Mtifuano Mkutano wa CCM - Dodoma

Mtifuano Mkutano wa CCM - Dodoma

Ngaliba Dume

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2010
Posts
1,710
Reaction score
3,685
Zikiwa zimebaki siku tatu kuanza kwa mkutano mkuu wa CCM Taifa,Dodoma kumesambazwa vipeperushi vinavyowataka Wajumbe wa CCM kumkataa Mwenyekiti J.KIKWETE sababu ya udhaifu wake wa kiuöngozi unaokifanya chama chao kikòngwe kupoteza mvuto na kukataliwa na watu.

Kada aliyetoa shutuma hizo mbele ya waandishi wa habari amewataja Fred Lowasa,Martin Shigela,Bashe Hussein na Benno Malisa kama ndo wahusika wakuu wa vipeperushi hivyo.

Lakini Nape Nnauye akihojiwa na waandishi wa habari ktk uwanja wa ndege Dodoma alipofika kumpokea Mwenyekiti,NAPE amesema hao ni wahuni tu,ambao hawana nguvu ktk chama,wanatumia fedha za kifisadi kuyumbisha chama,ni wahuni tu wa barabarani ambao miili yao ipo CCM lakini akili zao zipo kwingine.

Tayali Mwenyekiti J.K amefika leo Dodoma kwa ndege 5H-TGF aina ya F50 tayali kwa mkutano mkuu wa chama!

Je hii ni nguvu ya Lowasa kukitikisa chama chake?
 
mkuuu kuwa karibu na huo mkutano wakitwangana mangume usisite kupiga picha na kutuwekea humu janvini
 
Nilishawahi kusema hapa kuwa ccm kama chama kimoja haipo, kilichopo ni at least ccm 4. Sasa wanaodhani kuwa baada ya zoezi lao la kununua uongozi likiisha watarudi kuwa kitu kimoja wanajidanganya wenyewe!
 
nimeona sasa hivi kwenye taarifa ya ITV, naona ni jambo zuri maana CCM inaelekea tunakotaka...downfall.
 
Vijana wa Nape hao. Nape ameshindwa kumface Laigwanan Mkuu sasa anaamua kutumia vijana wenye Njaa kupambana na Laigwanan
 
nyote mmeoza tu, wachafu kabisa, nyie ndo mmefich ela uswiz mnachekelea deni la taifa lkiongezeka, mmeiba ela BOT, aibu hamna, wezi wakubwa mkishirikiana na baba zenu, nawaombea muuane kabisa na msirudi mfie uko uko. mbwa nyie
 
Waacheni wamvue uenyekiti na hata ikibidi na urais pia nawaruhusu wamvue tu. Mie bado nayafikiria mafweza yaliyotunzwa nje ya nchi yetu. Pengine maisha bora yangewezekana bila ya huyu dhaifu.
 
..."Kama hata UWT wanatoa hongo kwenye chaguzi, basi namwachia Mungu".,JK -Dodoma October 2012.
 
Lowasa hahusiki hapo. Engineer wa huyo mchezo ni Makonda kwa Maelekezo ya Nape
 
Kweli Nape kaiva kwa propaganda!!!! Na yule jamaa aliyekutana na waandishi wa habari bila ya shaka ni kambi ya Ridhione.

Jambo hili liliandikwa na gazeti la Tanzania Daima lakini wengi walipuuza habari hizo na sasa ukweli wake umedhihili.

Naamini kabisa uchaguzi huu wa CCM utazaa mpasuko mkubwa zaidi au utastaajabisha ulimwengu.
 
utakuwa ni mchezo wa membe na nape kuchafua laigwanan .
 
watu wanajua kujipanga bana ....we acha .....tu hao ndio Ccm...wanasafisha njia tu wajumbe wanapiga chenga hapo ....
 
Kweli Nape kaiva kwa propaganda!!!! Na yule jamaa aliyekutana na waandishi wa habari bila ya shaka ni kambi ya Ridhione.

Jambo hili liliandikwa na gazeti la Tanzania Daima lakini wengi walipuuza habari hizo na sasa ukweli wake umedhihili.

Naamini kabisa uchaguzi huu wa CCM utazaa mpasuko mkubwa zaidi au utastaajabisha ulimwengu.

Nape amerithi kipaji cha Propaganda kutoka kwa Kingunge
 
Ama kweli inaonekana haki haiiachi CCM kuishi. Inaonekana madhambi yao waliyoyatenda kwa miaka 50 yameshajaa kipimo chake, sasa kilichobaki ni kukabiliana na matokeo ya madhambi hayo. Kipimo cha uovu kikishajaa hakuna jinsi utaepuka kuvuna ulichopanda. Watajitahidi sana kukwepa kwa ujanja na hila zote lakini mwisho wa siku wataangukia pua tu. Hali hii ni kama Muda wa kuishi wa kiumbe hai. Muda ukishaisha hakuna jinsi utaepuka kifo hata kama utafanya nini. Hiki ndicho kinachoisumbua CCM kwa sasa. Tusubiri tuone jinsi huu mnyukano utakavyokuwa ukichukua sura mpya kila siku.
 
nawatakia mtifuano mwema na ikibidi waje wameuana kabisa awa wezi wa rasilimali za nchi ii
 
Back
Top Bottom