Mtikisiko CHADEMA: Harakati mpya zaibuka

Mtikisiko CHADEMA: Harakati mpya zaibuka

Raia Mwema wanasema kweli. Mbowe ndiye tatizo ndani ya CHADEMA na sio Zitto. Mtu asiye na shule kama kawaida huwa hajiamini anapokuwa madarakani. Kwa nini Mbowe anavuruga chama ili tu kulinda mapungufu yake binafsi?
Hakuna cha usomi , ni hao hao wasomi ndio walioligharimu taifa hili, shida ya wafrika wakisoma hata bosi wakohumheshimu ikiwezekana hata wakina Baregu ikithibitika ni miongoni timua. wasomi tuko wengi cdm lakini mbowe tunamheshimu kama mwenyekiti wetu ------- zenu, kama manahisi mmesoma sana zaidi ya viongozi wetu anzishe chama chenu sisi mtuache na cdm yetu then tukutane uwanjani 2015
 
Hii nchi waandishi wa habari wamekuwa waandishi bahasha tu. Raia mwema gazeti niliyoiheshimu imekuwa kama gazeti la udaku.
Hadi tunafika 2015 sijui ni magazeti gani yatakuwa na uweledi bila kushikwa breki na bahasha. Eti kambi ya Zitto iliyo na wasomi wengi. Unadhibitishaje hilo kama mwandishi kwa huu uandishi wa darala la saba.

litabaki gazeti la Tanzania Daima peke yake
 
Watz tuungane kumwondoa huyu mkoloni mweusi
Sisi ndo tunaochoshwa na sio hao maccm mafisadi
Hawa mafisadi wanaendesha nchi kibabe leo hii wanatangaza hadharani eti kama huna uwezo wa kulipa umeme
Kaa gizani hawa ndo viongozi tulio nao
Maumivu na shida tulizo nazo watz alafu mtu leo anakuambia maneno kama haya
 
"Kamati Kuu ilitaka niwatonye ili warekebishe mahesabu kabla sijamhimiza CAG kukagua hesabu za vyama" - Zitto...
 
“Nasikia hawasikilizi kabisa akina Zitto, Profesa Mwesiga Baregu, Marando na Dk. Kitila Mkumbo.
- See more at: Raia Mwema - Mtikisiko CHADEMA: Harakati mpya zaibuka

Kwa hiyo mwandishi anataka kutuambia kuwa Hawa ndio Masalia na Mabadiliko 2013??? Sitaki kuamini kama hawa wazee nao wameshiriki upuuzi ule. Vile vile mwandishi amesahau kuwa CDM ina wasomi wengi, na si kila msomi ana mawazo ya kujenga au busara Mfano ZZK, Dr Kitila. Na kwa manufaa ya wengi hakuna ushauri mzuri wa mtu aliyeshindwa kulinda nyumba yake mwenyewe. CDM chini ya kamanda wa Anga iko makini kinoma. Mnamuogopa Mbowe kwasababu hakuna dau la kumnunua kawapiga za kichwa wote.

CDM ingekuwa na Mwenyekiti masikini kwa mashambulizi ya CCM na kikundi cha masalia sidhani kama ingepona. Ila Ngome iko imara. Na nitashauri mpaka twende ikulu lazima mgombea wa uenyekiti awe na akaunti inayoelweka asiwe na shida za kulipia watoto ada wala, historia inaonyesha ukiwa na njaa huna tabia, unaweza uza utu. Mwenye njaa hata awe na elimu vipi anakuwa mjinga kwasababu ya njaa yake. Ndio maana makampuni makini na kazi muhimu duniani lazima ulipwe vyema kukutoa vishawishi.

Gazeti la Raimwema nalo naona linapata soko kama walivyoweza kununuliwa na Rostam enzi za RAI nguvu ya hoja.
 
Hii nchi waandishi wa habari wamekuwa waandishi bahasha tu. Raia mwema gazeti niliyoiheshimu imekuwa kama gazeti la udaku.
Hadi tunafika 2015 sijui ni magazeti gani yatakuwa na uweledi bila kushikwa breki na bahasha. Eti kambi ya Zitto iliyo na wasomi wengi. Unadhibitishaje hilo kama mwandishi kwa huu uandishi wa darala la saba.

wanashabikia ujinga ili wauze magezeti hawajui wanajirudisha nyuma wao,kiko wapi sasa cha kutetea wasaliti au wanaogopa kuwa kama mh.A.KIBADA.
 
hakuna namna yoyote kwa cdm kubaki na wasaliti , ni lazima watimuliwe .
 
hivi chama ambacho wananchi wote wanakitegemea eti kimuogope zitto kabwe ! Hakuna suluhu na mamluki ! Poor Raia Mwema !
 
hili gazeti lilikuwa kwenye bookmarks yangu kwa habari hii nimelifuta.
 
"Kamati Kuu ilitaka niwatonye ili warekebishe mahesabu kabla sijamhimiza CAG kukagua hesabu za vyama" - Zitto...

Zitto a.k.a tarishi wa ccm kwisha kazi ! Chali miguu juu ! Migebuka imegeuka vibua , unacheza na nguvu ya umma ! Watu wanapasua mwandiga yeye anapokea maagizo ya lumumba , yaani naye ni buku 7 fc !
 
Wakati wa Mussa aliwaambia wana wa Israel Wanaotaka kumuamini Mungu na sheria zake wakae upande huu na wasiotaka wakae kule... Mgawanyiko ukawa na waliokataa walindei na waliokubali wakaendelea na Safari.... CDM jisafisheni mapema Mtabarikiwa Mwenyezi Mungu analo Jambo analotuandalia hii nchi yetu ni Tajiri... Pengine nanyi huko wengine hawafai kuwepo ndani ya Raha 2015 mkiondosha hawa Wanyonyaji wenye mizizi mikuu
 
....Profesa Baregu na Marando ni miongoni mwa waliomtetea Zitto na hoja yao kubwa ilikuwa kwamba kwa vile walikiri makosa yao, kukubali kujiuzulu kwao kulitosha kulimaliza suala hilo badala ya kuliendeleza kwa kuwataka wajieleze kwa maandishi kuhusu makosa yao.
Dalili za mpasuko
Kuanzia wiki iliyopita, yamekuwepo matamko mbalimbali kutoka mikoani na taasisi mbalimbali kuhusiana na hatua ya akina Zitto kuvuliwa nyadhifa zao.
Matukio hayo yanaonyesha kwamba uamuzi huo haujakubaliwa na wanachama wote na ndiyo maana wiki iliyopita, makao makuu ya CHADEMA yalianza kutuma baadhi ya makada wake kwenda mikoani kwa ajili ya kueleza maamuzi hayo ya Kamati Kuu kwa wanachama wake.
Katibu Mkuu wa CHADEMA, alikuwa amepanga kufanya ziara katika mikoa ya Tabora na Kigoma – inayotajwa kuwa ngome kuu ya kisiasa ya Zitto, kuanzia kesho lakini tayari baadhi ya viongozi wa mikoani wameonyesha kutokuwa tayari kuandaa mikutano hiyo.
Katika taarifa yake iliyotolewa kwa vyombo vya habari juzi, Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Kigoma, Jafari Kasisiko, alisema ingawa ziara ya Slaa ina lengo la kujenga chama, mazingira yaliyopo sasa hayatoi fursa ya kufanya hivyo.
Hata hivyo, wana CHADEMA kutoka Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, wametoa taarifa inayoeleza kuunga mkono maamuzi hayo ya Kamati Kuu na taarifa yao ilitolewa na kiongozi wa matawi ya chama hicho, Frank Sumbe.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kwamba maamuzi hayo yanaungwa mkono zaidi katika mikoa ya Kaskazini na Nyanda za Juu lakini kuna upinzani kwenye mikoa ya Kanda ya Kusini na Ziwa Magharibi anakotoka Kabwe.
Jana Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Singida, Wilfred Kitundu, naye alitangaza kujiuzulu wadhifa wake huo akipinga maamuzi hayo ya Kamati Kuu. Pamoja na mambo mengine, Kitundu ndiye mwanachama wa kwanza kujiunga na chama hicho kutokea mkoani Singida.

...Hivi Baregu na Marando wanaamini hawa wasaliti walikiri makosa yao? Mbona katika ule mkutano ulioandaliwa na akina Mwampamba na Mchange hawakuonyesha kukiri makosa? wanaliongeleaje hilo?

CHADEMA itafanya kosa kubwa kudhani usomi wa akina Baregu ndio kigezo cha busara. Gharama ya kuishi na wasaliti ndani ya chama ni kubwa kuliko kuwatimua. waende tu na umaarufu wao kama wanao. Maana hata hao magamba wanaowashabikia hawawataki ndo maana wanashabikia sana wabakishwe CHADEMA.
 
Leo ndiyo nimejua kwanini CDM inayumba! Kumbe washauri wa mwenyekiti ni mwanamuziki na mwizi wa magari? Hapo uamuzi wa busara hakuna, tujiandae kwa msiba tu.

Body without head
 
Gazeti la Zitto unategemea nini? Eti wasomi? Wakati wanajiunga na Chadema hawakujua kuwa Mwenyekiti sio msomi? Kwanini wasijiunge CCM kwa Dr.Dr.Dr.Dr Kikwete?
 
Ni kipindi kirefu sasa tumeendelea kusomaPropaganda za kijinga za CCM mpaka imefikia muda sasa zimetushosha, labdaniwaambie kwa kifupi kuwa “WAKATI NI UKUTA” na “KILA KITU KINA WAKATI WAKE”,hatukatai kwamba toka serikali yetu iliyo chini ya CCM imeruhusu kwa shingoupande mfumo wa vyama vyingi vya siasa vimekuwepo vyama mbalimbali vyaupinzani, hatukatai kwamba kwa taarifa za ndani CCM imefanikiwa kuvivunja nguvuvyama hivyo vya upinzani na ikaendelea kuwadangaya Watanzania kwamba ni CCMpekee ndio yenye dhamana ya kuongoza Taifa la Tanzania na ni CCM pekee ndio itakayowezakuwaletea Watanzania maisha bora huku ikiwa imeshapita miaka zaidi ya 50 tokatupate uhuru, hivi kweli hamuwezi kuona aibu kwamba mmshindwa kuongoza vyemanchi ya Tanzania wakati imejaliwa rasilimali lukuki kuliko hata nchi za duniaya kwanza?

Labda kwa ushauri wa bure tu ni kwamba,propaganda na siasa za kijinga ambazo CCM wamezoea kuzifanya miaka ya nyuma zimefikiakikomo chake, sasa hivi teknolojia imekuwa na kupanuka kwa kiwango kikubwa namaeneo mengi wananchi wanajitahidi kujipatia elimu ya kuwatoa gizani japo sikatika kiwango kinachorodhisha, sasabadala ya kufanya ujinga ujinga na propaganda za kijinga wangejikita kwenyekutekeleza sera za chama chao pamoja na ilani yao ya uchaguzi, kuendeleza nchina wananchi wake, kulinda heshima ya nchi na rasilimali zake na kuhakikisharasilimali hizo zinamnufaisha Mtanzania, kujenga umoja wa Taifa n.k.


Inapotokea kwamba mambo marahisi namna hiyo yanawashindakuyatekeleeza na kubakia kupoteza muda kupambana na upinzani ndipo tunapotiliashaka uwezo wao wa kufikiri.


Kwa taarifa yenu ni kwamba CHADEMA HAIWEZIKUFA, na msikae hata siku moja mkafikiria kwamba CHADEMA ni chama ambachomtaweza kukimaliza kwa propaganda zenu za kijinga kama mlivyozoea.

CHADEMA ndio kila kitu kwa Watanzania, CHADEMA ndiyoinayobeba MATUMAINI ya maisha ya WATANZANIA wanyonge, CHADEMA ndiyoinayowasilisha SAUTI ya UKOMBOZI wa WATANZANIA.

Hatukatai kwamba njama zenu za kuua elimu kwawananchi wa kawaida imewasaidia kupata kundi la Watanzania wasioweza kuhojimambo muhimu ya nchi yao, pia njama zenu za kuendeleza UMASKINI wa Watanzaniazimewafanya Watanzania wasijiamini na kuwa wategemezi siku zote, lakini hivyoni vitu vya muda mfupi tu. Mwisho wenu uko karibu.


Kwa taarifa yenu ni kwamba mwaka 2020 ndiomwisho wa CCM, CCM hakitakuwa chama cha upinzani tu bali KITAKUFA. MUNGU ALIYEJUU NA ASHUHUDIE MANENO HAYA.
 
Back
Top Bottom