• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Mtikisiko CHADEMA: Harakati mpya zaibuka

Kakke

Kakke

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2010
Messages
1,882
Points
2,000
Kakke

Kakke

JF-Expert Member
Joined Dec 4, 2010
1,882 2,000
Mwandishi Wetu

Toleo la 328
4 Dec 2013

  • Mkakati wa usuluhishi waandaliwa

JUHUDI za chini kwa chini kusuluhisha kambi zinazokwaruzana katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), chini ya mwavuli wa usaliti zimeanza kuchukua nafasi yake, Raia Mwema, limebaini.
Kambi zinazosuguana kwa sasa chini ya kivuli hicho cha usaliti ni ile inayodaiwa kuwa ya Mwenyekiti, Freeman Mbowe, inayouwanganisha wabunge Tundu Lissu, Peter Msigwa, Godbless Lema, John Mnyika na Katibu Mkuu Dk. Wilbroad Slaa, ambayo inajitambulisha kwa ‘kete’ ya kudhibiti usaliti dhidi ya chama hicho.
Kambi nyingine ni ile ya Kabwe Zitto, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, yenye wasomi wengi inayotajwa kumuandaa Zitto kuwania nafasi ya uenyekiti wa chama hicho kikuu cha upinzani ili kumng’oa mwenyekiti wa sasa Mbowe, kama naye atajitosa kugombea tena wadhifa huo.
Miongoni mwa wasomi wanaotajwa kuwamo katka kambi hiyo ni pamoja na mwanasiasa mkongwe wa mageuzi nchini, Profesa Mwesiga Baregu na msomi mwingine aliyekwishajeruhiwa kisiasa ndani ya chama hicho, Dk. Kitila Mkumbo.
Hata hivyo, pamoja na juhudi hizo za usuluhishi wa kambi hizo mbili zinazoendelea chini kwa chini, kuna uwezekano mkubwa viongozi wa juu wa chama hicho, wakiongozwa na Mbowe, kususia usuluhishi huo na kama itakuwa hivyo, basi katika kipindi cha siku chache zijazo, hatari ya chama hicho kuzidi kupasuka ni kubwa.
Viongozi wakongwe katika masuala ya mageuzi nchini waliozungumza na gazeti hili wiki hii, wamefananisha kinachoendelea sasa ndani ya chama hicho na kilichokitokea chama cha NCCR-Mageuzi mwishoni mwa miaka ya 1990.
Wakati huo, NCCR kilikuwa ndiyo chama kikuu cha upinzani hapa nchini, chini ya uenyekiti wa Augustine Mrema, lakini mgogoro mkubwa uliokikumba ulimlazimu akihame chama hicho na kujiunga chama cha TLP na kuhama kwake kukawa mwisho wake wa kisiasa na mwisho wa nguvu kubwa za chama hicho cha mageuzi.
Mmoja wa wanasiasa wa mashuhuri wa kambi ya upinzani nchini ambaye amejitolea kusuluhisha mgogoro kati ya kambi inayotajwa kuwa ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na ile inayoongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, amesema haoni uwezekano wa CHADEMA kutopasuka endapo hali ya sasa itaendelea.
Kila anachofanya Mbowe kwa sasa kinafanana kabisa na kile alichokuwa akifanya Mrema. Wakati ule, Mrema alikataa kuwasikiliza wanasiasa waliokuwa na mrengo wa kisomi kama vile akina Dk. Sengondo Mvungi (sasa marehemu) na Mabere Marando na akawa anawasikiliza ‘makomandoo’ wa kisiasa.
Kwake, aliona wasomi wananyatia tu nafasi yake. Matokeo yake akawafanya kuwa maadui zake lakini wenzake walimshauri kwa nia njema tu. Taarifa zilizopo zinabainisha kwamba, kwa kadri inavyooneka, Mbowe naye anafanya makosa yale yale.
“Nasikia hawasikilizi kabisa akina Zitto, Profesa Mwesiga Baregu, Marando na Dk. Kitila Mkumbo. Yeye anawasikiliza akina Joseph Mbilinyi, Godbless Lema, Tundu Lissu na Peter Msigwa.
“Lakini huwezi kufananisha hawa watu. Akina Baregu wamekuwa kwenye mageuzi kwa miaka zaidi ya 20. Wanaheshimika ndani na nje ya nchi na upeo wao hauna mfano kwenye upinzani.
“Sasa unaachaje kumsikiliza huyu na ukamsikiliza zaidi mtu ambaye hana sifa za kimageuzi katika ngazi ya kitaifa? Wanaozua tuhuma dhidi ya wenzao hawana hata miaka mitano ndani ya chama?
“Labda nikupe mfano mzuri. Hivi unategemea leo, CCM kwa mfano, eti akina Richard Tambwe Hizza, waanzishe mkakati wa kumng’oa kwenye chama mtu kama Kingunge Ngombale Mwiru kwa madai ni msaliti? Haya mambo yako CHADEMA tu,” alisema mwanasiasa huyo ambaye hakutaka kutajwa jina lake kwa maelezo kwamba amefuatwa na baadhi ya viongozi wa CHADEMA ili awasuluhishe kwenye mgogoro huu wa sasa na kujulikana msimamo wake kunaweza kupunguza kuaminiwa kwake na pande hasimu kwenye mgogoro wa sasa.
Mgogoro wa sasa wa CHADEMA unatokana na hatua ya kikao kilichopita cha Kamati Kuu ya CHADEMA kuamua kuwavua nyadhifa zao zote ndani ya chama Zitto, Dk. Kitila na aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho mkoani Arusha, Samson Mwigamba.
Raia Mwema linafahamu kwamba mgawanyiko ndani ya chama hicho ulionekana wazi ndani ya Kamati Kuu ya chama kutokana na hoja zilizotolewa na baadhi ya wajumbe kukinzana; wengine wakimtetea Zitto na wengine wakitaka afukuzwe kwenye chama.
Gazeti hili limearifiwa kwamba kambi ya mashambulizi dhidi ya Zitto iliongozwa na Lissu lakini kwenye mitandao ya kijamii, Msigwa –ambaye ni Mbunge wa Iringa Mjini, amekuwa akiendesha mashambulizi dhidi ya Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali.
Profesa Baregu na Marando ni miongoni mwa waliomtetea Zitto na hoja yao kubwa ilikuwa kwamba kwa vile walikiri makosa yao, kukubali kujiuzulu kwao kulitosha kulimaliza suala hilo badala ya kuliendeleza kwa kuwataka wajieleze kwa maandishi kuhusu makosa yao.
Dalili za mpasuko
Kuanzia wiki iliyopita, yamekuwepo matamko mbalimbali kutoka mikoani na taasisi mbalimbali kuhusiana na hatua ya akina Zitto kuvuliwa nyadhifa zao.
Matukio hayo yanaonyesha kwamba uamuzi huo haujakubaliwa na wanachama wote na ndiyo maana wiki iliyopita, makao makuu ya CHADEMA yalianza kutuma baadhi ya makada wake kwenda mikoani kwa ajili ya kueleza maamuzi hayo ya Kamati Kuu kwa wanachama wake.
Katibu Mkuu wa CHADEMA, alikuwa amepanga kufanya ziara katika mikoa ya Tabora na Kigoma – inayotajwa kuwa ngome kuu ya kisiasa ya Zitto, kuanzia kesho lakini tayari baadhi ya viongozi wa mikoani wameonyesha kutokuwa tayari kuandaa mikutano hiyo.
Katika taarifa yake iliyotolewa kwa vyombo vya habari juzi, Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Kigoma, Jafari Kasisiko, alisema ingawa ziara ya Slaa ina lengo la kujenga chama, mazingira yaliyopo sasa hayatoi fursa ya kufanya hivyo.
Hata hivyo, wana CHADEMA kutoka Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, wametoa taarifa inayoeleza kuunga mkono maamuzi hayo ya Kamati Kuu na taarifa yao ilitolewa na kiongozi wa matawi ya chama hicho, Frank Sumbe.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kwamba maamuzi hayo yanaungwa mkono zaidi katika mikoa ya Kaskazini na Nyanda za Juu lakini kuna upinzani kwenye mikoa ya Kanda ya Kusini na Ziwa Magharibi anakotoka Kabwe.
Jana Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Singida, Wilfred Kitundu, naye alitangaza kujiuzulu wadhifa wake huo akipinga maamuzi hayo ya Kamati Kuu. Pamoja na mambo mengine, Kitundu ndiye mwanachama wa kwanza kujiunga na chama hicho kutokea mkoani Singida.
Hata hivyo, Raia Mwema limeambiwa kwamba baadhi ya wanachama waandamizi wa CHADEMA wameanza kujipanga kutafuta suluhu ya mgogoro wa sasa kwa kutafuta watu wanaoheshimika nje ya chama hicho kwa ajili ya kazi hiyo.
“Wenyewe kwa wenyewe hatuwezi kusuluhishana kwa sasa kwa vile tunajuana. La msingi hapa ni kutafuta watu kutoka nje ya chama ambao wanaheshimika na kila upande. Kukubali CHADEMA ife ni kuwaondolea Watanzania tumaini,”alisema mmoja wa wabunge wa CHADEMA ambaye hakutaka kutajwa jina.
Wakati hali hiyo ya kutokuelewana ndani ya CHADEMA ikiendelea, gazeti hili limeambiwa kwamba wanachama hao watatu waliotakiwa kujieleza, tayari wamekabidhiwa mashitaka yao 11 wanayotakiwa kuyajibu katika kipindi cha siku 14 tangu wakabidhiwe barua zao.- See more at: Raia Mwema - Mtikisiko CHADEMA: Harakati mpya zaibuka
 
Kakke

Kakke

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2010
Messages
1,882
Points
2,000
Kakke

Kakke

JF-Expert Member
Joined Dec 4, 2010
1,882 2,000
Mtikisiko wa chadema kete kwa ccm, kuna mambo maweli yamejitokea hivi sasa katika chadema,

a).kuna wenyekupenda chama
b). kuna wenye kupenda mtu

Kama wafuasi wa Chadema hawakutafauticha haya basi wataleta mgawanyo katika chadema.
 
M

Mkono

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2010
Messages
568
Points
170
M

Mkono

JF-Expert Member
Joined May 7, 2010
568 170
Maja ya hatua ya kusikitisha na kukatisha tamaa ni kitendo cha kutafuta suruhu na wasaliti.
 
Kubwajinga

Kubwajinga

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2008
Messages
2,190
Points
1,225
Kubwajinga

Kubwajinga

JF-Expert Member
Joined Jan 23, 2008
2,190 1,225
Kila anachofanya Mbowe kwa sasa kinafanana kabisa na kile alichokuwa akifanya Mrema. Wakati ule, Mrema alikataa kuwasikiliza wanasiasa waliokuwa na mrengo wa kisomi kama vile akina Dk. Sengondo Mvungi (sasa marehemu) na Mabere Marando na akawa anawasikiliza ‘makomandoo’ wa kisiasa.
Kwake, aliona wasomi wananyatia tu nafasi yake. Matokeo yake akawafanya kuwa maadui zake lakini wenzake walimshauri kwa nia njema tu. Taarifa zilizopo zinabainisha kwamba, kwa kadri inavyooneka, Mbowe naye anafanya makosa yale yale.
“Nasikia hawasikilizi kabisa akina Zitto, Profesa Mwesiga Baregu, Marando na Dk. Kitila Mkumbo. Yeye anawasikiliza akina Joseph Mbilinyi, Godbless Lema, Tundu Lissu na Peter Msigwa.
“Lakini huwezi kufananisha hawa watu. Akina Baregu wamekuwa kwenye mageuzi kwa miaka zaidi ya 20. Wanaheshimika ndani na nje ya nchi na upeo wao hauna mfano kwenye upinzani.
“Sasa unaachaje kumsikiliza huyu na ukamsikiliza zaidi mtu ambaye hana sifa za kimageuzi katika ngazi ya kitaifa? Wanaozua tuhuma dhidi ya wenzao hawana hata miaka mitano ndani ya chama?
- See more at: Raia Mwema - Mtikisiko CHADEMA: Harakati mpya zaibuka
Raia Mwema wanasema kweli. Mbowe ndiye tatizo ndani ya CHADEMA na sio Zitto. Mtu asiye na shule kama kawaida huwa hajiamini anapokuwa madarakani. Kwa nini Mbowe anavuruga chama ili tu kulinda mapungufu yake binafsi?
 
peche luke

peche luke

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2013
Messages
365
Points
0
peche luke

peche luke

JF-Expert Member
Joined Sep 8, 2013
365 0
Huyu profesa naye si msomi kama Dr. Cdm kuweni makini na watu hawa. Mkijidangaja kurudi nyuma katika maumuzi yenu mmekwisha.

Wasaliti hawa hakika hawatafanya makosa mara ya pili. Chuki watakazo pandikiza kwa mara pili ya kuwaondoa madarakani hazitakiacha chama hiki salama.

Hata waTz wanaotaka mabadiliko hawata waelewa kama mtageuka nyuma na kukubali kuwa nguzo ya chumvi.

Watu hawa hawana uungwana hata chembe, matendo na matamko yao yana thibitisha hivyo. Sasa unafanyaje suluhu na mtu anaye kuhujumu na asiye na uungwana kabisa.
 
T

Thesi

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2010
Messages
1,000
Points
1,195
T

Thesi

JF-Expert Member
Joined Aug 8, 2010
1,000 1,195
Hii nchi waandishi wa habari wamekuwa waandishi bahasha tu. Raia mwema gazeti niliyoiheshimu imekuwa kama gazeti la udaku.
Hadi tunafika 2015 sijui ni magazeti gani yatakuwa na uweledi bila kushikwa breki na bahasha. Eti kambi ya Zitto iliyo na wasomi wengi. Unadhibitishaje hilo kama mwandishi kwa huu uandishi wa darala la saba.
 
WAMASERO

WAMASERO

Member
Joined
Dec 4, 2013
Messages
71
Points
95
WAMASERO

WAMASERO

Member
Joined Dec 4, 2013
71 95
Tuweni makini na mpasuko huu wa makundi mawili haya! 1.) kundi la zitto,
2)kundi la Dr. silaa.
hawa wote ni viongozi wetu ambao tunawategemea kutuongoza wanaCDM jambo la msingi ni kutafuta mbinu za kuwakutanisha wote hawa ili tutafute suluhu kabla ya uchaguzi mwakani tukiwa pamoja kushinda ni halali
 
KirilOriginal

KirilOriginal

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2012
Messages
2,086
Points
2,000
KirilOriginal

KirilOriginal

JF-Expert Member
Joined Feb 13, 2012
2,086 2,000
"The worst pain in the world goes beyond the physical. Even further beyond any other emotional painone can feel. It is the betrayal of afriend."
Ni rahisi kumsamehe adui ni vigumu kumsameherafiki anapokusaliti.


 
Simiyu Yetu

Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2013
Messages
18,941
Points
2,000
Simiyu Yetu

Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2013
18,941 2,000
Hii sacos inakufa kifo kibaya sana bila zitto kuombwa msamaha marehemu chadema lazima tumzike na kumsahau kabisa.
 
Mkwawa

Mkwawa

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2011
Messages
1,336
Points
1,500
Mkwawa

Mkwawa

JF-Expert Member
Joined Jun 8, 2011
1,336 1,500
Hakuna Mgogoro Chadema, na Chadema sio NCCR wala TLP-Katiba itafuatwa hakuna wa kusuluhisha, kama kuna mtu anaona kaonewa afuate katiba na kanuni za chama. Nitashangaa sana Kuona viongozi wangu wakivunja katiba walioapa kuisimamia.

Wamepewa siku za kujitetea, haki imefwata, walikuwepo kwenye kikao cha maamuzi na walikiri dhambi zao. Hakuna aliyeonewa hizi sarakasi za kisiasa za wachumia matumbo haziwezi kufifisha haki.

Mwandishi na mhariri wa hili gazeti wote vilaza, kwanini hawakuwahoji hao waliowataja ili ku-balance story- naona na hili gazeti linaanza uandishi jalala kweli njaa hana nyumba.

Naomba mapindikizi yote popote yalipo yajue huu ni mwaka 2013 sio 1990. Kizazi hiki cha leo hakijapata huruma yoyote ya serikali, shule tunalipa, dawa tunanunua, maziwa tunanunua. Najua kizazi cha wengi waliosaliti mageuzi ni wale walioaminishwa maisha yao ni kwa huruma ya watawala. Hapa ngoma hailali, tupo tayari kumwajibisha yeyote.
 
Simiyu Yetu

Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2013
Messages
18,941
Points
2,000
Simiyu Yetu

Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2013
18,941 2,000
Nasema na nitaendelea kusema kuwa hakuna mtu wa kumfukuza zitto.
 
K

Kichakoro

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2008
Messages
2,196
Points
2,000
K

Kichakoro

JF-Expert Member
Joined Sep 10, 2008
2,196 2,000
Kakke,
Hii habari ina walakini mwingi sana. Kwanza msuluhishi hata hajafanya usuluhishi alioombwa ameanza kukutana na media, je akianza kazi si ndio atakua anaitisha press kila baada ya saa moja?

Pili hii habari inasema kuna watu wanaoitwa wasomi (prof Baregu na Dr. Kitila). Hivi hawa ndio wasomi pekee waliopo CDM? How about prof Safari na wengine je sio wasomi?

Kwenye hii habari inasema watu 5 ndio wamekua wanampinga zitto wengine walikua wanamtetea, je kamati kuu ilikua na wajumbe wangapi wakati wa kikao? Je hii agenda haikupigiwa kura kufikia muafaka je kati ya wajumbe 32 wangapi waliikubali hoja kama ni zaidi ya nusu iweje waseme Mbowe, slaa, mnyika, Lisu na lemma ndio wanaompinga?

Kama maamuzi yalifanywa na chombo cha taasis iweje tena issue watu 5 ndio wanaolaumiwa?

Kwa nini mwandishi hajaonesha nia ya kuzungumza na viongozi kupata ukweli kama huyo msuluhishi kweli amefuatwa na uongozi wa CDM kubalamce story?

Mwisho huu uandishi wa kikanjanja una shida. Nimekua nikitamani kupata habari za kina na za ukweli kutoka kwenye magazeti huru lakini wote naona wanaganga njaa. Ni lini media zetu mtakua neutral na kukosoa ukweli?
 
Z

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2008
Messages
13,586
Points
2,000
Z

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
Joined May 11, 2008
13,586 2,000
Dah, kama Sugu na Lema ndio washauri wa Mbowe basi hakuna muujiza unaokiua Chadema...
 

Forum statistics

Threads 1,403,487
Members 531,219
Posts 34,424,677
Top