Mtihani wa geography wafutwa!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtihani wa geography wafutwa!!

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Mzee wa Gumzo, Oct 9, 2008.

 1. Mzee wa Gumzo

  Mzee wa Gumzo Senior Member

  #1
  Oct 9, 2008
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 197
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Taarifa za kuaminika zinaeleza kuwa mtihani ulioripotiwa kuzagaa mitaani tangu jana ulikuwa ni a Geography.

  Taarifa nyingine zinadai kuwa mtihani huo umefutwa na utapangiwa tarehe nyingine.

  Hii ndiyo Tanzania bora
   
 2. f

  fnguma New Member

  #2
  Oct 9, 2008
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli kwa hali hii Watanzania Tutafika? Wahusika wenyewe waseme ni kwa nini wasichukuliwe hatua kali ikiwa ni pamoja na kujiudhulu nyazifa zao. Hapa ni swala zima la uwajibikaji.
   
 3. BantuGirl

  BantuGirl Senior Member

  #3
  Oct 9, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 157
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kusema kweli karibu kila mtihani ulionekana kabla.....Sijui tutafika na kizazi chetu cha wasomi.
   
 4. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #4
  Oct 9, 2008
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mie nafikiri kwa sasa wasione aibu,waseme tu kwamba mitihani yote imevuja,kwani dalili zote zinaonesha hivyo.
   
 5. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #5
  Oct 9, 2008
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,453
  Likes Received: 7,219
  Trophy Points: 280
  MHuuu sasa hii ndo nini?si wafute mitihani yote kama walivyofanya 1998!maana najua hata ilikwisha kufanyika nayo ilivuja!
   
 6. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #6
  Oct 9, 2008
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Sio kuifuta tuu first lady,na wao wakae pembeni kwa sababu wameshindwa kazi.Maana hii imepita hata open examination.
   
 7. BantuGirl

  BantuGirl Senior Member

  #7
  Oct 9, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 157
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Labda wapangue safu nzima, Unajua kuna wanafunzi wanasoma shule moja hapa dar wanasema wametozwa 200,000 kila mmoja ili kupata hayo mapaper.... Hivi wapi tunaenda na elimu yetu.. Yani miaka hii hatuna wanafunzi bora bali tuna bora wanafunzi..... na kuibuka kwa shule nyingi sasa kunachangia uvujaji wa mitihani maana wamiliki wanataka wateja hivyo wanaamua kufanya hivyo ili kujitengenezea jina.
   
 8. Maverick

  Maverick JF-Expert Member

  #8
  Oct 9, 2008
  Joined: May 29, 2008
  Messages: 308
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mmmh! Wizi huu wa mitihani unachangia kujenga taifa la mazezeta. Ukiangalia kwa makini tatizo hili halikuanzia miaka ya karibuni, ndio maana tunao mazezeta wenye digrii fake kama viongozi wetu.
  Tunaye Profesa kama waziri wa elimu na mama mwenye PhD kama mkurugenz wa NECTA. Kati yao hakuna anayeshtuka, hali inayonipa wasi wasi kuhusu uwezo na elimu zao. Sitashangaa kama nao si mazezeta.
   
 9. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #9
  Oct 9, 2008
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,315
  Likes Received: 5,609
  Trophy Points: 280
  Wafute kama 2001.....wajipange upya..wasione aibu ni mipango yao...mibovu
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  Oct 9, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Mimi nashangaa sana siku hizi wanafunzi wanavyo faulu duh balaa one two ni za kumwaga.Lakini kila mwaka iwa inareportiwa paper limevujaa lakini wahusika iwa wanakanusha na sisi mapaper tunashuhudia na watu wana solve.
  Hili la mwaka huu ndo balaa limezagaa kila kona na limeshuka bei balaa lilianza kuuzwa kwa 700,000/= lile la number saizi nasikia paper zingine zimeshuka bei sana....
  Wenye stationary wana shuhudia wanafunzi wana miminika kutoa copy paper hizo jamani wamehindwa kazi hawa NECTA wafute paper zote wasijivunge vunge.
   
 11. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #11
  Oct 9, 2008
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,603
  Likes Received: 6,770
  Trophy Points: 280
  This is a political scadal nashangaa Mod haipeleki hii thread kwenye ukumbi husika
   
 12. W

  WildCard JF-Expert Member

  #12
  Oct 9, 2008
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Serikali ina mchango MZITO katika hili; kwanza imeweka kigezo kwamba wanaokopesheka ni lazima wapate div 2 au 1; imeacha suala la ELIMU liwe ni biashara HURIA, kwa hiyo kila mwenye kauwezo ka kujenga darasa ameanzisha shule na tabia ya biashara ni ushindani halali au haramu! Halafu ni RUSHWA, UFISADI na UBADHIRIFU kila kona.
   
 13. Mushobozi

  Mushobozi JF-Expert Member

  #13
  Oct 9, 2008
  Joined: Aug 20, 2007
  Messages: 543
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  mwenye papers aziscann na atuwekee hapa, ili iwe aibu kwa mitihani inayotarajiwa kufanyika. pia magazeti wenye nayo wafanye vilevile. waandishi kuweni mstari wa mbele kuokoa kiwango cha elimu tafadhari.
   
 14. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #14
  Oct 9, 2008
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,281
  Likes Received: 4,286
  Trophy Points: 280
  Hii wizara mawaziri wake wote wanakuwa mabwege,then UProf. sio kigezo
  Prof Kapuya, Prof Msola, Prof Maghembe but hamna wanalofanya mi nafikiri hii wizara wangempa Mwanajeshi
   
 15. Himawari

  Himawari JF-Expert Member

  #15
  Oct 9, 2008
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 2,189
  Likes Received: 682
  Trophy Points: 280
  Mhhh kizazi cha mafisadi kwa kupenda njia za mkato..!
   
 16. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #16
  Oct 9, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Huko baraza la mitihani hamna kitengo maalumu knichomonitor utolewaji wa mitihani?Swali lingine la kuuliza jee ni baraza ama mashule yenye headmaster wasroho wa fedha?
   
 17. P

  Paullih Member

  #17
  Oct 9, 2008
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 85
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkurugenzi wa NECTA na Waziri wa Elimu wajiuzuru. Ni aibu na kashfa kwa Taifa!!
   
 18. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #18
  Oct 9, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Wakubwa ni kwamba pepa zinavuja kuanzia shule ya msingi hadi vyuo vikuu, na hii kitu haijaanza leo. Kilichobadilika ni teknolojia ya habari tu, kwa hiyo hata wasio kwenye mtihani wanapata habari. Zamani hizi habari ziliishia huko mashuleni, na wale ambao hawajafanya mtihani walitunza siri ili hiyo "channel" ya pepa iendelee kudumu zamu yao ya kufanya mtihani ikifika nao waitumie. Mitihani ya kuvuja ilikuwa na majina mengi kama "nondo", "kirungu", kule chuo kikuu mlimani waliita "desa", Muhimbili waliita "mwezi" nk.

  Wavujishaji wakuu wa mitihani wako katika makundi kadhaa:
  1. Wafanyakazi wasio waaminifu wanaotaka kujipatia fedha kwa kuuza mitihani. Hawa wako katika sections mbalimbali katika process ile ya kuandaa mitihani kuanzia uchapaji, kurudufu, kufungasha, kusafirisha nk. Na hawa ni ngazi zote, shule ya msingi hadi university. Uzuri ni kwamba hawa ni rahisi kuwadhibiti kwa kuziba mianya yote na kuweka kanuni za usalama zinazozingatiwa na zinazoji-monitor zenyewe.
  2. Kundi la pili ni la wamiliki wa mashule na wakuu wa mashule wanaotaka kujenga sifa kuwa shule zao ni bora. Hawa hununua mitihani kwa gharama yoyote na kuifundisha mashuleni, na wala huwa hawaoni aibu kuwaambia wazazi waongeze michango ya "special tuition" kwa ajili ya watoto wenye mitihani (form 2, 4, 6). Kinachowawezesha hawa kufanikisha hii ni kupenyeza vigogo wa baraza la mitihani kwenye payroll za shule zao, kwa hiyo hizi paper zinatoka kwa wakuu wa Baraza la Mitihani, wale wenye dhamana ya mwisho kabisa ya kuaminiwa (actually wale wanaodhibiti wizi wa mitihani ndio wanaopelekea hawa jamaa hizo pepa). Mitihani ya namna hii inapovuja si rahisi kuonekana mizimamizima maana wahusika huwa wanakabidhi maswali kwa waalimu wa masomo, ambao wanayafundisha darasani kama "revision" za kawaida, kwa hiyo si rahisi kuwastukia. Tatizo linatokea wanapomkabidhi mwalimu paper nzima na yeye ana tamaa ya pesa, anauuza kwa dalali (au madalali) ambao wanaanza kuutembeza kama njugu, hapo ndio "soo" linabumburuka!
  3. Kundi la tatu ni wazazi wenye influence huko baraza la mitihani ambao wanaiba mitihani hiyo kwa ajili ya watoto wao. Hawa pia ni vigogo, na huipata kutoka kwa vigogo wa baraza. Anapofikisha mtihani nyumbani anamkabidhi mwanae anamwambia "ushindwe mwenyewe sasa!" Ikitokea mtoto hajiamini, anatafuta rafiki (au marafiki) anaoamini ni "kipanga" katika kila somo ili wamfundishe (siri imeanza kutoka hapo). Wakimaliza kufundishana, wanakumbuka "unajua tunaweza kutengeneza hela hapa?" Wanaanza biashara kuuzia wenzao.

  Udhibiti wa mitihani unatakiwa uanze kwanza na vigogo wa baraza la mitihani, maana hawa wengine wa chini wanaumiza vichwa kulinda mitihani ambayo ilishavuja kabla hawajakabidhiwa!

  (BTW hii ndio ilikuwa proposal yangu ya awali kwa ajili ya tasnifu yangu ya masomo ya uzamivu, lakini kutokana na "siasa" zilizomo ndani yake niliiacha maana uwezekano wa kuifanikisha ulikuwa mdogo sana. Changamoto kwa anayeipenda aichukue, awe jasiri!)
   
 19. K

  Kipanga JF-Expert Member

  #19
  Oct 9, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 679
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Na muungwana JK anasubiri nini kuwatimua hawa akina Maghembe na Ndalichako wamekuwa na vichwa vigumu hawataki kukubali ukweli wakati uharo ndio umetapakaa hadharani hapo sio suala la harufu tu ni kwamba na kinyesi kimeonekana wao bado wanakalia viti vyao kwa nini?

  Na huyu mama Katibu mkuu Ndalichako ni msanii sana alitangaza hadharani kuwa kuna wanachuo 816 wa chuo cha ualimu Kange kule Tanga kuwa matokeo yao ya mitihani yamefutwa kwa madai kuwa watahiniwa hawakuwa na sifa. Jana afisa tawala wa hicho chuo amenukuliwa TBC taifa akisema kuwa huyo mama ni muongo kwani orodha ya watahiniwa ilipelekwa NECTA kabla ya mitihani ili kuchunguza uhalali wao na kati yao 807 waliruhusiwa kufanya mitihani ikiwemo kupatiwa namba na NECTA kasoro watu 9 tu. Leo bila aibu anatamka hadharani kuwa wamefutiwa mitihani. Uongozi wa kile chuo wanafanya taratibu za kisheria dhidi ya huyo mama....
   
 20. Mzee wa Gumzo

  Mzee wa Gumzo Senior Member

  #20
  Oct 9, 2008
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 197
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Nakuunga mkono Mushobozi
   
Loading...