Mtikisiko kibano kipya cha Escrow

Mtikisiko kibano kipya cha Escrow

Siyo kwamba anauchukia ukristu,huo ndio ukweli hapa kinachotakiwa ni wathumiwa wote kuchukuliwa hatua na si habari kwamba ni kiongozi wa dhehebu gani,lakini pia haki itendeka asiachwe hata mtu mmoja kwenye sakata hili,hata wale waliosema pesa si za Umma wanatakiwa wachukuliwe hatua.

Mimi naona maigizo tu, hivi kuna kifungu kinacho kataza mtu kupokea pesa uliyopewa ikiwa pesa hiyo ni halali na mkuu wa nchi alilihutubia taifa na kuthibitisha kuwa siyo ya pesa siyo ya umma?, je hawa watuhumiwa hawawezi kuepuka adhabu kwa kuwa mkuu wa nchi alishawahakikishia fedha walizopewa ni halali?
Benki ya mkombozi iliyotumika kugawa mgao vipi? Haina kesi?

Maaskofu watatu vipi?

Hapo hakuna kesi kwa kuwa rais alilihakikishia taifa na kuwahakikishia watz wote waliokuwa na wasiwasi kuhusu pesa hizi siyo za umma na wanaweza kuzitumia kwa mambo yao binafsi
 
Ngoja tuone Mkuu kama kweli huyu anayejinadi kama ni mpambanaji na mafisadi atagusa kila mtu, lakini naye ni fisadi pia hapo ndiyo ngoma inogile.
Akizungumza na wanaccm wenye njaa wa jijini DSM , kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee , ambao walipachikwa jina la uongo la wazee wa DSM , Profesa Kikwete alisema PESA ZILE HAZIKUWA PESA ZA UMMA .
 
Kilaini ndani?
Nadhani kilaini alipelekewa sadaka, hakupewa rushwa, sidhani kama alikuwa na ushawishi wowote katika utoaji hizo pesa. Sidhani kama kwa namna yoyote alishiriki uchotwaji yeye alipelekewa sadaka fungu la kumi labda.

Muhimu sana wale wa ile benki nyingine. Waliobeba kwenye mifuko.
 
nataka nimpime magufuli hapa kwenye kuwashughulikia wakatoliki.
 
Nadhani kilaini alipelekewa sadaka, hakupewa rushwa, sidhani kama alikuwa na ushawishi wowote katika utoaji hizo pesa. Sidhani kama kwa namna yoyote alishiriki uchotwaji yeye alipelekewa sadaka fungu la kumi labda.

Muhimu sana wale wa ile benki nyingine. Waliobeba kwenye mifuko.
haya maelezo atayatoa mahakamani.
 
Siyo kwamba anauchukia ukristu,huo ndio ukweli hapa kinachotakiwa ni wathumiwa wote kuchukuliwa hatua na si habari kwamba ni kiongozi wa dhehebu gani,lakini pia haki itendeka asiachwe hata mtu mmoja kwenye sakata hili,hata wale waliosema pesa si za Umma wanatakiwa wachukuliwe hatua.
Mbona wa Stanbic hawataji?
 
Back
Top Bottom