Mtifuano Mkutano wa CCM - Dodoma

Mtifuano Mkutano wa CCM - Dodoma

Nyerere alisema wapinzani wa CCM watatoka CCM humohumo.

nyerere hakuwa nabii,mimi ni mpinzani wa ccm na sipo ccm wala chama chochote,unadhan hao walotoa vipeperush ni wapinzan wa ccm ndani ya ccm,hao ni zao la makundi ndani ya ccm,hakuna mpinzan hapo,wanafata upepo wa pesa tu,hata jk alipotaka kuchukua madaraka pesa zilimwagwa sana dodoma,
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Sichangii hoja kufurahisha watu au kutafuta kuungwa mkono na watu, bali nachangia hoja kutokana na mawazo yangu huru, hasa nikisimamia kitu ninachoamini, sasa kama inaonekana ni hoja dhaifu, hilo linajadilika lakini kwa hoja mbadala; natarajia urudi na hoja mbadala juu ya suluhisho kwa suala lililo mbele yetu badala ya kutoa hoja za kulaumu mawazo yangu au kuyashangaa; Vinginevyo mgongano wa mawazo ni sehemu muhimu ya mijadala kama hii;

Nadhani unapenda kuliangalia suala hili kwa wepesi; Ni vizuri ukafahamu kwamba suala hili sio dogo kama unavyopenda kufikiri; Linahitaji busara kuliko jazba; Jaribu kutulia na ufanye a cost-benefit analysis kwa kuweka in the centre the fact kwamba huyu ni Rais wa nchi, sio Rais wa CCM au Chama Cha Soka;

Naendelea kusisitiza kwamba - iwapo wajumbe wa kikao husika watafikia ‘a consensus' kwamba Mwenyekiti wa CCM Taifa, J.K Kikwete ni Dhaifu na ni mzigo kwa Chama, basi kwa kuanzia, watazame kwanini walifikia huko, na iwe ni fundisho kwao kwamba next time wanapochagua mgombea Urais kupitia chama chao, wawe makini zaidi kuchagua mtu ambae atakuwa ni kiongozi bora na sio bora kiongozi; Hakuna mwenyekiti wa chama ambae atapendwa na watu wote katika nyakazi hizi; Kiongozi kuwa dhaifu au kutokuwa dhaifu inatokana na kuungwa au kutoungwa mkono na wenzako, nothing less, nothing more;

Vinginevyo kuanza kuvuruga mambo sasahivi kama unavyoashiria kushauri, just because of mistake iliyofanywa huko nyuma ya kuweka mtu ambae anamaliza muda wake within three years would render more costs than benefits, sio kwa CCM tu bali kwa Taifa; Again, huyu ni rais wa nchi, sio wa CCM au Chama cha Soka; Hakuna mtanzania anayetaka utawala wa nchi uwe na msukosuko zaidi ya huu wa sasa ambao unatokana na minyukano yao wenyewe huko CCM, na hali itakuwa mbaya iwapo maamuzi juu ya suala hili yatafanyika kwa kukurupuka badala ya kutumia busara;

Iwapo kikao husika kitakubaliana kwamba kuna tatizo, option nyingine nzuri ni kuanzisha ‘a transition period' na kuchagua mwenyekiti mpya ambae huyo ndiye ataandaliwa kuwa mgombea Urais kupitia CCM 2015; Kuchagua tu mtu yeyote bila ya kuweka mazingira ya transition period nchi itajuta kwa kushabikia yaliyotokea kwani mwenyekiti mpya atamvuruga Rais na atavuruga mchakato wa kumpata mgombea 2015 aidha kwa kuvutia ngoma kwake au kukandamiza wengine kwa faida ya chaguo lake;

Unchoeleza ni sahihi lakini nadhani hoja yako umeijenga katika misingi ya hofu tu na zaidi kuikanyaga demokrasia yenyewe unless kama wewe si muumini wa falsafa ya check and balances (separation of powers) ili mambo yaende vema na kuchochea uwajibikaji.

Kama hoja ni kufanya cost benefit analysis kama unavyosema watu walishafanya hivyo zamani ndiyo maana unaona hayo mabango huko Dodoma na hata wananchi kushindwa kuyaona Maisha Bora. J.M Kikwete ameprove failure ya kiuongozi ndani ya chama chake na hata katika nchi muda mrefu. Evidences ziko nyingi sana lakini moja tu ni ile ya kushindwa kuitetea na kuitekeleza hoja aliyoiasisi ya Kujivua gamba.Mimi binafsi naamini hilo moja tu ndilo linalokifanya chama chake leo kionekane kama kituko kwa watu wengi makini.

Kumbuka alivyowachoresha akina Nape, Chiligati na Mukama kwenye hoja hiyo ya kuvua gamba.Watu wamezunguka nchi nzima kuhubiri dhana hiyo lakini mwisho wa siku aliyeasisi hoja hiyo yuko kimya hadi leo. Yaani mwasisi wa hoja anaikimbia hoja, anashindwa kuisimamia na kuifkisha mwisho. Huu ni udhaifu mkubwa wa kiuongozi. Sasa utaona hili la udhaifu limekuwa kubwa sana kiasi cha kutishia kusambaratisha chama chake na hata taifa lenyewe (Rejea uprisings za Udini na ukabila nchini)

Unaposema udhaifu wa kiongozi unapimwa kwa kuungwa au kutoungwa mkono na watu nadhani si sahihi, kiongozi anapimwa kwa maamuzi anayochukua, utendaji wake, uadilifu na uwezo wa kusimamia maslahi mapana ya chama chake na kwa maana hiyohiyo taifa. Sasa ukiwa na kiongozi anayekwama katika mambo yote hayo unategemea nini?
 
Acha ccm ife, tunahitaji fikra nyingine kutoka chama kingine, miaka 50 watu wanatoka kwenye mkondo mmoja tu wa ccm kwani tumerogwa? Wacha watwanganane, lefthook! Righthook! Jab one! Uppercut..! Kama wale mayoso wa uvccm, labda wakija wengine mapema hata bibi yangu ataona mwanga wa umeme kijijini
 
Iwe ni CCM, CUF, au CHADEMA Madarakani, ni kosa kubwa sana kutenganisha kofia ya Mwenyekiti wa Chama na Urais, sisi bado ni wachanga sana katika mfumo huo, hasa kutokana na kila mtu kutaka kuwa Rais hata akionja hata ukatibu kata; Nafasi ya mwenyekiti wa chama kwa nchi changa maana yake huyo ni Rais moja kwa moja au ana mkono mrefu wa kuteua Rais awe nani; Ni muhimu nafasi hii ibakia kama ilivyo huku nguvu za kiti hicho zikianza kupunguzwa taratibu na kupelekwa kwenye organs nyingine za chama;

Ni nchi kubwa kama marekani na kwingine ambao wamekomaa kiasi cha kwamba mwenyekiti wa DNC au RNC rarely proceed kutaka Urais wa nchi; Kama kuna consensus na pia hoja ya msingi juu ya tatizo hili, solution ya busara ni aidha:

  • Achagulie mtu ambae officially na kwa uwazi kabisa, atakuwa ndiye anayeandaliwa kuwa mrithi wa kiti cha Urais kupitia CCM kama wanavyofanywa Botswana, na hili lije chini ya mfumo mpya wa transitional leadership..., au
  • iwekwe kanuni kwamba mwenyekiti wa Chama cha siasa hatoruhusiwa kugombea Urais wa nchi katika kipindi cha miaka mitano baada ya kuachia nafasi yake hiyo; au
  • Katiba ya CCM ifanyie marekebisho nguvu na mamlaka ya mwenyekiti ili asiwe na absolute power ndani ya chama, na hilo likiwezekana, basi nafasi hizi mbili ndio zitenganishwe;

Pengine ni muhimu kwa mapinduzi haya yafanikiwe ili muone nilikuwa nina maanisha nini kama mtanzania;

Bado una mawazo ya chama kushika hatamu ndiyo maana....Hakuna zaidi ya hilo. Lakini hayo ni mawazo yako si lazima yawe yangu. SS CDM ndiyo maana tulimsimamisha Dr. Slaa kuwa Rais huku mwenyekiti akiwa Mh. Mbowe..Maana hatufikiri ki CCM je sisi si wa-Tanzania? We unapoiona hatari katika nchi nchi yako ni CCM? Maana unashindwa hata kuelewa kuwa CCM si synonym ya Tanzania labda kama unawaza mfumo wa chama kimoja na chama kushika hatamu..Watu kama nyinyi ni hatari kwa usalama wa nchi hii maana ukada umewajaa hadi mnashindwa kufikiria nje ya box la dude linaloitwa CCM..Maana unajua CCM ni chama dola na wala siyo democratic party bila dola CCM haipo and thats exactly what you say without realising! Na hii inaji-reflect sasa ambapo democratically CCM is out votted lakini inalindwa kwa mtutu isiondoke na pale dola inapotaka kuji-detach na CCM wewe unaona hatari (ambayo in reality ni kwako zaidi kama kada) na salama kwa raia wa kawaida wa Tanzania.
 
It has nothing to do with mfumo wa chama kimoja, wala chama kushika hatamu; Hivi unajua maana ya chama kushika hatamu ni nini? nadhani wengi wana uelewa usio sahihi juu ya hili; Vinginevyo laiti ungejua role ya Mbowe katika kuchagua mgombea urais, usingesema hayo, kwani zaidi ya kuwa na mkono wa Mwenyekiti, pia he makes paternal decisions, na hili linanyemelewa CCM pia kwani nacho kimeanza kuwa chama cha wenyewe, ndio maana nasema kwamba sisi bado ni wachanga sana kisiasa; Lakini huu ni mjadala mwingine;

Tukirudi kwenye point ya msingi, hata kama ningekwa mwanachama wa Chadema, ningekwepa ushabiki huu kwa hoja kama zako za ukada wa ccm, sijui chama kimoja, sijui hatamu ya chama, sijui hatari kwa usalama wa nchi na mambo mengine mengi ambayo yamejaa hoja za hasira kuliko zenye busara, na vile vile kimsingi yanaegemea zaidi utamaduni wetu wa kufurahia crisis za kisiasa zisizokuwa na manufaa yoyote; Kama wewe ni chadema, jipangeni, 2015 nchi ni yenu, na ikiwa tofauti na hili, wa kujilaumu itakuwa ni nyinyi wenyewe;

Vinginevyo nina imani kwamba kwa wengine wengi, hoja yako kuhusu umuhimu wa Kikwete kutolewa uenyekiti wa CCM nakubakishiwa Urais, imeeleweka, na hoja yangu kupinga hilo kupitia bandiko langu namba 85 na namba 99 la uzi huu imeeleweka; kilicho muhimu sana ni matatu:

  • Kwanza, tukubaliane kutokukubaliana, kwani huu ni mgongano tu wa mawazo;
  • Pili, tusubiri historia itatufundisha nini, na
  • Tatu na muhimu zaidi - pengine tuombee mapinduzi hayo ya kumtoa Kikwete kwenye uenyekiti yafanikiwa ili theory ikutane na practice, kwani sasahivi mimi na wewe tunachofanya ni Ku-theorize tu, kwahiyo sio hoja zako, wala zangu ndio zipo sahihi na zenye maana, ingawa wewe you fall short of kutoa hoja mbadala na badala yake ni malalamiko yale yale tu ya CCM CCM CCM CCM; CCM ina kera, sio uongo, lakini jengeni hoja, sio lawama;

Ukiwa na muda, pinga kwa hoja bandiko lango namba 99, kwani hivyo ndivyo tutakuwa na mjadala wenye manufaa kwa taifa;
 
Unchoeleza ni sahihi lakini nadhani hoja yako umeijenga katika misingi ya hofu tu na zaidi kuikanyaga demokrasia yenyewe unless kama wewe si muumini wa falsafa ya check and balances (separation of powers) ili mambo yaende vema na kuchochea uwajibikaji.

Kama hoja ni kufanya cost benefit analysis kama unavyosema watu walishafanya hivyo zamani ndiyo maana unaona hayo mabango huko Dodoma na hata wananchi kushindwa kuyaona Maisha Bora. J.M Kikwete ameprove failure ya kiuongozi ndani ya chama chake na hata katika nchi muda mrefu. Evidences ziko nyingi sana lakini moja tu ni ile ya kushindwa kuitetea na kuitekeleza hoja aliyoiasisi ya Kujivua gamba.Mimi binafsi naamini hilo moja tu ndilo linalokifanya chama chake leo kionekane kama kituko kwa watu wengi makini.

Kumbuka alivyowachoresha akina Nape, Chiligati na Mukama kwenye hoja hiyo ya kuvua gamba.Watu wamezunguka nchi nzima kuhubiri dhana hiyo lakini mwisho wa siku aliyeasisi hoja hiyo yuko kimya hadi leo. Yaani mwasisi wa hoja anaikimbia hoja, anashindwa kuisimamia na kuifkisha mwisho. Huu ni udhaifu mkubwa wa kiuongozi. Sasa utaona hili la udhaifu limekuwa kubwa sana kiasi cha kutishia kusambaratisha chama chake na hata taifa lenyewe (Rejea uprisings za Udini na ukabila nchini)

Unaposema udhaifu wa kiongozi unapimwa kwa kuungwa au kutoungwa mkono na watu nadhani si sahihi, kiongozi anapimwa kwa maamuzi anayochukua, utendaji wake, uadilifu na uwezo wa kusimamia maslahi mapana ya chama chake na kwa maana hiyohiyo taifa. Sasa ukiwa na kiongozi anayekwama katika mambo yote hayo unategemea nini?

Umemjibu vizuri huyu kada wa CCM...

Kilichopo hapo ni struggle of power kati ya makundi ndani ya CCM....Yaani kuna kundi ambao lina resources za kutosha lakini halina power na hivyo linataka ku-gain power ili kuendeleza statusquo yao (aspirant wa urais i.e do or die in consolidating the power combined with resources ili waweze ku-rule)....Kuna kundi ambalo kwa sasa lina power na lina resources pia in the same ways kama wao wengine lakini ukweli ni kwamba power iliyonayo ni shortlived kuanzia sasa and soon what i-loose kama hawatapata watu wakuendeleza statusquo yao...Kwa hivyo wana struggle ku maintain the consolidated power.....

Uzuri ni kuwa nature ilitusaidia kukawa na uadui kati ya haya makundi kwahiyo kila mmoja hana uhakika na mwenzake ata react vipi soon atakapo gain hiyo power so they cannot form coarlition to consolidate the power...

Hapa hakuna hatari kwa raia ila hatari ipo kwa allies tu ambao wanaji associate na hayo makundi na ndiyo amabao wana fight for their lords....

Mwananchi wakawaida atafaidika iwapo tu hayo makundi yatashindwa ku-consolidate hiyo power na kubakiwa na resources ambazo kama hawakuzipata kwanjia ya halali badi zitamnufaisha zaidi mwananchi zaidi ya kudhoofisha....Sasa tungekuwa na system nzuri zenye integrity inayotakiwa its a time to render the two groups powerless ili democracy ichukue mkondo wake huku wakisaidia kujenga system ambayo itakuwa na checks and balance ili tusijeingia katika hii hali ya individuals kuwa na power kuliko system....Kazi kwenu wenye mamlaka ya ulizni wa utaifa wetu ama mtuuze tuingie kwenye historia mpya ya mapambano ambapo wengi watakuwa wanapigana bila kujua they are just being used to serve the lords ama mtuokoe sote tubaki kuwa salama na kuwaondoa hawa wachache ambao wametufikisha hapo tulipo sasa....
 
Unchoeleza ni sahihi lakini nadhani hoja yako umeijenga katika misingi ya hofu tu na zaidi kuikanyaga demokrasia yenyewe unless kama wewe si muumini wa falsafa ya check and balances (separation of powers) ili mambo yaende vema na kuchochea uwajibikaji.

Kama hoja ni kufanya cost benefit analysis kama unavyosema watu walishafanya hivyo zamani ndiyo maana unaona hayo mabango huko Dodoma na hata wananchi kushindwa kuyaona Maisha Bora. J.M Kikwete ameprove failure ya kiuongozi ndani ya chama chake na hata katika nchi muda mrefu. Evidences ziko nyingi sana lakini moja tu ni ile ya kushindwa kuitetea na kuitekeleza hoja aliyoiasisi ya Kujivua gamba.Mimi binafsi naamini hilo moja tu ndilo linalokifanya chama chake leo kionekane kama kituko kwa watu wengi makini.

Kumbuka alivyowachoresha akina Nape, Chiligati na Mukama kwenye hoja hiyo ya kuvua gamba.Watu wamezunguka nchi nzima kuhubiri dhana hiyo lakini mwisho wa siku aliyeasisi hoja hiyo yuko kimya hadi leo. Yaani mwasisi wa hoja anaikimbia hoja, anashindwa kuisimamia na kuifkisha mwisho. Huu ni udhaifu mkubwa wa kiuongozi. Sasa utaona hili la udhaifu limekuwa kubwa sana kiasi cha kutishia kusambaratisha chama chake na hata taifa lenyewe (Rejea uprisings za Udini na ukabila nchini)

Unaposema udhaifu wa kiongozi unapimwa kwa kuungwa au kutoungwa mkono na watu nadhani si sahihi, kiongozi anapimwa kwa maamuzi anayochukua, utendaji wake, uadilifu na uwezo wa kusimamia maslahi mapana ya chama chake na kwa maana hiyohiyo taifa. Sasa ukiwa na kiongozi anayekwama katika mambo yote hayo unategemea nini?

Sio siri, siungi mkono siasa za Nape, Mukama, na hao wote ndani ya hicho chama; Kwanini? Kwa sababu siasa zao hawa wote ni za ovyo, hazijengi nchi bali kubomoa, na Kolimba alishalisemea sana hili; Wananchi wana hasira sana na CCM, mimi nikiwa mmoja wao, na kuwa mwanachama wa CCM haina maana nakubaliana na uongozi uchwara wa hao niliowataja hapo juu, ni kwamba naangalia zaidi maslahi ya taifa hili; Ni muhimu kwa CCM kumwachia Kikwete amalize akiwa na kofia zake mbili kwa hoja nilizojenga, na hii sio kutokana na hofu kama unavyosema, bali mapenzi kwa nchi yetu; Ni dhahiri kwamba kofia ya mwenyekiti imeyumba, lakini kumtoa na kumwachia Urais nchi itayumba zaidi;

Kama ni kumtoa kwenye kiti, basi aidha:

  1. Yafanywe marekebisho ya nafasi hiyo ili huyo watakaomweka isiwe na absolute power ndani ya chama, au
  2. Katiba ipitishe kanuni kwamba mwenyekiti wa chama asigombee nafasi ya Urais kwa miaka mitano baada ya kumaliza muda wake katika nafasi hiyo, au
  3. ipitishwe kanuni kwamba miaka miwili kabla ya uchaguzi mkuu wa nchi, kuwe na transition period ambapo mwenyekiti mpya anateuliwa kama mtu anayeandaliwa kumpokea Rais aliyepo madarakani kwenye uchaguzi mkuu unaofuatia;

I can assure you, iwapo option 1 au 2 hapo juu itakuwa pursued, kiti hicho kitaanza kukimbiwa kama ukoma na kukirudisha chama katika mstari in a way; otherwise ni kutokana na zoezi hili kuwa na implication ya option 3 indirectly, ndio maana suala hili limefikia lilipo sasa!!!

Hata Nyerere alipinga sana hoja ya kutenganisha kofia hizi mbili licha ya yeye pia kuwa mstari wa mbele kukemea udhaifu wa mwinyi kama Rais na Mwenyekiti wa CCM miaka ya tisini; Nyerere alikuwa na mapungufu yake lakini katika baadhi ya mambo alikuwa na busara sana, huku akiweka maslahi ya taifa mbele zaidi kuliko ya CCM, na hili la kofia hizi mbili ikiwa ni moja wapo;
 
Wacha wamvue uenyekiti, kasababisha umasikini, ameshindwa kukemea udini, kaongeza deni la taifa, karuhusu mafisadi wateue spika anaewalinda
 
hii ndio safari ya CCM kuwa KANU, subiri Nov. 2015
 
Hivi wale waliopigana na kurushiana viti kwenye uchaguzi wa UVCCM kule wilayani Tarime walifikishwa Mahakamani? Maana lile ni kosa la jinai kupigana.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
It has nothing to do with mfumo wa chama kimoja, wala chama kushika hatamu; Hivi unajua maana ya chama kushika hatamu ni nini? nadhani wengi wana uelewa usio sahihi juu ya hili; Vinginevyo laiti ungejua role ya Mbowe katika kuchagua mgombea urais, usingesema hayo, kwani zaidi ya kuwa na mkono wa Mwenyekiti, pia he makes paternal decisions, na hili linanyemelewa CCM pia kwani nacho kimeanza kuwa chama cha wenyewe, ndio maana nasema kwamba sisi bado ni wachanga sana kisiasa; Lakini huu ni mjadala mwingine;

Tukirudi kwenye point ya msingi, hata kama ningekwa mwanachama wa Chadema, ningekwepa ushabiki huu kwa hoja kama zako za ukada wa ccm, sijui chama kimoja, sijui hatamu ya chama, sijui hatari kwa usalama wa nchi na mambo mengine mengi ambayo yamejaa hoja za hasira kuliko zenye busara, na vile vile kimsingi yanaegemea zaidi utamaduni wetu wa kufurahia crisis za kisiasa zisizokuwa na manufaa yoyote; Kama wewe ni chadema, jipangeni, 2015 nchi ni yenu, na ikiwa tofauti na hili, wa kujilaumu itakuwa ni nyinyi wenyewe;

Vinginevyo nina imani kwamba kwa wengine wengi, hoja yako kuhusu umuhimu wa Kikwete kutolewa uenyekiti wa CCM nakubakishiwa Urais, imeeleweka, na hoja yangu kupinga hilo kupitia bandiko langu namba 85 na namba 99 la uzi huu imeeleweka; kilicho muhimu sana ni matatu:

  • Kwanza, tukubaliane kutokukubaliana, kwani huu ni mgongano tu wa mawazo;
  • Pili, tusubiri historia itatufundisha nini, na
  • Tatu na muhimu zaidi - pengine tuombee mapinduzi hayo ya kumtoa Kikwete kwenye uenyekiti yafanikiwa ili theory ikutane na practice, kwani sasahivi mimi na wewe tunachofanya ni Ku-theorize tu, kwahiyo sio hoja zako, wala zangu ndio zipo sahihi na zenye maana, ingawa wewe you fall short of kutoa hoja mbadala na badala yake ni malalamiko yale yale tu ya CCM CCM CCM CCM; CCM ina kera, sio uongo, lakini jengeni hoja, sio lawama;

Ukiwa na muda, pinga kwa hoja bandiko lango namba 99, kwani hivyo ndivyo tutakuwa na mjadala wenye manufaa kwa taifa;

You suffer from ego-centrism that mine is gud yours is bad, and I guess have nothing to discuss with people of your kind....
 
Wowowo, Ame

Unaposema udhaifu wa kiongozi unapimwa kwa kuungwa au kutoungwa mkono na watu nadhani si sahihi, kiongozi anapimwa kwa maamuzi anayochukua, utendaji wake, uadilifu na uwezo wa kusimamia maslahi mapana ya chama chake na kwa maana hiyohiyo taifa. Sasa ukiwa na kiongozi anayekwama katika mambo yote hayo unategemea nini?

Kiongozi ni yule mwenye wafuasi, kwani bila ya kuwa na wafuasi, hakuna kiongozi, pengine atakuwa ni mtawala tu; Na katika muktadha huu, wafuasi ni synonym na kuungwa mkono; Masuala ya maamuzi, utendaji, uadilifu, usimamizi wa maslahi mapana n.k, haya yote ndio yanapelekea mtu mwenye nafasi ya uongozi kuungwa mkono au kutoungwa mkono na wale anawaongoza au kuwa na wafuasi au kutokuwa na wafuasi;

Weakness or Strength ya Kiongozi inapimwa na jinsi gani anaungwa mkono kutokana na maamuzi yake, utendaji, uadilifu, usimamizi wa maslahi ya umma n.k; Sasa tukirudi kwa Kikwete, tatizo alilonalo ni kwamba haungwi mkono unanimously ndani ya chama chake, hasa baada ya February 2008, na ndio maana maamuzi, utendaji, usimamizi wa maslahi ya umma n.k unakuwa mgumu kwani wanaofanikisha haya ni viongozi wenzake, sasa kama hawamuungi mkono, definitely he will appear weak as a leader;
 
You suffer from ego-centrism that mine is gud yours is bad, and I guess have nothing to discuss with people of your kind....

my comment was very objective, but wewe you are getting personal; You chose to respond to my post, sikukulazmisha, just as now choosing to quit, sikukufukuza; Ulichofanya ni kutafuta AN EXIT STRATEGY kutokana na kuishia au kulemewa na hoja by picking on me, something which 5 yrs ago i would have done the same; Otherwise yote haya ni haki yako, lakini muhimu na nachojali zaidi ni kwamba mimi, wewe, na wengine wengi humu tumejifunza katika exchanges zetu; Kila la kheri;
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Sio siri, siungi mkono siasa za Nape, Mukama, na hao wote ndani ya hicho chama; Kwanini? Kwa sababu siasa zao hawa wote ni za ovyo, hazijengi nchi bali kubomoa, na Kolimba alishalisemea sana hili; Wananchi wana hasira sana na CCM, mimi nikiwa mmoja wao, na kuwa mwanachama wa CCM haina maana nakubaliana na uongozi uchwara wa hao niliowataja hapo juu, ni kwamba naangalia zaidi maslahi ya taifa hili; Ni muhimu kwa CCM kumwachia Kikwete amalize akiwa na kofia zake mbili kwa hoja nilizojenga, na hii sio kutokana na hofu kama unavyosema, bali mapenzi kwa nchi yetu; Ni dhahiri kwamba kofia ya mwenyekiti imeyumba, lakini kumtoa na kumwachia Urais nchi itayumba zaidi;

Kama ni kumtoa kwenye kiti, basi aidha:

  1. Yafanywe marekebisho ya nafasi hiyo ili huyo watakaomweka isiwe na absolute power ndani ya chama, au
  2. Katiba ipitishe kanuni kwamba mwenyekiti wa chama asigombee nafasi ya Urais kwa miaka mitano baada ya kumaliza muda wake katika nafasi hiyo, au
  3. ipitishwe kanuni kwamba miaka miwili kabla ya uchaguzi mkuu wa nchi, kuwe na transition period ambapo mwenyekiti mpya anateuliwa kama mtu anayeandaliwa kumpokea Rais aliyepo madarakani kwenye uchaguzi mkuu unaofuatia;

I can assure you, iwapo option 1 au 2 hapo juu itakuwa pursued, kiti hicho kitaanza kukimbiwa kama ukoma na kukirudisha chama katika mstari in a way; otherwise ni kutokana na zoezi hili kuwa na implication ya option 3 indirectly, ndio maana suala hili limefikia lilipo sasa!!!

Hata Nyerere alipinga sana hoja ya kutenganisha kofia hizi mbili licha ya yeye pia kuwa mstari wa mbele kukemea udhaifu wa mwinyi kama Rais na Mwenyekiti wa CCM miaka ya tisini; Nyerere alikuwa na mapungufu yake lakini katika baadhi ya mambo alikuwa na busara sana, huku akiweka maslahi ya taifa mbele zaidi kuliko ya CCM, na hili la kofia hizi mbili ikiwa ni moja wapo;

Naelewa sana wasiwasi unaoujenga lakini katika Demokrasia hicho unachokitetea cha kutaka Rais awe pia Mwenyekiti wa chama chake kinakosa mantiki sana.Kwanza kinajenga hofu ya wanachama kumpinga kutokana na yeye kuwa amiri jeshi mkuu na Rais lakini pia ni njia ya yeye kufanya atakavyo kutokana na sababu ya kwanza.

Kwa ujumla utenganishaji wa kofia hizi ni afya zaidi katika uwajibikaji wa kweli kuliko hofu unayoijenga ya nchi kutotawalika. Kwa nini isitawalike wakati vyombo vya Usalama na kidola viko chini ya Rais? Yaani Mwenyekiti wa chama tawala kutokuwa Rais wa nchi ni tatizo? Ninachokiona hii ni move ileile ya kuendeleza Falsafa ya zidumu fikra za Mwenyekiti.

Hata mimi siungi mkono baadho ya siasa zinazofanywa na CCM hasa kutokana na kujikita katika ubinafsi, ujambazi wa rasilimali za umma na zaidi kuwa zisizo na maslahi ya Taifa lakini tukubali hoja ya kutenganisha kofia hizi mbili ni ya msingi sana na ni wakati muafaka wa kuizungumza tena kwa nguvu zote
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Mkuu umemshambulia sana Mchambuzi bila kujibu hoja alizotoa. Mimi naona ni za msingi unless kama umempania toka wakati unamuaga wife home. Kwi kwi kwi

Hapana simshambulii mkuu wangu!!ila nimewaza jinsi anavyojaribu kuzuia gari moshi lililo kwenye mwendo kasi,,tena lililokatika breki,nilifikiri atawashauri hao wanamabadiliko wa ndani ya ccm(kama kweli wapo)njia bora ya kukiondoa chama hapa kilipofikia ambapo ni pabovu,ila yeye anashauri namna bora ya kuendelea kubaki hapo!!kumbuka kofia inayolalamikiwa na wapinzani hao wa ndani ya chama ni ile inayohusu maslahi ya chama moja kwa moja,na si taifa kwa ujumla wake,naamini kabisa kuwa watu haohao wanao demand kumvua kofia ya uenyekiti ndio watakaokuwa mstari wa mbele kumtetea pale chadema au cuf itakapo mtaka avue kofia ile nyingine ya urais,u amirijeshi nk,mkuu mchambuzi!kama ungeweza kukiri matumizi mabaya ya kofia hizi mbili yana tokana moja kwa moja na kofia hii moja ya kitaifa kuzidiwa nguvu na ile nyingine ya u-chama nadhani ungeinua mguu wako uanze safari mpya ya kifikra!angalia jinsi rasilimali za umma zilivyoporwa na chama kwa mgongo wa kofia hiyo ya uenyekiti,huko ndiko ilipoota ile falsafa maarufu ya bila ccm imara nchi itayumba,kilichopo ccm kwa sasa ni kila mmoja ku-struggle for existence,and finally the fittest one should survive,muda wa kuchomeka public interest kwenye power based crisis iliyopo ccm kwa sasa bado muda wake,wao wakidundana sisi tuilinde nyumba yetu,ili wasije n'goa fito na kuzitumia kama silaha,kwani vita yao ikchelewa kumalizika kuna hatari ya nyumba yetu kumalizika.
 
CCM itasambaratika kwasababu imeacha kusimamia misingi yake.
Sishangai yanayotokea ndani ya CCM kwani hata kwenye nchi kubwa duniani mambo haya hutokea. Kila msafara wa mamba hakukosekani kenge na kuna kipindi kenge nao hujizani ni mamba na kuanza kuwadharau mamba. Leo hii nimeona kwenye news HU JINTAO akistaafu ramsi na kuonya rushwa ndani ya chama tawala ambacho ni kikubwa na kina wanachama wengi kuliko chama chochote duniani. sasa kama china kunatokea shutuma kama hizi kwa nini zisitokee kwenye nchi masikini kama tanzania? Mie binafsi sipendi vurugu zinazotokea ccm kwa sababu ndio chama tawala na kama wakigombana madhara yake yataikumba nchi nzima na yatamgusa kila mtu.Hata chadema kuna mitafaruku yake kila mtu anajua. Mkumbuke mabadiliko ya ghafla husababisha tumbo la kuhara.
Ninawatakia mkutano mwema na wa wamani kwa faida ya nchi yetu.
 
my comment was very objective, but wewe you are getting personal; You chose to respond to my post, sikukulazmisha, just as now choosing to quit, sikukufukuza; Ulichofanya ni kutafuta AN EXIT STRATEGY kutokana na kuishia au kulemewa na hoja by picking on me, something which 5 yrs ago i would have done the same; Otherwise yote haya ni haki yako, lakini muhimu na nachojali zaidi ni kwamba mimi, wewe, na wengine wengi humu tumejifunza katika exchanges zetu; Kila la kheri;

I hope its a gud exit strategy what do you think? Kama hoja ni kama hizi I think is wise to remain quite than to discuss things in one dimension while in actual sense you need to look at them in three dimensions....

Nimekuuliza swali moja tu kwamba unavyosema nchi itaingia kwenye msukosuko nchi ni CCM kwa definition yako? Think in that context and see what I was trying to show....Hoja ya kutengenisha kofia ina nguvu zaidi kupitia hoja zako kuliko hata zangu if you are objective...

Kama Rais atakuwa independent from manipulation na influence za chama then system itakuwa na uhuru na uwanja mpana wakuisaidia nchi isiingie kwenye machafuko...Hatari kubwa ni pale ambapo mtu huyo huyo ni dola at the same time anatakiwa ku-play politics...

Lakini in practice CCM inapata nguvu kwasababu ya huo muundo kama Rais akiwa siyo mwenyekiti CCM itajiendesha ki-democrasia na kisiasa ili iipiku CDM....Hatari waliyoiona wengine ndani ya CCM ni kuwa ambao wana political influence hawana resources za kutosha...Makundi yenye resources moja lina power lingine ndiyo lina saka hiyo power..Then think who is more theoratical kati yetu mimi kada wa CDM na wewe kada wa CCM? Be fair to yourself and to others!
 
Back
Top Bottom