Kenya 2022 Mtihani wa kuwapata wagombea-wenza sahihi wa kiti cha urais Kenya

Kenya 2022 General Election

Ikaria

Member
Jul 17, 2019
72
195
Mtihani mkubwa ulioko mbele ya Wagombea wa kiti cha Urais #Kenya (Odinga na Ruto) ni chaguo la Mgombea-mwenza.

Chaguo lao wote wawili huenda likabadilisha mchakato mzima wa siasa na kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu Agosti 9.

Ni suala la kusubiri tu.

20220303_170355.jpg
 
Ndio maana nawashangaa sana wakenya wenzangu, ambao tayari wameshatoa mashati kabisa. Wakiashiria wazi kwamba watafunga mabao upande wa pili, yaani kwenye goli la waliovalia mashati. 😄

Naamini kwamba chaguo la mgombea-mwenza, kutoka kwa wagombea urais wote, ni jambo ambalo linafaa kutazamwa kwa umakini mkubwa. Watu hawajajifunza, kutoka kwa mengi tuliyoyaona kwenye utawala huu wa rais UK. Ugomvi, malumbano, maigizo, 'makasiriko', yote tumeyashuhudia, kati ya rais na naibu wake.

Katiba ya Kenya 2010 ilituletea NAIBU rais, umakamu, ukimya na unyenyekevu wa ovyo ukaishia hapo. Sasa hivi kiti hicho kina hadhi, ushawishi, mamlaka sawa na ya 'co-president'. Tunangoja, ni wazi kwamba atakayeteleza kwenye hili ndoto yake ya kuwa rais itapata pigo kubwa kupindukia. Tena punde tu atakapomtangaza rasmi mgombea-mwenza wake.
 
Back
Top Bottom