Mtikisiko kibano kipya cha Escrow

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,007
Mtikisiko kibano kipya cha Escrow
ippmedia.com/sw/habari/mtikisiko-kibano-kipya-cha-escrow

Hali hiyo, kwa mujibu wa chanzo cha Nipashe, tayari imezua hofu kubwa na kuwatikisa baadhi yao huku taarifa zikidai kuwa wakati wowote watuhumiwa wengine wanaweza kufikishwa kortini na pengine kuishia katika mahabusu za Keko na Segerea ikiwa watakumbana na mashtaka yasiyotoa mwanya wa kuwapo kwa dhamana.

Mwishoni mwa wiki, Mbunge wa Singida Mashariki ambaye pia Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), aligusia uwezekano wa kuwapo kwa vigogo zaidi watakaofikishwa mahakamani baada ya kuhoji hatua zilizochukuliwa hadi sasa dhidi ya wote waliofanikisha uchotwaji wa mabilioni hayo ya fedha, wakiwamo wale walioidhinisha.

Hata hivyo, wakati Lissu akihoji hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupata dhamana katika kesi yake inayohusiana na uchochezi, imebainika kuwa hakuna yeyote aliyeshiriki kufanikisha uchotwaji huo atasalimika pasi na kufikishwa mbele ya mkono wa sheria ili haki itendeke.


“Vyombo vya uchunguzi havijalala hata kidogo kuhusiana na suala hili. Uchunguzi mkali unaendelea na wapo wakubwa wengi tu wanaoweza kujikuta kortini,” chanzo cha uhakika kiliiambia Nipashe.

Hata hivyo, alipoulizwa na Nipashe jana kuhusiana na taarifa za kuwapo kwa uchunguzi zaidi dhidi ya kila aliyehusika na sakata la Escrow, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz, alisema suala hilo linashughulikiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), hivyo ni vyema mwandishi akawauliza wao.

“Suala hili linachunguzwa na PCCB (Takukuru), hivyo wanaweza kukupa majibu ukiwauliza,” alisema DCI Boaz.

Aidha, Msemaji wa Takukuru, ambayo ndiyo iliyowafikisha kortini baadhi ya watuhumiwa wa Escrow, Mussa Misalaba, aliitaka Nipashe iwe na subira kuhusiana na hilo, hasa kutokana na ukweli kuwa hakuwa katika sehemu nzuri ya kulielezea.

Hata hivyo, chanzo kilisisitiza kuwa uchunguzi zaidi unaendelea na huenda orodha ya watakaguswa itakuwa kubwa.

Aidha, chanzo kilidai kuwa kibano hicho kipya cha Escrow, kilichokaziwa pia na dhamira ya serikali ya Magufuli kupambana na rushwa bila kujali itikadi, kimeibua mtikisiko mkubwa kwa baadhi ya watuhumiwa wanaohisi kuwa hawawezi kupona dhidi ya uwezekano wa kufikishwa mahakamani.

“Kama ujuavyo, hao Takukuru sasa hivi wamecharuka kwelikweli. Na Rais (John Magufuli) kila uchao amekuwa akisisitiza nia ya serikali yake katika kuhakikisha kuwa vitendo hivi vinavyohusiana na ufisadi havipati nafasi katika serikali yake kila senti ya umma itumike kunufaisha wananchi.

“Matokeo yake, wapo waliotikiswa kwa sababu kuna taarifa kuwa wengi wako hatarini kuguswa na kibano hiki kipya,” chanzo kiliongeza.

Hivi karibuni, akiwa katika ziara zake za kikazi mkoani Kigoma, Rais Magufuli aliliigusia upya sakata la Escrow kwa kusifu ushujaa wa aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, ambaye ndiye aliyeliibua sakata hilo bungeni na kusimama kidete licha ya kuitwa tumbili.

Aidha, mmoja wa watu waliotajwa bungeni kunufaika na mgawo wa Escrow kwa kupewa zaidi ya Sh. milioni 40, na ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, Willam Ngeleja, alitangaza kuzirudisha fedha hizo kwa Mamlaka ya Kodi (TRA), akitaja sababu kuwa ni baada ya kuona kuwa aliyempatia fedha hizo amehusishwa na tuhuma za Escrow.
 
Your spoiling the movie!

"the highest risk should give maximum profit"
 
PCCB fanyeni yenu,hizo hela zikirudishwa zinaweza lipia nyongeza ya mishahara,kujenga miundombinu na kusomesha vijana wetu!
 
Ngoja tuone Mkuu kama kweli huyu anayejinadi kama ni mpambanaji na mafisadi atagusa kila mtu, lakini naye ni fisadi pia hapo ndiyo ngoma inogile.

kila nikimtazamaaaa halafu nikimtazama na joka lenye makengeza naishia kucheka tu..... maana lile jamaa la Harvard kila dili limepiga na hakuna wakuligusa..... haya Said Lugumi nae vipi? takukuru hawamuoni? hapa kuna booooooooonge la tamthilia la kikorea linaendelea steling anaitwa kang yi kyung na adui mkuu ni pacha wake wasiejuana anaeitwa kang se yeone.... hahahah ila kama kawaida yetu sisi ni wadanganyika......na wanafiki tuliotukuka kuna kipindi zitto alifikia hatua ya kusema rais anaendesha nchi bila kua hata na mpango kazi pia hafati katiba, pia anakula na kulala bure ikulu haioni njaa na dhiki zinazowatesa watanzania, pia akasema rais anaongea mno yaani anaropoka saana baada ya kuwatimua wale madogo Udom na kusema kua serikali yake haitosomesha vilaza..... leo mnafiki zitto anamsifia saaana malaika mkuu na kusema yupo sahihi na anaongoza nchi vizzuuuuri saana.... huu unafiki wa akina zito na pro pesa na wengi wao utaendelea kulitafuna taifa na tutapata dhiki saana....mpaka tutubu
 
Kuna pesa imekaa tu tangu 2013? Sidhani weeee hawa wa 40m labda ndio wanweza kulipa kwa mipango yao mingine!! Wale wa 1.6Bil zitakuwa zimezungushwa hasa Majengo makubwa ya biashara!! Kazi ipo!!!
PCCB fanyeni yenu,hizo hela zikirudishwa zinaweza lipia nyongeza ya mishahara,kujenga miundombinu na kusomesha vijana wetu!
 
unalichukia sana Kanisa?

Msafwa
Mpoloto, Mbeya

Siyo kwamba anauchukia ukristu,huo ndio ukweli hapa kinachotakiwa ni wathumiwa wote kuchukuliwa hatua na si habari kwamba ni kiongozi wa dhehebu gani,lakini pia haki itendeka asiachwe hata mtu mmoja kwenye sakata hili,hata wale waliosema pesa si za Umma wanatakiwa wachukuliwe hatua.
 
Huu utakuwa mtikisiko

si mpaka uwe huo mtikisiko unaoufikiria ndani ya akili yako? we nae unajiita grat thinker halafu unashindwa hata kuona haya maigizo? wanaotakiwa kubaki salama ni wale tu ambao katiba inawalinda tena ni wawili tu ambao malaika mkuu na mtukufu kasema tusiwataje tuwaache wapumzike wazee wetu hao wamfenya kazi ngumu saana za kuijenga nchi na mmoja wao juzijuzi kule chato alituita tena kua sisi ni wapumbavu na zile nyumba pengine zitasaidia kupunguza upumbavu wetu......haya nenda ikulu yoote nani atabaki salama.... then nenda BOT anza na gavana pamoja na wasaidizi wao nani atabaki salama, nenda kwa aliekua waziri wa fedha sada mkuya na wale wasaidizi wake akiwemo comrade Nchemba..... hapo hujaenda bungeni.... kutana na akina tibaijuka, chenge, naskia hadi zitto kuna mtu alimtuma akamchukulie hela yake ya kahawa kwa sauti ya mheshimiwa mzee wa vijembe kwa upinzani bwana LUsinde, hapo hujaenda makanisani.........

hapa kuna wachache tu wanaotafutwa hakuna cha nchi kutikisika wala nini...........use ajmi chakra to see the unseen by your physical eyes.
 
Back
Top Bottom