Mtikisiko kibano kipya cha Escrow

Mtikisiko kibano kipya cha Escrow

PCCB fanyeni yenu,hizo hela zikirudishwa zinaweza lipia nyongeza ya mishahara,kujenga miundombinu na kusomesha vijana wetu!

wezi na mafisadi haitakiwi kusamehewa kama wale walioiba pesa ya epa wakaambiwa warudishe bila kufikishwa mahakamani......

inatakiwa sheria ichukue mkondo wake...
 
Kuweka hii article hapa kutoka gazetini haina maana ninafurahia chochote kile katika utawala huu wa mabavu wa dikteta uchwara. Usipotoshe msimamo wangu hata kwa sekunde moja.

Kuwa na msimamo mkuu mara unafurahia hatua za Mheshimiwa Rais Magufuli sometimes ndio matusi kibao. I think unaanza kusoma alama za nyakati (If you can't beat him then join him)
 
Mimi naona maigizo tu, hivi kuna kifungu kinacho kataza mtu kupokea pesa uliyopewa ikiwa pesa hiyo ni halali na mkuu wa nchi alilihutubia taifa na kuthibitisha kuwa siyo ya pesa siyo ya umma?, je hawa watuhumiwa hawawezi kuepuka adhabu kwa kuwa mkuu wa nchi alishawahakikishia fedha walizopewa ni halali?

Hapo hakuna kesi kwa kuwa rais alilihakikishia taifa na kuwahakikishia watz wote waliokuwa na wasiwasi kuhusu pesa hizi siyo za umma na wanaweza kuzitumia kwa mambo yao binafsi

mkuu
zipo taratibu za mtumishi wa serikali anatakiwa kuzifanya... ndio maana ukimsikiliza ngereja utaona ni kwa nini amezirudisha zile pesa za eskrow...
pia ht wale wakatoriki wanahaki ya kusema ilikuwa sadaka

je pesa chafu au pesa ya serikali ni halali watukugawana!?
 
Benki ya mkombozi iliyotumika kugawa mgao vipi? Haina kesi?

Maaskofu watatu vipi?
kwani Mkombozi na Kilaini walichota pesa? Mkombozi ilikuwa na haki ya kutekeleza maagizo ya mteja wake tena ilifanya kazi kufuata taratibu za kibenki kupitia accounts sahihi za wateja, sasa kosa lao ni nini? Bibi Faiza kwanini hujasema Benki ya stanbick iliyotoa fedha kwenye mifuko?
Acha udini na roho mbaya bibi wewe. Halafu eti Kilaini ndani, hujaona wengine? Ndiyo utashangaa kupambana na hali yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kila nikimtazamaaaa halafu nikimtazama na joka lenye makengeza naishia kucheka tu..... maana lile jamaa la Harvard kila dili limepiga na hakuna wakuligusa..... haya Said Lugumi nae vipi? takukuru hawamuoni? hapa kuna booooooooonge la tamthilia la kikorea linaendelea steling anaitwa kang yi kyung na adui mkuu ni pacha wake wasiejuana anaeitwa kang se yeone.... hahahah ila kama kawaida yetu sisi ni wadanganyika......na wanafiki tuliotukuka kuna kipindi zitto alifikia hatua ya kusema rais anaendesha nchi bila kua hata na mpango kazi pia hafati katiba, pia anakula na kulala bure ikulu haioni njaa na dhiki zinazowatesa watanzania, pia akasema rais anaongea mno yaani anaropoka saana baada ya kuwatimua wale madogo Udom na kusema kua serikali yake haitosomesha vilaza..... leo mnafiki zitto anamsifia saaana malaika mkuu na kusema yupo sahihi na anaongoza nchi vizzuuuuri saana.... huu unafiki wa akina zito na pro pesa na wengi wao utaendelea kulitafuna taifa na tutapata dhiki saana....mpaka tutubu
Lugumi inasemekana anatoka mitaa ya CALL ME J!!
 
Hivi ni wapi askofu Kilaini, Nzingirwa na padri waliwahi kusaini makaratasi ya serikali! Au hayo ya escrow au Pap, au iptl!!? Kuna kitu mgongano wa kimaslahi, hakipo hapo! Kwa waliokuwa watumishi wa serikali wakati huo au kabla huenda hao! Nani miongoni mwenu aliwahi peleka sadaka kwenye nyumba za ibada akaulizwa alikozitoa?!
 
kwani Mkombozi na Kilaini walichota pesa? Mkombozi ilikuwa na haki ya kutekeleza maagizo ya mteja wake tena ilifanya kazi kufuata taratibu za kibenki kupitia accounts sahihi za wateja, sasa kosa lao ni nini? Bibi Faiza kwanini hujasema Benki ya stanbick iliyotoa fedha kwenye mifuko?
Acha udini na roho mbaya bibi wewe. Halafu eti Kilaini ndani, hujaona wengine? Ndiyo utashangaa kupambana na hali yako

Sent using Jamii Forums mobile app
Unaonesha husomi habari zinazoshushwa JF. Kuna habari ililetwa humu, kuna mmoja wa kati ya waliotajwa kupewa mgao alisema, anashangaa kuwa na account na kuwekewa pesa benki ya mkombozi kwa jina lake kwakuwa yeye hajawahi kufunguwa account benki ya mkombozi!

Sasa jiulize, mkombozi walitumia vigezo vipi kumfungulia hiyo account?
 
nasikitika namna Magufuli anavyokukosesha amani ya maisha..
tangu awamu ya 5 iingie sioni vurugu zako humu mtandaoni..

Msafwa
Mpoloto, Mbeya
Sheria za mitandao zilibadilishwa muda mchache kabla ya awamu ya tano kuingia madarakani. Kumbuka hilo.
 
Back
Top Bottom