Mtela Mwampamba afunguka ndani ya Passion FM

Mtela Mwampamba afunguka ndani ya Passion FM

Hivi mtu ukienda CCM ni lazima kwanza ujitoe akili ndio ukubalike huko! Sasa hii Agenda ya Baba wa Dr. Slaa kwamba Mwampamba anamjua huku akishindwa kumtaja inatija gani kwa Mtanzania ambae ananunua Unga wa Ugali kwa Shilingi 1500 kwa Kilo huku kilo ya nyama ya Ng'ombe ikifikia 6000? Je Inatija gani kwa Mzazi ambaye mwanaye amepata Division 0? Inatija gani kwa taifa ambalo 62% ya wanafunzi waliomaliza form four wamepata Division 0? Inatija gani katika kutokomeza wimbi hili la Ugaidi linalozidi kushamiri sasa hivi nchini? Inaweza vipi kuzuia kuuawa kwa Mapadri na Wachungaji kuchinjwa? Inaweza vipi kuzuia Makanisa kuchomwa kila uchwao? CCM mkiendelea na walemavu wa akili kama hawa na kuwafanya ndio misukule ya kupeleka sera zenu kwa wananchi hakika kihama chenu kitakuwa kabla 2015.
 
Huyo Mtela ndio wale wimbi la wasomi w.a.p.u.u.z.i yaani wasomi vyeti,ina maana yeye anaijua root ya Wibroad Slaa kuliko Dr anavyojijua?au ye Mtela ndio mama mzazi wa Dr Slaa?yote kwa yote kumjua baba mzazi wa Dr Slaa ina tija gani na taifa ili au inampunguziaje Dr Slaa utendaji na uadilifu wake?kuna mengi ya msingi kama taifa,60% ya wanafunzi wamefeli kidato cha nne,mauaji ya viongozi wa dini na choko choko zinazotia amani ya taifa letu,yeye kang'ang'ania Dr Slaa mara elimu ya Mnyika,wakati yeye mwenyewe Mwampamba hata kuelimika hajaelimika,ila ana vyeti tu,maana mtu aliye elimika hawezi kuamka kila siku analeta viroja kwa kushambulia watu tu badala ya hoja!shame on you
 
Yaani hiyo ndo kazi akina mwampamba wamekuja kufanya ndani ya ccm??? nani anaratibu shughuli za chama ndani ya ccm ama ndege haina rubani???
Hawa jamaa mimi nataka mdahalo nao.Mwampamba na SHONZA.Hawa wanasababisha watanzania waone siasa ni uhuni.
 
Huu utoto wa mazuzu yaliyovamia siasa unafundishwa katika shule walizotoka?
Itabidi niende chuoni kwa mwanangu nikasikilize wanachofundishwa. Nina wasi wasi sana na elimu ya Tanzania.
 
  • Thanks
Reactions: Pai
Hivi hii ID ya Taswira ndo mbadala wa ile ya Tuntemeke au ni hisia zangu tu? Manake naona ni kama iko maalum kwa ajili ya kutuletea habari za masalia tu hasa hasa Shonza na Mtela. Ile ya Tuntemeke siioni sana kwa sasa lakini maudhui yake hayana tofauti na ya Taswira. Ni mtazamo tu lakini.
 
Jana nilichangia issue ya Elimu ya John Mnyika kwamba hana degree lakini uwezo wake wa kupambanua mambo na hata kujenga hoja zenye maana kwa faida ya nchi yetu ni mkubwa kulinganisha na akina fulani pale waliopo magamba, tena wengine wana hata PHDs i said na naomba nirudie tena, mtu ukiwa CCM hata kama una madegree, sharti lao la kwanza lazima sehemu ya ubongo wako uuache pale Lumumba, mwoneni tena huyu degree holder, anaongea utadhani kijana wa darasa la pili, utakuta baada ya interview hiyo tayari alikwenda Lumumba kuchukua posho, sasa sisi baba wa Dr. Slaa anatuhusu nini, Kiwete amekua rais wa nchi, kuna hata mtu hua anajali kama wazazi wake wapo hai au wamekufa? Hali kadhalika Mkapa nae alikua rais wa nchi, kwanza juzi ndio nimejua kijiji chake kinaitwa Lupaso, sasa kama Dr. Slaa baba yake awe au asiwe mzee Peter Slaa, hilo lina nini kwetu? Kichwa kikubwa akili/ubongo ujazo wa kijiko cha chai.
 
Nape bwana,swali kaulizwa yeye badala ya kujibu anatuletea huyu kituko mwenye njaa,naye anauliza swali
 
Mungu nijalie maisha marefu nione mwisho wa hawa vijana
 
Mtela Mwambapa unaposema unamheshimu mtu huwezi tena ukatoka kwenda kumvua nguo barabarani.Ninasikitikia familia yako walidhani wamekupeleka shule kuelimika kumbe ulikuwa unajifunza kusoma na kuandika.Na mpaka unamaliza degree yako bado umejifunza kusoma na kuandika ni aibu sana.
 
WAKATI WA KAMPENI Mtela Mwampamba aliwahi kusema.....'' kijana kama upo CCM utakua mchawi ''.........sasa nimeanza kuamini
 
Last edited by a moderator:
Ngozi za kuchuna zimeisha sasa mmegeukia siasa
 
Mtela Mwambapa unaposema unamheshimu mtu huwezi tena ukatoka kwenda kumvua nguo barabarani.Ninasikitikia familia yako walidhani wamekupeleka shule kuelimika kumbe ulikuwa unajifunza kusoma na kuandika.Na mpaka unamaliza degree yako bado umejifunza kusoma na kuandika ni aibu sana.

Samahani isije kuwa ana degree ya c.u.pi
 
Wanajamvi nawahitaji hawa watu wawili waliovuliwa uanachama toka Chadema watueleze Watanzania, hizo propaganda wanazotoa ndiyo majibu ya shida za Watanzania?

Hayo marumbano yanawasaidia nini wauza nyanya, mboga au wafanyakazi na wakulima? leo mfuko wa mbolea unauzwa Tsh. 50,000 kule Songea wakati tumewaeleza watanzania kuwa kilimo ni uti wa mgongo, je wanayepi ya kutueleza kimikakati ya kuondokana na hayo, au mfumuko wa bei wa bidhaa mbalimbali?

Suala la kutafuta mababa, mama, mabibi wa watu sio suluhisho la umasikini wa watanzania wengi. Mtanzania akijua asipojua baba yako hakumwongezei wala kumpunguzia kitu. Tunahitaji watu mahiri watakao tutoa hapa tulipo katika lindi la umasikini, elimu kuwa chini, na hali ya huduma za afya kuwa sio zenye ubora na zenye gharama kubwa.

Tunahitaji tuone mikakati ya kuboresha afya ya msingi, kama huduma ya afya ya kinywa inatakiwa kutolewa kuanzia kituo cha afya basi vifaa na wataalamu wapatikane ili kupunguza adha kwa mgonjwa, kupunguza gharama ya kfuata huduma hizo wilayani na mwisho kupunguza gharama ya serikali kwa kufanya hospitali za taifa na kanda kuwa na msululu wa wagonjwa ambapo huduma zingeboreshwa kule chini mzigo wa majukumu ungepungua. Haya ndiyo tunataka tusikie, siyo mipasho ya jikoni.

Nawashauri hawa vijana kuchunga ndimi zao, hata Biblia inaonya kuhusu kiungo ulimi, kuwa waweza kukuletea shida au neema kadri ya matumizi yake. Unachokinena na kusema sasa ndicho kinachojenga future yako. Jamii itakuhukumu kwa matendo yako.
 
Suala la baba yake Dr. Slaa ni la mamake Dr. Slaa, huyo ndo pekee anaeweza kutoa uhakika wa baba halisi na kuwa Mzee Peter Slaa sio baba ake Dr. Kinyume cha hapo Bwana Mwampamba anajitukana mwenyewe kwa sababu hata kipindi Dr. Slaa anazaliwa, inawezekana baba ake Mwampamba (yule mzee alietimuliwa uanachama juzi) alikua bado hajabalehe au bado anajikojolea.
 
Yaani nashindwa kuelewa huko CCM kuna nini?? Naona imekaliwa vibaya sana!!! Kwa Dr. Slaa, hana haja ya kujibu huu ujinga kwani ataonekana ana-simple mind kama Mwampamba mwenyewe. Kama yeye Mwampamba anataka majibu aende kumuuliza mama yake Slaa na kama huyo mama ametangulia mbele ya haki amuulize Mungu. CCM inatumbukia kaburini yenyewe!!
 
Back
Top Bottom