Mhifadhi mwandamizi
New Member
- Oct 26, 2022
- 1
- 1
Wakuu,
Nimesoma katika magazeti kadhaa Kwa kipindi Cha hivi karibuni habari kuhusiana na ukame unaotokana na mabadiliko Tabia ya nchi ambayo pamoja na mambo mengine yanasababishwa Kwa kiasi kikubwa sana na shughuli za Binaadamu.
Leo gazeti la JAMVILAHABARI wameandika kuhusu MTO RUVU kukaushwa na wakieleza namna mambo kama ufugaji, kilimo, ukataji miti na uchimbaji Madini unavyo athiri mto huo muhimu.
Sote tunafahamu umuhimu wa mto RUVU kwa maisha ya mwana Dar, uchumi wa Taifa na maendeleo ya nchi kwa ujumla.
Nawaomba wanajukwaa tushauriane Kwa pamoja na tufuate suluhu ya mambo haya ya Utunzaji wa mazingira.
Hivi ni Hadi lini patakuwepo na ukame huu wa kujitakia wenyewe?
Hivi Hadi lini tutaendelea kupata shida ya maji na umeme kipindi cha kiangazi?
Hivi wataalamu wetu wa Mifugo na Kilimo, wameshindwa kabisa kutengeneza mifumo kwa wadau wao Ili wafuge na walime bila kuathiri mwelekeo na mtiririko wa waji?
Hivi ni sahihi kabisa Kwa mtu kwenda kuchimba na kuchenjua Madini kwenye chanzo Cha maji?
Je hivi ni sawa kabisa Kwa mtu kichepusha mtiririko wa maji kupeleka shambani kwake Ili amwagilie maji apate hela halafu watu wanalalamika mgao?
Tutafakari pamoja
=====================
WALIVYOANDIKA JAMVI LA HABARI.
MTO RUVU UMEKAUSHWA MTO RUVU UMEKAUSHWA - Jamvi La Habari
Wakati mgao wa ,maji ukiendelea jijini Dar es salaam, hali imezidi kuwa mbaya sana katika kina cha maji kwa mto ruvu unaotegemewa kwa kiasi kikubwa kuzalisha maji jijini humo kutokana na kuharibiwa vibaya sana kwa mto huo na mito mingine midogo midogo kama mto mvuha, mgeta, Dutumi na mingine Zaidi ya 40
Uchunguzi uliofanywa na JAMVI LA HABARI umejionea namna ambavyo vyanzo hivyo muhimu vya maji vilivyoathirika huku shughuli za kibinaadamu zikiwa ni chanzo kikubwa cha uharibifu huo.
====