Mtikisiko CHADEMA: Harakati mpya zaibuka

Mtikisiko CHADEMA: Harakati mpya zaibuka

Usuluhishi gani na watovu wa nidhamu?

Wasaliti wanaandika habari na kuihariri wao wenyewe.

Habari hii itoshe kupuuzwa tu

Nikweli kiongozi lazima ifike mahali maamuzi ya chama ya heshimiwe. Imefika mahali sasa wanajiandikia story wenyewe kwenye magezeti kuonyesha kuna kundi kubwa linawaunga mkono kumbe ni janja yao tu. Tusikubali kuyumbishwa kama wanajiona wasomi basi wakaanzishe chama chao cha wasomi.
 
Tunapaswa kuchunguza mgogoro wa CHADEMA kwa tahadhari kubwa tukiangalia uwezekano wa kuchochewa na yafuatayo;

1. Uchu wa fedha (Ruzuku), kwamba wanaoitwa wasaliti wanataka wapate kujikwamua kiuchumi baada ya kupata madaraka. Wengi wao ni vijana wanaotegemea siasa kama njia ya kujikwamua kiuchumi (tuhuma za hongo).

2. Uchu wa madaraka, kwamba wanaoitwa wasaliti wanajiona ni wasomi hivyo wanataka nafasi za juu hata kama ni wasomi wapumbavu (siyo wasomi wote wenye vyeti wanaweza kufanikisha mambo). Zingatia ustawi na mafanikio ya chama kwenye maeneo yao.

3. Chama tawala kwa kutumia serikali yake na vyombo vya dola kinatumia madhaifu yaliyotajwa hapo juu (1&2) kujihakikishia udhibiti wa upinzani (Zingatia matamko mbali mbali ya viongozi hata mawaziri kuhusu kusambaratika kwa CHADEMA.
 
hadi raia mwema limekua gazeti la kidaku.!!??

sasa hivi nisomage tu mwanaspoti basi.!!
 
Huyu mwandishi nae mweu "KAMBI YA WASOMI" siku hizi kila mtu amesoma hata madiwani wanabachelor, bodaboda wanabachelor, hakuna cha wasomi wala nn!! Walio watimua ni wasomi nasisi wafuasi wao (CDM) ni wasomi. Fukuzisha mdudu mbali kwa DUMU.
 
Kwa ushauri huu uliotoa wewe lazima ni Gamba nia yako CDM ife.

Mimi ni MTz kwa kuzaliwa na kama ikilazimu Mtanganyika kwa asili. Haya ya siasa tunalazimika tu kwa sababu ni sehemu ya maisha uwe unapenda au hupendi siasa itakugusa maishani.

Hata hivyo una uhuru wa kutoa mawazo yako na nina lazimika kuheshimu huo uhuru wako.
 
sisi wanachama tutamfukuza subiri uone. CDM sio CCM inalala na mizoga

hapo sawa mkuu. CDM kwa kutumia katiba kitamfukuza ZZK. Nilishtuka kuiona kauli kuwa hakuna mtu wa kumfukuza zzk.
 
Hizi habari zina dhihirisha nia halisi ya ZZK ambayo ni kete ya CCM, kubomoa chama!!
Namuomba Dr Baregu asijihusishe
na hao wasliti, ajiweke mbali tusimfikilie vibaya!!
Mbinu zote za MaCCM zimefeli, wameshikilia ndago, wasaliti wanazama!!!
 
Mwandishi usitutishie up.umbavu eti 'wasomi'hawa wanaotuuza kwa wakoloni weusi hata kama watasoma wawe na mapembe hatuwakubali wasaliti!!
 
Tatizo letu watanzania tunapenda kufananisha migogoro, mgogoro wa NCCR kipindi kile ni tofauti kabisa na huu wa CDM na mimi sioni kama hawa CDM wanamgogoro hii ni kawaida tu kwenye taasisi kutokea mambo kama haya, mimi naamini kama Mbowe analaumiwa sana hao wanaomlaumu au wanaodhani wameonewa nawaomba wajiondoe hafu waanzishe chama chao ndio waone shughuli ya kuwa na chama. Zito namheshim sana bado ni kijana kama anahitaji kuendela na siasa ahamie chama ambacho anadhani atafanikiwa zaidi. Ila siasa ya Tanzania haikui kwani tuna watu amabao wandhani ukimpinga kimawazo basi wewe ni adui.









328_slaa.jpg



  • Mkakati wa usuluhishi waandaliwa





JUHUDI za chini kwa chini kusuluhisha kambi zinazokwaruzana katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), chini ya mwavuli wa usaliti zimeanza kuchukua nafasi yake, Raia Mwema, limebaini.
Kambi zinazosuguana kwa sasa chini ya kivuli hicho cha usaliti ni ile inayodaiwa kuwa ya Mwenyekiti, Freeman Mbowe, inayouwanganisha wabunge Tundu Lissu, Peter Msigwa, Godbless Lema, John Mnyika na Katibu Mkuu Dk. Wilbroad Slaa, ambayo inajitambulisha kwa ‘kete’ ya kudhibiti usaliti dhidi ya chama hicho.
Kambi nyingine ni ile ya Kabwe Zitto, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, yenye wasomi wengi inayotajwa kumuandaa Zitto kuwania nafasi ya uenyekiti wa chama hicho kikuu cha upinzani ili kumng’oa mwenyekiti wa sasa Mbowe, kama naye atajitosa kugombea tena wadhifa huo.
Miongoni mwa wasomi wanaotajwa kuwamo katka kambi hiyo ni pamoja na mwanasiasa mkongwe wa mageuzi nchini, Profesa Mwesiga Baregu na msomi mwingine aliyekwishajeruhiwa kisiasa ndani ya chama hicho, Dk. Kitila Mkumbo.
Hata hivyo, pamoja na juhudi hizo za usuluhishi wa kambi hizo mbili zinazoendelea chini kwa chini, kuna uwezekano mkubwa viongozi wa juu wa chama hicho, wakiongozwa na Mbowe, kususia usuluhishi huo na kama itakuwa hivyo, basi katika kipindi cha siku chache zijazo, hatari ya chama hicho kuzidi kupasuka ni kubwa.
Viongozi wakongwe katika masuala ya mageuzi nchini waliozungumza na gazeti hili wiki hii, wamefananisha kinachoendelea sasa ndani ya chama hicho na kilichokitokea chama cha NCCR-Mageuzi mwishoni mwa miaka ya 1990.
Wakati huo, NCCR kilikuwa ndiyo chama kikuu cha upinzani hapa nchini, chini ya uenyekiti wa Augustine Mrema, lakini mgogoro mkubwa uliokikumba ulimlazimu akihame chama hicho na kujiunga chama cha TLP na kuhama kwake kukawa mwisho wake wa kisiasa na mwisho wa nguvu kubwa za chama hicho cha mageuzi.
Mmoja wa wanasiasa wa mashuhuri wa kambi ya upinzani nchini ambaye amejitolea kusuluhisha mgogoro kati ya kambi inayotajwa kuwa ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na ile inayoongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, amesema haoni uwezekano wa CHADEMA kutopasuka endapo hali ya sasa itaendelea.
Kila anachofanya Mbowe kwa sasa kinafanana kabisa na kile alichokuwa akifanya Mrema. Wakati ule, Mrema alikataa kuwasikiliza wanasiasa waliokuwa na mrengo wa kisomi kama vile akina Dk. Sengondo Mvungi (sasa marehemu) na Mabere Marando na akawa anawasikiliza ‘makomandoo’ wa kisiasa.
Kwake, aliona wasomi wananyatia tu nafasi yake. Matokeo yake akawafanya kuwa maadui zake lakini wenzake walimshauri kwa nia njema tu. Taarifa zilizopo zinabainisha kwamba, kwa kadri inavyooneka, Mbowe naye anafanya makosa yale yale.
“Nasikia hawasikilizi kabisa akina Zitto, Profesa Mwesiga Baregu, Marando na Dk. Kitila Mkumbo. Yeye anawasikiliza akina Joseph Mbilinyi, Godbless Lema, Tundu Lissu na Peter Msigwa.
“Lakini huwezi kufananisha hawa watu. Akina Baregu wamekuwa kwenye mageuzi kwa miaka zaidi ya 20. Wanaheshimika ndani na nje ya nchi na upeo wao hauna mfano kwenye upinzani.
“Sasa unaachaje kumsikiliza huyu na ukamsikiliza zaidi mtu ambaye hana sifa za kimageuzi katika ngazi ya kitaifa? Wanaozua tuhuma dhidi ya wenzao hawana hata miaka mitano ndani ya chama?
“Labda nikupe mfano mzuri. Hivi unategemea leo, CCM kwa mfano, eti akina Richard Tambwe Hizza, waanzishe mkakati wa kumng’oa kwenye chama mtu kama Kingunge Ngombale Mwiru kwa madai ni msaliti? Haya mambo yako CHADEMA tu,” alisema mwanasiasa huyo ambaye hakutaka kutajwa jina lake kwa maelezo kwamba amefuatwa na baadhi ya viongozi wa CHADEMA ili awasuluhishe kwenye mgogoro huu wa sasa na kujulikana msimamo wake kunaweza kupunguza kuaminiwa kwake na pande hasimu kwenye mgogoro wa sasa.
Mgogoro wa sasa wa CHADEMA unatokana na hatua ya kikao kilichopita cha Kamati Kuu ya CHADEMA kuamua kuwavua nyadhifa zao zote ndani ya chama Zitto, Dk. Kitila na aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho mkoani Arusha, Samson Mwigamba.
Raia Mwema linafahamu kwamba mgawanyiko ndani ya chama hicho ulionekana wazi ndani ya Kamati Kuu ya chama kutokana na hoja zilizotolewa na baadhi ya wajumbe kukinzana; wengine wakimtetea Zitto na wengine wakitaka afukuzwe kwenye chama.
Gazeti hili limearifiwa kwamba kambi ya mashambulizi dhidi ya Zitto iliongozwa na Lissu lakini kwenye mitandao ya kijamii, Msigwa –ambaye ni Mbunge wa Iringa Mjini, amekuwa akiendesha mashambulizi dhidi ya Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali.
Profesa Baregu na Marando ni miongoni mwa waliomtetea Zitto na hoja yao kubwa ilikuwa kwamba kwa vile walikiri makosa yao, kukubali kujiuzulu kwao kulitosha kulimaliza suala hilo badala ya kuliendeleza kwa kuwataka wajieleze kwa maandishi kuhusu makosa yao.
Dalili za mpasuko
Kuanzia wiki iliyopita, yamekuwepo matamko mbalimbali kutoka mikoani na taasisi mbalimbali kuhusiana na hatua ya akina Zitto kuvuliwa nyadhifa zao.
Matukio hayo yanaonyesha kwamba uamuzi huo haujakubaliwa na wanachama wote na ndiyo maana wiki iliyopita, makao makuu ya CHADEMA yalianza kutuma baadhi ya makada wake kwenda mikoani kwa ajili ya kueleza maamuzi hayo ya Kamati Kuu kwa wanachama wake.
Katibu Mkuu wa CHADEMA, alikuwa amepanga kufanya ziara katika mikoa ya Tabora na Kigoma – inayotajwa kuwa ngome kuu ya kisiasa ya Zitto, kuanzia kesho lakini tayari baadhi ya viongozi wa mikoani wameonyesha kutokuwa tayari kuandaa mikutano hiyo.
Katika taarifa yake iliyotolewa kwa vyombo vya habari juzi, Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Kigoma, Jafari Kasisiko, alisema ingawa ziara ya Slaa ina lengo la kujenga chama, mazingira yaliyopo sasa hayatoi fursa ya kufanya hivyo.
Hata hivyo, wana CHADEMA kutoka Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, wametoa taarifa inayoeleza kuunga mkono maamuzi hayo ya Kamati Kuu na taarifa yao ilitolewa na kiongozi wa matawi ya chama hicho, Frank Sumbe.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kwamba maamuzi hayo yanaungwa mkono zaidi katika mikoa ya Kaskazini na Nyanda za Juu lakini kuna upinzani kwenye mikoa ya Kanda ya Kusini na Ziwa Magharibi anakotoka Kabwe.
Jana Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Singida, Wilfred Kitundu, naye alitangaza kujiuzulu wadhifa wake huo akipinga maamuzi hayo ya Kamati Kuu. Pamoja na mambo mengine, Kitundu ndiye mwanachama wa kwanza kujiunga na chama hicho kutokea mkoani Singida.
Hata hivyo, Raia Mwema limeambiwa kwamba baadhi ya wanachama waandamizi wa CHADEMA wameanza kujipanga kutafuta suluhu ya mgogoro wa sasa kwa kutafuta watu wanaoheshimika nje ya chama hicho kwa ajili ya kazi hiyo.
“Wenyewe kwa wenyewe hatuwezi kusuluhishana kwa sasa kwa vile tunajuana. La msingi hapa ni kutafuta watu kutoka nje ya chama ambao wanaheshimika na kila upande. Kukubali CHADEMA ife ni kuwaondolea Watanzania tumaini,”alisema mmoja wa wabunge wa CHADEMA ambaye hakutaka kutajwa jina.
Wakati hali hiyo ya kutokuelewana ndani ya CHADEMA ikiendelea, gazeti hili limeambiwa kwamba wanachama hao watatu waliotakiwa kujieleza, tayari wamekabidhiwa mashitaka yao 11 wanayotakiwa kuyajibu katika kipindi cha siku 14 tangu wakabidhiwe barua zao.











- See more at: Raia Mwema - Mtikisiko CHADEMA: Harakati mpya zaibuka[/QUOTE]
 
Mleta thread kwanza ondoa mawazo ya kijinga kwa kutuaminisha kuwa wasomi ndio wanafaa kuwa viongozi. Mtu yeyote awe amesoma ama hajasoma kwa kiwango unachoamini wewe anaweza kuwa kiranja mzuri au mbovu kupita kiasi. Kiongozi mzuri ni yule mwenye kujiona kuwa yuko pale kwa nguvu za mungu nasio mi degree yake ya UDSM,tunao wasomi wengi huku ambao wamefeli kuongoza si umma hata familia zao nakubaki kuchomekea,kuvaa miwani na kupangilia kalamu kibao kwenye mfuko wa shati lake. Mbaya zaidi huwa wagumu kushauriwa na mtu anayemuona hamfikii elimu. Mimi nayasema haya kwa kuangalia mfn toka kwa wazazi wangu,mama hakuwa na elimu wakati baba alikuwa na elimu ya kutosha sana,siku zote baba hakupokea ushauri kirahsi toka kwa mama hata kwa jambo wazi kabisa japo walikuwa wanapendana sana japo siku zingine mama alikuwa anasononeka sana. Mimi bado naamini ili CCM ifanye kazi kwa uadilifu na kipendwe ni pale patakapokuwepo upinzani wa kweli lakini sio wasomaji malaya kama Zitto, wabunge wendawazimu kama Lema ambao akisimama kuongea ama utoke ulipokaa ama uzime TV/RADIO halafu ndo unaambiwa mpambanaji. Namuunga mkono Mh. Pinda aliposema Zitto yanayompata sasa ni laana ya kutoheshimu waliokuzidi umr.i
 
Lazima wafukuzwe tu,kuhusu magazeti hata mimi nashangaa sana coz hata yale tuliyokuwa tunayaheshimu kwa habari za uhakika sasa yamegeuka kuwa ya udaku. waandishi makanjanja wamejaa na nadhani kuna fungu kubwa sana lilikuwa limeandaliwa kwa kazi hii ya kuwasafisha wasaliti na mamluki wa magamba walioko CDM.Ukisoma hiyo habari utaona kuwa mwandishi anataka kupotosha umma anapoyapa uhalali matamko feki ya wapambe wa wasaliti (ccm) yaliyotolewa mikoani.Natolea mfano tamko la Mwanza lililotolewa na watu waliofukuzwa cdm Gwanchele,Chagulani na Matata.Kwa ukweli huo tu mdogo naona hiyo habari ktk gazeti la raia mwema ni ya kidaku na imeandikwa na mwandishi mdaku au kanjanja mganga njaa tu.
 
Huyu profesa naye si msomi kama Dr. Cdm kuweni makini na watu hawa. Mkijidangaja kurudi nyuma katika maumuzi yenu mmekwisha.

Wasaliti hawa hakika hawatafanya makosa mara ya pili. Chuki watakazo pandikiza kwa mara pili ya kuwaondoa madarakani hazitakiacha chama hiki salama.

Hata waTz wanaotaka mabadiliko hawata waelewa kama mtageuka nyuma na kukubali kuwa nguzo ya chumvi.

Watu hawa hawana uungwana hata chembe, matendo na matamko yao yana thibitisha hivyo. Sasa unafanyaje suluhu na mtu anaye kuhujumu na asiye na uungwana kabisa.

:disapointed:Hapana bro ni vema usuluhishi kuliko kutunishiana misuli. Watakaoumia ni watanzania wapenda demokrasia endapo chadema itagawanyika au hata chama kingine chochote kile. Ukumbuke maelfu ya watanzania waliokipigia chadema kura si hawa tunaoshinda kwenye mitandao tukilumbana. Idadi kubwa hawajuii hata kutumia internet na wamehamasishwa tu na vyama mbalimbali kutetea haki zao. Kuwepo na Chadema moja ni ushindi mkubwa sana kidemokrasia. Kuna uwezekano kabisa ya hilo kuwezekana kwani hadi sasa hali inaruhusu. Madhara yatakayotokea endapo Zitto ataambiwa afungashe manyanga, hata kama ni madogo yasipuuzwe kwani yatawaliza wapenda demokrasia. Huwezi amini kwamba itachukua pengine miaka ishirini na hata na zaidi kupata chama cha upinzani kitakachoaminiwa na watanzania tena. Kama inavyopendekezwa watafutwe watu wa nje wa upande wa Mbowe na upande wa Zitto wawaweke mezani kupata suluhu. Na sala nazo zinahitajika. Nashangaa mpaka dakika hizi viongozi wetu wa dini hawajajitokeza kufanya maombi kwa yanayotokea si ndani ya Chadema tu bali hata kwa vyama vingine ambavyo vinadalili ya vurugu. Nimesikia kuna viongozi wengine badala ya maombi wamedhiriki kushauri msajili akifute Chadema. Suluhu ni jambo jema sana na mfano mzuri ni wa Rais wetu JK aliochukua juzi juzi kwenye tofauti zake na Kagame wa Ruanda na Muungano wa afrika Mashariki. Ungesoma huku kwenye JF wakati huo kuna waliokua wanatoa ushauri wa kutisha na kama si busara za Rais angechukua ushauri wao sijui taifa letu lingekuwa liko wapi leo. Wasiotaka suluhu kweli wajiangalie. Wanaweza wakakiponza Chama hiki. Kuna ushauri uliopendekezwa kwamba Zitto achukue nafasi ya Makamu mwenyekiti iliyoachwa na Mh Arfi. Zitto akubaliane na hilo na ingeondoa adha kubwa sana. Muda ukifika ataipata hiyo nafasi ya Uenyekiti. Binadamu huteleza na binadamu husameheana. Mandela ni mfono bora wa kusameheana. Chadema imuige. Ninaamini baada ya usuluhishi kambi zote mbili yaani ya Mbowe na ile ya Zitto zitajisahihisha kasoro zake ambazo watanzania wengi wamesifahamu sasa na hakuna atakaerudia makosa tena.
 
Limwandishi litakuwa lina utaira au limepitiwa na ZITTO PESA
 
Hakuna cha usomi , ni hao hao wasomi ndio walioligharimu taifa hili, shida ya wafrika wakisoma hata bosi wakohumheshimu ikiwezekana hata wakina Baregu ikithibitika ni miongoni timua. wasomi tuko wengi cdm lakini mbowe tunamheshimu kama mwenyekiti wetu ------- zenu, kama manahisi mmesoma sana zaidi ya viongozi wetu anzishe chama chenu sisi mtuache na cdm yetu then tukutane uwanjani 2015

Kwa hiyo kama hutaki wasomi ina maana unataka CHADEMA iwe ya vihiyo? Kwanini unafikiri uanachama wako ni bora kuliko wa msomi anayekosoa uongozi kiasi kuwa yeye awe ndie wa kuondoka na sio uongozi au wewe?
 
Walianza M1 na M3 kumtetea MM badala ya kujitetea wao wenyewe, hawajijali wako tayari kuondoka lakini Key Player abaki

Sasa gazeti linaloaminiwa na kutofungamana na upande wowote linaleta uswahiba kwa mmoja aliyepururwa kulitumia ili mission iwe accomplished

itatumiwa kila mbinu zzk anayeamiwa kuweza kuvuruga na kugharimikiwa kulikofanywa hadi sasa abaki CDM

RAIA MWEMA kama kweli 'uungwana ni vitendo' kuweni professional... waachieni Jambo Leo,Uhuru na Tanzania Daima mnachokifanya
 
Back
Top Bottom