Mtifuano Mkutano wa CCM - Dodoma

Mtifuano Mkutano wa CCM - Dodoma

Zikiwa zimebaki siku tatu kuanza kwa mkutano mkuu wa CCM Taifa,Dodoma kumesambazwa vipeperushi vinavyowataka Wajumbe wa CCM kumkataa Mwenyekiti J.KIKWETE sababu ya udhaifu wake wa kiuöngozi unaokifanya chama chao kikòngwe kupoteza mvuto na kukataliwa na watu.

Kada aliyetoa shutuma hizo mbele ya waandishi wa habari amewataja Fred Lowasa,Martin Shigela,Bashe Hussein na Benno Malisa kama ndo wahusika wakuu wa vipeperushi hivyo.

Lakini Nape Nnauye akihojiwa na waandishi wa habari ktk uwanja wa ndege Dodoma alipofika kumpokea Mwenyekiti,NAPE amesema hao ni wahuni tu,ambao hawana nguvu ktk chama,wanatumia fedha za kifisadi kuyumbisha chama,ni wahuni tu wa barabarani ambao miili yao ipo CCM lakini akili zao zipo kwingine.

Tayali Mwenyekiti J.K amefika leo Dodoma kwa ndege 5H-TGF aina ya F50 tayali kwa mkutano mkuu wa chama!

Je hii ni nguvu ya Lowasa kukitikisa chama chake?[/QUOTE]

Kitendawiliiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!! Tega nikutegue. tulilala hadingwadingwa. HAPO KWENYE RED.
 
Hakuna kipengele kwenye katiba ya ccm kinachoruhusu mgombea mwingine zaidi ya aliepo madarakani
 
Hata kura za hapana ziwe nyingi kuliko za ndio mwenyekiti ni yule yule habadilishwi hadi 2015
 
kwishaaaaa Chama cha wanafiki safari yake inafikia ukingoni sasa
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Dalili za jk kumbeba Membe ndio zinamponza, aangalie sana aweza nyanganywa kadi mhe rais lowasa ni mtu mwingine kabisa, kuna watu wanamtii kuliko kristo na mtume muhamad
 
...... Ni muhimu kwa kofia hizi mbili ziendelee kubakia chini ya mtu mmoja kama ilivyo sasa, na iwapo hoja kwamba Mwenyekiti ni dhaifu itaungwa mkono na wengi, basi iwe ndio wake-up call juu ya umuhimu wa kuwa na uangalifu zaidi katika kuteua wagombea Urais kupitia CCM; Vinginevyo Mwenyekiti amebakisha miaka mitatu tu, aachwe amalizie muda wake;

Mkuu,
Hapo kwenye red.
Miaka mitatu kama Rais lakini wasipotenganisha baada ya muda wake kuisha kama Rais atakuwa bado ana miaka miwili kama Mwenyekiti wa chama kabla ya uchaguzi wa 2017 na haijulikani itakuwaje baada ya hapa kwa vile hatujui kama chama kitashinda uchaguzi wa Rais 2015
 
Lowassa hahusiki na huu mchezo mchafu. Ni mbinu wanazotumia wabaya wa Lowassa kumchonganisha na JK. Hawatafanikiwa. Lowassa ni mwanasiasa wa mikakati zaidi.
 
Kwa vyovyote vile hii si dalili nzuri kwa chama tawala.
Umoja na mshikamano umeenda wapi?

Nape anasema kama vile anawajuwa waliosambaza hivyo vipeperushi. kimsingi angesema vipeperushi ameviona lakini hawezi kusema zaidi kwa vile hajui anayehusika na hivi vipeperushi. Kwani nani amebainisha kuwa hivyo vipeperushi vinatoka kwa wana CCM, inawezekana vikawa vinatoka popote pale ili kuwamega zaidi wana CCM katika makundi.
 
Zikiwa zimebaki siku tatu kuanza kwa mkutano mkuu wa CCM Taifa,Dodoma kumesambazwa vipeperushi vinavyowataka Wajumbe wa CCM kumkataa Mwenyekiti J.KIKWETE sababu ya udhaifu wake wa kiuöngozi unaokifanya chama chao kikòngwe kupoteza mvuto na kukataliwa na watu.

Kada aliyetoa shutuma hizo mbele ya waandishi wa habari amewataja Fred Lowasa,Martin Shigela,Bashe Hussein na Benno Malisa kama ndo wahusika wakuu wa vipeperushi hivyo.

Lakini Nape Nnauye akihojiwa na waandishi wa habari ktk uwanja wa ndege Dodoma alipofika kumpokea Mwenyekiti,NAPE amesema hao ni wahuni tu,ambao hawana nguvu ktk chama,wanatumia fedha za kifisadi kuyumbisha chama,ni wahuni tu wa barabarani ambao miili yao ipo CCM lakini akili zao zipo kwingine.

Tayali Mwenyekiti J.K amefika leo Dodoma kwa ndege 5H-TGF aina ya F50 tayali kwa mkutano mkuu wa chama!

Je hii ni nguvu ya Lowasa kukitikisa chama chake?
Nilichokicapture hapa ni kwamba CCM ni chama cha wahuni na ndo mana Nape wala hajisumbui kufkiria ni wakina nani hao waliosambaza vipeperushi zaid ya kuwaita wahuni. Na mimi nadhan mwili ulipo ndipo mtu alipo, so kwa kinywa chake anakiri kuwa ndani ya CCM kuna majitu mahuni. Aidha, namtaka Nape agundue kuwa wanaompinga mgombea au kiongoz flani si busara kuwaita wahuni, napenda awatambue tu kama watu ambao wana itikadi tofauti. Haiwezekan wanachama wote ndani ya CCM wakawa na wazo moja. Hivyo mawazo mbadala yasionekane kama ni uhuni, kinyume na hapo utakuwa ni ushamba wa kisiasa!
 
Mbona hakuna cha ajabu, hii ndio kukua Kwa demokrasia ndani ya chama.

JK Na Nape Inabidi watii demokrasia bila shuruti

Hakuna kipengele ndani ya katiba ya CCM kinachosema rais lazima awe mwemyekiti Wa chama.

Wanaolalamika nawashangaa, Au ndio MBUMBUMBU hawajui kusoma hata katiba!
 
Alikwisha kaanga mbuyou na kuwaachia wenyemeno watafune, kama vile jini alilolifuga linaomba damu yake Dkt. baba riz
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Baada ya CCM kusambaratika kitafuata CHADEMA ambayo nayo inaharufu mbaya ya udini na umajimbo!
Anaponyolewa mwenzako we tia maji!

Ama kweli inaonekana haki haiiachi CCM kuishi. Inaonekana madhambi yao waliyoyatenda kwa miaka 50 yameshajaa kipimo chake, sasa kilichobaki ni kukabiliana na matokeo ya madhambi hayo. Kipimo cha uovu kikishajaa hakuna jinsi utaepuka kuvuna ulichopanda. Watajitahidi sana kukwepa kwa ujanja na hila zote lakini mwisho wa siku wataangukia pua tu. Hali hii ni kama Muda wa kuishi wa kiumbe hai. Muda ukishaisha hakuna jinsi utaepuka kifo hata kama utafanya nini. Hiki ndicho kinachoisumbua CCM kwa sasa. Tusubiri tuone jinsi huu mnyukano utakavyokuwa ukichukua sura mpya kila siku.
 
Asante kwa taarifa ila kunukuu aina na namba ya ndege aliyowasili nayo inasaidia nn au inaongeza nn kwenye hiyo thread yako?
 
[FONT=courier
new]Nape ndo muhuni akishirikiana na Riz Lengo ni
kumchafua Lowassa, Sisqo a.k.a Mwamba wa Kaskazini ni mzee wa strategy,
hawezi fanya huu upuuzi ingekuwa VIPEPERUSHWA Sawa tungeweza doubt
lakini sio huu upuuzi wa kisekondari tatu bila itawaumiza walale,
wainame, waamke 3-0, tatu bila dadadeki
zao
[/FONT]
mkuu naunga mkono Lowasa hawezi fanya upuuzi wa namna hii, huu ni ujinga wa baadhi ya maadui wa EL. haina tofauti na mtambo wa kujitumia sms kwa namba za maadui kama Mwigulu.
 
Back
Top Bottom