Alipeleka na mtiririko ulifuatwa,Kwani huyu askofu alichotewa ngapi,na kama ni sadaka alizotoa kuzionyesha na kuzikabidhi ili zihesabiwe na kupangiwa matumizi na halmashauri ya kanisa ktk diocese yake? Boss wake,askofu mkuu alikuwa na habari na fedha hizo? Kama ni fungu la kumi,alizionyesha wapi! Kama hazikwenda ktk mtiririko huo kwa mujibu wa kazi yake anapaswa nae kujieleza!
Sent using Jamii Forums mobile app
Aanze na Kikwete ndipo tutajua sio usaniiKilaini ndani?
Bank kwani ndio iliyoweka pesa? Wahusika ni walioweka pesa sio bank pesa zilipowekwaBenki ya mkombozi iliyotumika kugawa mgao vipi? Haina kesi?
Maaskofu watatu vipi?
Kilaini ndani?
Bila kuwaunganisha walioidhinisha malipo tajwa kesi tajwa haina mashiko. Ni kesi mfu.Mtikisiko kibano kipya cha Escrow
ippmedia.com/sw/habari/mtikisiko-kibano-kipya-cha-escrow
Hali hiyo, kwa mujibu wa chanzo cha Nipashe, tayari imezua hofu kubwa na kuwatikisa baadhi yao huku taarifa zikidai kuwa wakati wowote watuhumiwa wengine wanaweza kufikishwa kortini na pengine kuishia katika mahabusu za Keko na Segerea ikiwa watakumbana na mashtaka yasiyotoa mwanya wa kuwapo kwa dhamana.
Mwishoni mwa wiki, Mbunge wa Singida Mashariki ambaye pia Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), aligusia uwezekano wa kuwapo kwa vigogo zaidi watakaofikishwa mahakamani baada ya kuhoji hatua zilizochukuliwa hadi sasa dhidi ya wote waliofanikisha uchotwaji wa mabilioni hayo ya fedha, wakiwamo wale walioidhinisha.
Hata hivyo, wakati Lissu akihoji hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupata dhamana katika kesi yake inayohusiana na uchochezi, imebainika kuwa hakuna yeyote aliyeshiriki kufanikisha uchotwaji huo atasalimika pasi na kufikishwa mbele ya mkono wa sheria ili haki itendeke.
“Vyombo vya uchunguzi havijalala hata kidogo kuhusiana na suala hili. Uchunguzi mkali unaendelea na wapo wakubwa wengi tu wanaoweza kujikuta kortini,” chanzo cha uhakika kiliiambia Nipashe.
Hata hivyo, alipoulizwa na Nipashe jana kuhusiana na taarifa za kuwapo kwa uchunguzi zaidi dhidi ya kila aliyehusika na sakata la Escrow, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz, alisema suala hilo linashughulikiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), hivyo ni vyema mwandishi akawauliza wao.
“Suala hili linachunguzwa na PCCB (Takukuru), hivyo wanaweza kukupa majibu ukiwauliza,” alisema DCI Boaz.
Aidha, Msemaji wa Takukuru, ambayo ndiyo iliyowafikisha kortini baadhi ya watuhumiwa wa Escrow, Mussa Misalaba, aliitaka Nipashe iwe na subira kuhusiana na hilo, hasa kutokana na ukweli kuwa hakuwa katika sehemu nzuri ya kulielezea.
Hata hivyo, chanzo kilisisitiza kuwa uchunguzi zaidi unaendelea na huenda orodha ya watakaguswa itakuwa kubwa.
Aidha, chanzo kilidai kuwa kibano hicho kipya cha Escrow, kilichokaziwa pia na dhamira ya serikali ya Magufuli kupambana na rushwa bila kujali itikadi, kimeibua mtikisiko mkubwa kwa baadhi ya watuhumiwa wanaohisi kuwa hawawezi kupona dhidi ya uwezekano wa kufikishwa mahakamani.
“Kama ujuavyo, hao Takukuru sasa hivi wamecharuka kwelikweli. Na Rais (John Magufuli) kila uchao amekuwa akisisitiza nia ya serikali yake katika kuhakikisha kuwa vitendo hivi vinavyohusiana na ufisadi havipati nafasi katika serikali yake kila senti ya umma itumike kunufaisha wananchi.
“Matokeo yake, wapo waliotikiswa kwa sababu kuna taarifa kuwa wengi wako hatarini kuguswa na kibano hiki kipya,” chanzo kiliongeza.
Hivi karibuni, akiwa katika ziara zake za kikazi mkoani Kigoma, Rais Magufuli aliliigusia upya sakata la Escrow kwa kusifu ushujaa wa aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, ambaye ndiye aliyeliibua sakata hilo bungeni na kusimama kidete licha ya kuitwa tumbili.
Aidha, mmoja wa watu waliotajwa bungeni kunufaika na mgawo wa Escrow kwa kupewa zaidi ya Sh. milioni 40, na ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, Willam Ngeleja, alitangaza kuzirudisha fedha hizo kwa Mamlaka ya Kodi (TRA), akitaja sababu kuwa ni baada ya kuona kuwa aliyempatia fedha hizo amehusishwa na tuhuma za Escrow.
Hao walosema pesa si za umma ndo wakuanza nao kwani walichangia kuwatia viburi na jeuri wale waliochota pesaSiyo kwamba anauchukia ukristu,huo ndio ukweli hapa kinachotakiwa ni wathumiwa wote kuchukuliwa hatua na si habari kwamba ni kiongozi wa dhehebu gani,lakini pia haki itendeka asiachwe hata mtu mmoja kwenye sakata hili,hata wale waliosema pesa si za Umma wanatakiwa wachukuliwe hatua.
hah hah umenikumbusha Kanali Lubinga na kifaru cha jeshi..Ushuhuda ni wao ndio watakaoulezea umma!
Aliidhinisha au umemeza maharagwe ya Chunya? Msaada kwa kanisa siyo ufisadi kuupokeaKilaini ndani?
Maaskofu waliidhinisha au hujui jinai ni niniBenki ya mkombozi iliyotumika kugawa mgao vipi? Haina kesi?
Maaskofu watatu vipi?
Kilaini ndani?
Kilaini ndani?
Ndio waliosaini BOT.?Benki ya mkombozi iliyotumika kugawa mgao vipi? Haina kesi?
Maaskofu watatu vipi?
nataka nimpime magufuli hapa kwenye kuwashughulikia wakatoliki.

Mkuu mbona hakuna jipya?Mtikisiko kibano kipya cha Escrow
ippmedia.com/sw/habari/mtikisiko-kibano-kipya-cha-escrow
Hali hiyo, kwa mujibu wa chanzo cha Nipashe, tayari imezua hofu kubwa na kuwatikisa baadhi yao huku taarifa zikidai kuwa wakati wowote watuhumiwa wengine wanaweza kufikishwa kortini na pengine kuishia katika mahabusu za Keko na Segerea ikiwa watakumbana na mashtaka yasiyotoa mwanya wa kuwapo kwa dhamana.
Mwishoni mwa wiki, Mbunge wa Singida Mashariki ambaye pia Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), aligusia uwezekano wa kuwapo kwa vigogo zaidi watakaofikishwa mahakamani baada ya kuhoji hatua zilizochukuliwa hadi sasa dhidi ya wote waliofanikisha uchotwaji wa mabilioni hayo ya fedha, wakiwamo wale walioidhinisha.
Hata hivyo, wakati Lissu akihoji hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupata dhamana katika kesi yake inayohusiana na uchochezi, imebainika kuwa hakuna yeyote aliyeshiriki kufanikisha uchotwaji huo atasalimika pasi na kufikishwa mbele ya mkono wa sheria ili haki itendeke.
“Vyombo vya uchunguzi havijalala hata kidogo kuhusiana na suala hili. Uchunguzi mkali unaendelea na wapo wakubwa wengi tu wanaoweza kujikuta kortini,” chanzo cha uhakika kiliiambia Nipashe.
Hata hivyo, alipoulizwa na Nipashe jana kuhusiana na taarifa za kuwapo kwa uchunguzi zaidi dhidi ya kila aliyehusika na sakata la Escrow, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz, alisema suala hilo linashughulikiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), hivyo ni vyema mwandishi akawauliza wao.
“Suala hili linachunguzwa na PCCB (Takukuru), hivyo wanaweza kukupa majibu ukiwauliza,” alisema DCI Boaz.
Aidha, Msemaji wa Takukuru, ambayo ndiyo iliyowafikisha kortini baadhi ya watuhumiwa wa Escrow, Mussa Misalaba, aliitaka Nipashe iwe na subira kuhusiana na hilo, hasa kutokana na ukweli kuwa hakuwa katika sehemu nzuri ya kulielezea.
Hata hivyo, chanzo kilisisitiza kuwa uchunguzi zaidi unaendelea na huenda orodha ya watakaguswa itakuwa kubwa.
Aidha, chanzo kilidai kuwa kibano hicho kipya cha Escrow, kilichokaziwa pia na dhamira ya serikali ya Magufuli kupambana na rushwa bila kujali itikadi, kimeibua mtikisiko mkubwa kwa baadhi ya watuhumiwa wanaohisi kuwa hawawezi kupona dhidi ya uwezekano wa kufikishwa mahakamani.
“Kama ujuavyo, hao Takukuru sasa hivi wamecharuka kwelikweli. Na Rais (John Magufuli) kila uchao amekuwa akisisitiza nia ya serikali yake katika kuhakikisha kuwa vitendo hivi vinavyohusiana na ufisadi havipati nafasi katika serikali yake kila senti ya umma itumike kunufaisha wananchi.
“Matokeo yake, wapo waliotikiswa kwa sababu kuna taarifa kuwa wengi wako hatarini kuguswa na kibano hiki kipya,” chanzo kiliongeza.
Hivi karibuni, akiwa katika ziara zake za kikazi mkoani Kigoma, Rais Magufuli aliliigusia upya sakata la Escrow kwa kusifu ushujaa wa aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, ambaye ndiye aliyeliibua sakata hilo bungeni na kusimama kidete licha ya kuitwa tumbili.
Aidha, mmoja wa watu waliotajwa bungeni kunufaika na mgawo wa Escrow kwa kupewa zaidi ya Sh. milioni 40, na ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, Willam Ngeleja, alitangaza kuzirudisha fedha hizo kwa Mamlaka ya Kodi (TRA), akitaja sababu kuwa ni baada ya kuona kuwa aliyempatia fedha hizo amehusishwa na tuhuma za Escrow.
VIP kuhusu mkwere, Na ile kampuni ya simba whatever hivi mmiliki wake ni Nani?Kilaini ndani?