Mtikisiko kibano kipya cha Escrow

Mtikisiko kibano kipya cha Escrow

Mtikisiko kibano kipya cha Escrow
ippmedia.com/sw/habari/mtikisiko-kibano-kipya-cha-escrow

Hali hiyo, kwa mujibu wa chanzo cha Nipashe, tayari imezua hofu kubwa na kuwatikisa baadhi yao huku taarifa zikidai kuwa wakati wowote watuhumiwa wengine wanaweza kufikishwa kortini na pengine kuishia katika mahabusu za Keko na Segerea ikiwa watakumbana na mashtaka yasiyotoa mwanya wa kuwapo kwa dhamana.

Mwishoni mwa wiki, Mbunge wa Singida Mashariki ambaye pia Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), aligusia uwezekano wa kuwapo kwa vigogo zaidi watakaofikishwa mahakamani baada ya kuhoji hatua zilizochukuliwa hadi sasa dhidi ya wote waliofanikisha uchotwaji wa mabilioni hayo ya fedha, wakiwamo wale walioidhinisha.

Hata hivyo, wakati Lissu akihoji hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupata dhamana katika kesi yake inayohusiana na uchochezi, imebainika kuwa hakuna yeyote aliyeshiriki kufanikisha uchotwaji huo atasalimika pasi na kufikishwa mbele ya mkono wa sheria ili haki itendeke.


“Vyombo vya uchunguzi havijalala hata kidogo kuhusiana na suala hili. Uchunguzi mkali unaendelea na wapo wakubwa wengi tu wanaoweza kujikuta kortini,” chanzo cha uhakika kiliiambia Nipashe.

Hata hivyo, alipoulizwa na Nipashe jana kuhusiana na taarifa za kuwapo kwa uchunguzi zaidi dhidi ya kila aliyehusika na sakata la Escrow, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz, alisema suala hilo linashughulikiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), hivyo ni vyema mwandishi akawauliza wao.

“Suala hili linachunguzwa na PCCB (Takukuru), hivyo wanaweza kukupa majibu ukiwauliza,” alisema DCI Boaz.

Aidha, Msemaji wa Takukuru, ambayo ndiyo iliyowafikisha kortini baadhi ya watuhumiwa wa Escrow, Mussa Misalaba, aliitaka Nipashe iwe na subira kuhusiana na hilo, hasa kutokana na ukweli kuwa hakuwa katika sehemu nzuri ya kulielezea.

Hata hivyo, chanzo kilisisitiza kuwa uchunguzi zaidi unaendelea na huenda orodha ya watakaguswa itakuwa kubwa.

Aidha, chanzo kilidai kuwa kibano hicho kipya cha Escrow, kilichokaziwa pia na dhamira ya serikali ya Magufuli kupambana na rushwa bila kujali itikadi, kimeibua mtikisiko mkubwa kwa baadhi ya watuhumiwa wanaohisi kuwa hawawezi kupona dhidi ya uwezekano wa kufikishwa mahakamani.

“Kama ujuavyo, hao Takukuru sasa hivi wamecharuka kwelikweli. Na Rais (John Magufuli) kila uchao amekuwa akisisitiza nia ya serikali yake katika kuhakikisha kuwa vitendo hivi vinavyohusiana na ufisadi havipati nafasi katika serikali yake kila senti ya umma itumike kunufaisha wananchi.

“Matokeo yake, wapo waliotikiswa kwa sababu kuna taarifa kuwa wengi wako hatarini kuguswa na kibano hiki kipya,” chanzo kiliongeza.

Hivi karibuni, akiwa katika ziara zake za kikazi mkoani Kigoma, Rais Magufuli aliliigusia upya sakata la Escrow kwa kusifu ushujaa wa aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, ambaye ndiye aliyeliibua sakata hilo bungeni na kusimama kidete licha ya kuitwa tumbili.

Aidha, mmoja wa watu waliotajwa bungeni kunufaika na mgawo wa Escrow kwa kupewa zaidi ya Sh. milioni 40, na ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, Willam Ngeleja, alitangaza kuzirudisha fedha hizo kwa Mamlaka ya Kodi (TRA), akitaja sababu kuwa ni baada ya kuona kuwa aliyempatia fedha hizo amehusishwa na tuhuma za Escrow.
Kuwa na msimamo mkuu mara unafurahia hatua za Mheshimiwa Rais Magufuli sometimes ndio matusi kibao. I think unaanza kusoma alama za nyakati (If you can't beat him then join him)
 
YULE baba askofu mkuu naye atatiwa hatiani? italeta maana gani kwa kiongozi mkuu wa kididini kuhusishwa na kashfa ya fedha kama hii? Ina maana hata mafundisho yake ni tata kama haishi kulingana na anachokihubiri.
 
Halafu Zitto anapoongea maneno makali ya kuikosoa serikali hajawahi kukaa selo hata kwa nusu saa, lakini Tundu Lissu kila siku lupango. sasa rangi halisi ya Zitto inaanza kuonekana baada ya chama chake kupewa ulaji na Magufuli sasa nae anatafuta nafasi ya uwaziri. p...mbavu zake njaa haijawahi waacha ACT salama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Benki ya mkombozi iliyotumika kugawa mgao vipi? Haina kesi?

Maaskofu watatu vipi?
Na Stanbic pia wamo. Ndio waliopitisha zile za viroba, ambazo recipients wake hawajulikani.
 
vipi kuhusu gavana alieidhinisha mzigo utoke? Tibaijuka na chenge je?
Sijawaona kuwekwa ndani au kutajwa kupokea mgao. Isipokuwa Kilaini na maaskofu wengine wawili, jumla maaskofu watatu wa kanisa katoliki walitajwa na kima walichokatiwa kiliwekwa wazi humu humu JF.

Eti kweli benki ya mkombozi, zilipogawanyiwa pesa za escrow ni benki ya kanisa katoliki?
 
Benki ya mkombozi iliyotumika kugawa mgao vipi? Haina kesi?

Maaskofu watatu vipi?
Hahah! Unasubiri kina Shaban Gurumo wakishafuatiliwa useme ni udini kwasababu machoni pako makosa ni Mkombozi bank. Ila wakiguswa Simba trust itakuwa udini kwako, ndicho unasubiri. This time huyu rais ni noma hatabiriki. Your feelings will be hurt so bad this time around.
 
Kuna pengine hapagusiki, Mkombozi!!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkombozi siyo first priority. Hapo ziliwekwa tu na siyo kwamba zilikuwa za hiyo benki. Labda kama kuna tatatibu za kibenki zilivunjwa wakati wa kufungua akaunti, kuweka ama kutoa fedha nk.

Mafisadi ni waliozichukuwa pesa hizo na si vinginevyo. Waliojimilikisha hizo pesa ndo wezi na wanatakiwa kujibu tuhuma.
 
Mzee wa msoga alishasema pesa za escrow ni pesa binafsi na siyo ya umma sasa kesi ya nn?
 
Back
Top Bottom