Mtihani wa taifa wa somo la mahusiano mwaka 2025

Mtihani wa taifa wa somo la mahusiano mwaka 2025

Mr George Francis

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2022
Posts
274
Reaction score
486
MTIHANI WA TAIFA WASOMO LA MAHUSIANO MWAKA 2025.

JIBU MASWALI YOTE.
Kulia inaruhusiwa kwenye chumba cha mtihani. 😂

1. Umekuwa kwenye mahusiano na mtu kwa miaka (5) mitano lakini ghafla amekuacha na ameenda kuoana na mtu mwingine. Piga hesabu ya muda uliopoteza. (Maksi 15)

2. Umenunua zawadi umempa mpenzi wako naye mpenzi wako amechukua zawadi hiyo na kumpa mpenzi wake. Tumia trigonometric kuelezea haina hii ya upendo. (Maksi 15)

3. Mwanaume unadate na wanawake (7) saba na kila mwanamke anahitaji huduma yako ya kifedha na vitu mbalimbali.
(a). Toa maelezo kwa kutumia namba za kirumi jumla ya kiwango cha pesa utakachotumia kwa mwezi. (Maksi 10)
(b). Toa maelezo kwa maneno ya hisia kuonesha namna utakavyokuwa masikini maisha yako yote. (Maksi 10)

4. Umeachana na mpenzi wako alafu bado unaumia ukiona ana mpenzi mwingine na wanafurahia mahusiano yao. Hesabu asilimia za kiwango cha ujinga uliokujaa kichwani. (Maksi 15)

5. Wewe ni mzazi, kipato chako na mke au mumeo kwa mwezi hakizidi laki (5) tano alafu mtoto wenu wa kike mwanafunzi na hana kazi yoyote anamiliki iPhone 16 pro au simu yoyote ya gharama thamani yake ni zaidi ya milioni moja.
Tumia logarithms kuelezea kiwango cha uzembe na upumbavu katika malezi yenu kama wazazi au walezi. (Maksi 15)

6. Baba unashindwa kutoa huduma nzuri kwa mke na watoto wako lakini unatoa huduma bora kwa michepuko na watoto wao waliozaa na wanaume wengine. Elezea kiwango cha ufala ukionao. Tumia Diameter Formula Area = π(Radius)2 ( Maksi 15)

7. Una mpenzi lakini hujali hisia zake wala humpi muda wa kuenjoy na wewe ili uonekane una msimamo. Tathimini namna atakavyokusaliti au kukuacha akimpata mtu anayejali hisia zake. ( Maksi 5)

MTIHANI MWEMA___

Mtihani by Mr George Francis

#No_Learning_No_Earning
So We Have To Learn.
 
Dogo mwenye simu anajua kuwa unaichezea?
 
Nilivyo popoma nimesoma mpaka mwisho, ila najua kuna popoma mwingine atasoma nayeye mpaka mwisho. Kiufupi ndio maana dia mondi anatuona mapopoma square.
 
Back
Top Bottom