Ama kweli 'upumbavu ni kipaji'.
Ninajiuliza kuna umuhimu gani wa sisi wananchi kujua baba yake Dr Slaa?
Hata kama huyo sio baba yake mzazi, je itatusaidia nini watanzania kumjua huyo baba wa ukweli? Je itaweza kuboresha huduma za afya kwa wananchi? Je itaongeza ufaulu wa watoto wetu mashuleni? Je itaweza kutatua matatizo ya maji katika mikoa mingi kama sio yote? Je itaweza kuturudishia rasilimali zetu zinazoibiwa kila kukicha huku wananchi wakiteseka na umaskini uliokithiri?
Nadhani Mtela amesahau kuwa huyo anayeshindana nae alishavuka vipimo vya muda, vya maneno na vya utendaji na ndio maana ameweza kuaminiwa kwa kiasi chote hiki na watanzania walio wengi.
Hofu waliyonayo CCM ni uadilifu na ile imani iliyojengeka kwa wananchi juu ya Dr Slaa, na ndio maana wanataka wabadili hiyo picha kwa maneno ya kuumba.
Mtela anajua kuwa kila propaganda iliyoletwa ilidunda, either kwa kuwa sio kipaumbele cha wananchi walio wengi ama kwa kuwa sio ukweli. Nini kinachomfanya kuja na upuuzi wa aina hii? Je ni njaa? Ama ndio purukushani za kutafuta kukubalika katika chama kipya?
Naamini ni muda pekee ndio utampa jibu sahihi!