa msaada, tunamtandika tu kwa Jina lipitalo majina yote, Jina la Yesu Kristo Mwana wa Mungu aliye hai...utasikia kanatoa mapovu sasaivi.
 
Asikiaye na Afahamu! Maana wataokea wengi....Watasema Bwana hatukutoa pepo kwa jina lako...hatukuponya magonjwa kwa jina lako ndipo atasema...ONDOKENI KWANGU SIWAJUI NINYI
 
Back
Top Bottom