MTEI: Nililipwa Mshahara sawa na Nyerere

tatizo lenu hamsomi, mnakurupuka tu kuchangia.
mtei alipunguza mshahara kwa kuona aibu atamzidi nyerere na sio kuwaonea huruma wananchi
nyerere hata asingelipwa hana cha kupoteza maana kila kitu alichohitaji ilikuwa juu ya kodi zetu

Big up jembe letu la moshi mtei

jembe la Arusha na Meru

Mzee umechoka pumzika, Maelezo yako yanadhihirisha ulivyo na hata Chama chako pia. Bila aibu unawaambia watz Kuwa ulipunguza mshahara wako kwa Kuwa Mwalimu Nyerere alipunguza wa kwake na kwa kuona Kuwa usingefanya hivyo mshahara wako ungekuwa mkubwa kuliko was Mwalimu, kumbe hukusukumwa na uzalendo wala huruma kwa wananchi wa kipato cha chini, una tofauti gani na wale waliopunguziwa kwa nguvu? Huu ni unafiki usiovumilika kusikika masikioni. Eti Huyu ndio mwasisi wa Chama mbadala! Tumekusikia Mzee hatutafanya makosa kamwe.

Uwe unasoma na kuelewa kabla Ya kupost, Mshahara wake ulikuepo kisheria na sheria ilikua inamlinda asiguswe na mamlaka yoyote ile juu mshahara wake. Hivyo uamuzi wa kupunguza kipato chake ilikua ni heshima kwa mkuu wake na kwa wananchi.

Je, kwenye CCM Ya sasa nani anaweza kupunguza mshahara wake kwa hiyari achilia mbali kwa lazima.?

Huyo mzee hakutaka kabisa kutumikia wa-Tz, hakushiriki kabisa hata kutafuta uhuru japo tayari alikuwa ana kaelimu kake. Na hata kuja kufanya kazi Tz ilikuwa ni kwa masharti ya kulipwa pesa nyingi sana. Hana hata chembe ya uzalendo.

Jamani lini tutaacha ushabiki? Wakati mwingine tutumie akili ya kawaida kubishana wakati aliyoyasema Mtei ni mambo ya msingi na hayagusi vyama kabisa. Yana akisi utaifa mbele na si vinginevyo.

Kuhusu Nyerere hata asipochukua mshahara alikuwa na shida ipi? Jamani! Kama rais hana shida kwa vile anapewa kila kwa nini wanalipwa mshahara wa zaidi ya mil.30?
 
tatizo lenu hamsomi, mnakurupuka tu kuchangia.
mtei alipunguza mshahara kwa kuona aibu atamzidi nyerere na sio kuwaonea huruma wananchi
nyerere hata asingelipwa hana cha kupoteza maana kila kitu alichohitaji ilikuwa juu ya kodi zetu

Kilichomfanya Nyerere apunguze mshahara wake ndicho pia kilimfanya Mtei apunguze wake pia sasa shida iko wapi! Tatizo la kujiona unajua mambo kuliko wengine ndo linaloisumbua nchi yetu
 
inaonesha ni jinsi gani umerukia kuchangia tu bila ya kusoma mada. mtei hakupunguza mshahara wake kwa sababu ya kuwaonea wananchi huruma bali kwa ajili ya kuona aibu kuwa atamzidi mshahara boss wake, haya ni maneno yake mtei. usitake kumlisha maneno mtei.
Mara nyingi asiye na hoja hujiita mwelevu na kuwatweza waliowelevu kuliko yeye kuwa ni wajinga. Hulka ya mjinga ni kujikweza, mweledi hujipambanua kwa hoja zake zenye uweledi ndani yake. Kuhitimisha hoja yako kwa kuwaita watanzania wenzako ni wajinga ni kiashiria tosha cha jinsi ulivyo. Punguani wa Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili huona watu wote wanamzunguka kama ni punguani wakiwemo madaktari wake. Sisemi wewe ndiwe ila unafananafanana na mfano huo.
Mtei hazungumzii jinsi ya kuendesha Taasisi ya Uraisi, anazungumzia jinsi viongozi wa sasa wasivyowaonea huruma masikini kiasi kuwa aliona apunguze mshahara wake ili kupunguza pengo la kipato kati ya walio nacho na wasionacho.
Ikiwa huoni uhusiano uliopo kati ya mshahara wa Raisi na uchumi wa nchi hapo kuna tatizo kubwa. Ikiwa sehemu kubwa ya pato la nchi linachukuliwa na wachache ina maana wananchi waliowengi hubakia kuwa masikini. Wananchi wakiwa masikini maana yake wanashidwa kumudu mahitaji yao ya kwaida kama vile kupeleka watoto wao shule, hospitali na kuwekeza kwa maendeleo yao binafsi.
Kubwa zaidi kiongozi wa nchi akiwa mbinafsi wasaidizi wake wote huwa wa binafsi kwa kuwa kiongozi wao ( their role model) ni fisadi. Raisi akijilimbikizia mshahara mkubwa kupita kiasi na wasaidizi wake pia hudai waongezewe na Raisi anakosa nguvu ya kuwazuia kwa sababu anaogopa kuzodolewa. Mawaziri, Wabunge na viongozi wengine kudai posho na marupurupu kila mara ni matokeo ya viongozi wao kujilimbikizia mali kupitia nafasi zao za uongozi. Uadilifu wa Baba au mama ni muhimu kwa uadilifu wa familia. Sio ajabu baba mzinzi kuwa na watoto wazinzi pia. Kama FaizaFoxy haya hujayaona ni kwa sababu bado hujakuwa, kuwa utayaona. Ni hulka ya watoto kuona wamekuwa sawa na wazazi wao lakini ukweli ni kuwa wanakuwa bado hawajakuwa.
 
ukweli mtupu. viongozi wa sasa kweli hawana haya hata kidogo. na hata wakimpa au wakasaidia kujinga makanisa jua kuna wanachokiwinda in return huko mbeleni. halafu kwa sababu wengi ni mazuzu basi wanawachekea kuwashangilia.

Uelewa wako unatia shaka. Mzee mtei anamlinganisha Nyerere katika nafasi yake na maraisi wengine wa siku hizi katika nafasi ile ile. Kama Nyerere hakuwa na shida ni vivyo hivyo kwa Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa na Jakaya. Hata hawa wasipochukuwa mishahara yao haina tofauti na Marehemu Nyerere asingalichukua. Sasa kama vile haitoshi hawa viongozi wa sasa sio hawapunguzi mishahara kwa kuwahurumia masikini bali pia huwaibia zaidi masikini na kujilimbikizia wao wenyewe na jamaa zao. Inashangaza kama huelewi mantiki ya Mzee Mtei, basi una safari ndefu sana kuweza kuchambua mambo. Mtei hamlinganishi Marehemu Nyerere na mtu kama wewe anamlinganisha na viongozi walioshika au kupata kushika nafasi kama yake. Upo hapo? Ua umejianda kutetea tu jambo lolote ili mradi uonekane umechangia? Hivi kweli unaweza kulinganisha uadilifu wa Marehemu Nyerere na kiongozi yupi wa sasa Tanzania ya leo? Mtei ingawaje haikuwa dhamira yake kupunguza mshahara wake lakini kwa kuona Boss wake amepunguza alipunguza pia mshahara wake, ina maana Mzee Mtei aliona aibu Boss wake apunguze halafu yeye apate zaidi ya Boss wake. Angalao Mtei aliona aibu, viongozi wa sasa hata HAYA hawana.
 
Kilichomfanya Nyerere apunguze mshahara wake ndicho pia kilimfanya Mtei apunguze wake pia sasa shida iko wapi! Tatizo la kujiona unajua mambo kuliko wengine ndo linaloisumbua nchi yetu
acha kumlisha maneno Mzee mtei. kwa kinywa chake anakiri kupunguza mshahara kwa kuona aibu kuwa mshahara wake utakuwa mkubwa kuliko wa boss wake. RUDIA KUSOMA KABLA HUJANIJIBU KAMA UTAHITAJI ILI TUWE KWENYE LEVEL MOJA.
 
Mara nyingi asiye na hoja hujiita mwelevu na kuwatweza waliowelevu kuliko yeye kuwa ni wajinga. Hulka ya mjinga ni kujikweza, mweledi hujipambanua kwa hoja zake zenye uweledi ndani yake. Kuhitimisha hoja yako kwa kuwaita watanzania wenzako ni wajinga ni kiashiria tosha cha jinsi ulivyo. Punguani wa Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili huona watu wote wanamzunguka kama ni punguani wakiwemo madaktari wake. Sisemi wewe ndiwe ila unafananafanana na mfano huo.
Mtei hazungumzii jinsi ya kuendesha Taasisi ya Uraisi, anazungumzia jinsi viongozi wa sasa wasivyowaonea huruma masikini kiasi kuwa aliona apunguze mshahara wake ili kupunguza pengo la kipato kati ya walio nacho na wasionacho.
Ikiwa huoni uhusiano uliopo kati ya mshahara wa Raisi na uchumi wa nchi hapo kuna tatizo kubwa. Ikiwa sehemu kubwa ya pato la nchi linachukuliwa na wachache ina maana wananchi waliowengi hubakia kuwa masikini. Wananchi wakiwa masikini maana yake wanashidwa kumudu mahitaji yao ya kwaida kama vile kupeleka watoto wao shule, hospitali na kuwekeza kwa maendeleo yao binafsi.
Kubwa zaidi kiongozi wa nchi akiwa mbinafsi wasaidizi wake wote huwa wa binafsi kwa kuwa kiongozi wao ( their role model) ni fisadi. Raisi akijilimbikizia mshahara mkubwa kupita kiasi na wasaidizi wake pia hudai waongezewe na Raisi anakosa nguvu ya kuwazuia kwa sababu anaogopa kuzodolewa. Mawaziri, Wabunge na viongozi wengine kudai posho na marupurupu kila mara ni matokeo ya viongozi wao kujilimbikizia mali kupitia nafasi zao za uongozi. Uadilifu wa Baba au mama ni muhimu kwa uadilifu wa familia. Sio ajabu baba mzinzi kuwa na watoto wazinzi pia. Kama FaizaFoxy haya hujayaona ni kwa sababu bado hujakuwa, kuwa utayaona. Ni hulka ya watoto kuona wamekuwa sawa na wazazi wao lakini ukweli ni kuwa wanakuwa bado hawajakuwa.

Ewe punguani, hao viongozi wa zamani waliwafanya masikini wakapange mawe kwenye foleni saa 8 za usiku mpaka siku ya pili hawajui hiyo foleni watakipata nini siku hiyo unga wa ngano, wa yanga, mchele au sukari au waambulie betri za national.

Nyerere aliwahamisha watu makazi na vijiji vyao vya asili akaenda kuwatupa maporini, walioliwa na simba haya, walioliwa na chui haya, waliogongwa na nyoka haya. Waliokufa kwa kukosa tiba haya, waliokufa kwa njaa ndio usiseme.Watu wamekula majani, wamekunywa maji ambayo hata ukimpa ng'ombe anayakataa.

Watu wanaishi ndani ya nyumba mume anamuogopa mke, mke anamuogopa mume. Hawana uhuru hata wakuyatoa ya moyoni.

Ukitembe ana kikapu njiani, mgambo wanakusimamisha kukuuliza umebeba nini, wakikukuta na kilo mbili za mchele au sabuni ya lux ni kosa la kuwekwa detention bila kuulizwa wala kupelekwa mahakamani.

Nyama kwenye mabucha ni foleni na utachukuwa unayopewa bila kuchaguwa, kama siku hiyo ni nusu kilo, haya tena, ugongewe kwenye kadi yako ya resheni usirudi mpaka wiki ijayo.

Halafu eti anajidai kukata mshahara wake huku anajichekesha bila mpango.

Ewe punguani hiyo ndiyo huruma? Huyo mzee Mtei anabwabwaja na kuhororoja tu, yeye alikuwa katika elites wa Nyerere waliofaidika na huo udhalim wa siku hizo, hayo nnayokueleza hayajamkumba, muulize alikaa hata siku foleni ya sukari?

Punguani wahed.
 
Uongozi ulikuwa enzi hizo sasa hivi tunatawaliwa tu!
Long live Edwin mtei.
 
Nitajitahidi kukuelimisha kwa sababu nijiendeleza kwa kadiri ya uwezo wangu wote kwa faida ya wote ukiwemo wewe. Kumwelewesha mtu anayejua kuwa anajua wakati hajui ni kazi ngumu. Ni vizuri ungeanza kwanza kuangalia kiini cha tatizo kabla hujamlaumu mtu binafsi. Sio Nyerere aliyeficha bidha bali nchi haikuwa na viwanda vya kutosha. Nyerere alitaka kujenga uchumi wa kujitegemea wakati viongozi wako wa sasa wanaamini katika kutembeza bakuli kuomba misaada. Nchili wekewa vikwazo na nchi tajiri ili isiweze kujitegemea. Hali ya kupotea kwa bidha na kuwa na mgao ni matokeo ya vita ya Kagera sio sababu ya Nyerere. Wakati nchi inavamiwa na Nduli Idd Amini ungetegemea Nyerere afanye nini? Nadhani kwa akili yako ungeona sawa watanzania wenzetu wa Kagera watekwe.
Msingi wa operation Sgeza ulikuwa na lengo la kuwaweka wananchi pamoja kwa nia ya kuwapa huduma za maji elimu na hospitali kw aurahisi zaidi, lakini kila jambo jipya liwe zuri au baya ni lazima wapinzani watakuwepo, sio lazima wawe wengi lakini wapo. Ni kama wewe tu unayeng'ang'ania kushinda hata pasipokuwa na hoja. Unaona tofauti na wenzako wanavyoona (hallucination). Hali hii huwatokea wenye matatizo ya Afya ya Akili. Wapo watu wanaokataa kuchemsha maji ya kunywa ati wamezoea tangu enzi za mababu zao. Wapo watu hadi leo serikali ikiwapa chandarua wajikinge na mbu ili kuzui mbu wasiwaume, ili kupunguza uwezekano wa kuambukizwa na malaria hutumia chandarua kuvulia samaki au kuzuia mwewe wasichukue vifaranga wa kuku. Mpo wengi hauko peke yako. Hata kama mpango huo ulikuwa na madhara madogo machache lakini ulileta mafanikio makubwa. Katika transformation yoyote huwezi kuepuka madhara angalao kidogo. Kuna wakati inabidi ukose mtoto aliyeko tumboni ili kuokoa uhai wa mama. Kufanya hivyo ni busara kuliko kuacha wote wapotee. Pengine kwa akili yako utachagua kuwaacha wote wafe. Kwangu mimi ilikuwa ni busara na wala haikupangwa, wengine wapate madhara ili maendeleo kwa wengi yapatikane. Mapinduzi yoyote ya maana lazima yawe na madhara .Hata dawa iwe nzuri namna gani haichi kuwa na side effect. Kama haujaelewa niulize tena nitakusaidia nina uzoefu wa kufundisha wanafunzi wazito kuliko wewe.

Ujinga mwingine unatisha sana,

Hivi Nyerere hata asipochukuwa mshahara alikuwa anashida ipi, nyumba bure, kula bure, kulala bure, na huku anazidi kuiangamiza Tanzania kuwa nchi masikini ya mwisho duniani.

Mtei asitafute umaarufu wa Kisiasa kwa kupitia jina la Nyerere, yeye kwanini aliachia/aliachishwa uwaziri? aeleze ukweli.

Unasema mengi mabaya kuhusu Nyerere lakini ukweli ni kuwa una chuki ya kidini, ewe shet.wany.

Hata kama asingekuwa analipwa kuna maraisi wangapi wa Afrika waliofanya kufuru, Nyerere angekuwa na roho ya kishetw..any kama yako asingesubiri hata mshahara.
 
Nitajitahidi kukuelimisha kwa sababu nijiendeleza kwa kadiri ya uwezo wangu wote kwa faida ya wote ukiwemo wewe. Kumwelewesha mtu anayejua kuwa anajua wakati hajui ni kazi ngumu. Ni vizuri ungeanza kwanza kuangalia kiini cha tatizo kabla hujamlaumu mtu binafsi. Sio Nyerere aliyeficha bidha bali nchi haikuwa na viwanda vya kutosha. Nyerere alitaka kujenga uchumi wa kujitegemea wakati viongozi wako wa sasa wanaamini katika kutembeza bakuli kuomba misaada. Nchili wekewa vikwazo na nchi tajiri ili isiweze kujitegemea. Hali ya kupotea kwa bidha na kuwa na mgao ni matokeo ya vita ya Kagera sio sababu ya Nyerere. Wakati nchi inavamiwa na Nduli Idd Amini ungetegemea Nyerere afanye nini? Nadhani kwa akili yako ungeona sawa watanzania wenzetu wa Kagera watekwe.
Msingi wa operation Sgeza ulikuwa na lengo la kuwaweka wananchi pamoja kwa nia ya kuwapa huduma za maji elimu na hospitali kw aurahisi zaidi, lakini kila jambo jipya liwe zuri au baya ni lazima wapinzani watakuwepo, sio lazima wawe wengi lakini wapo. Ni kama wewe tu unayeng'ang'ania kushinda hata pasipokuwa na hoja. Unaona tofauti na wenzako wanavyoona (hallucination). Hali hii huwatokea wenye matatizo ya Afya ya Akili. Wapo watu wanaokataa kuchemsha maji ya kunywa ati wamezoea tangu enzi za mababu zao. Wapo watu hadi leo serikali ikiwapa chandarua wajikinge na mbu ili kuzui mbu wasiwaume, ili kupunguza uwezekano wa kuambukizwa na malaria hutumia chandarua kuvulia samaki au kuzuia mwewe wasichukue vifaranga wa kuku. Mpo wengi hauko peke yako. Hata kama mpango huo ulikuwa na madhara madogo machache lakini ulileta mafanikio makubwa. Katika transformation yoyote huwezi kuepuka madhara angalao kidogo. Kuna wakati inabidi ukose mtoto aliyeko tumboni ili kuokoa uhai wa mama. Kufanya hivyo ni busara kuliko kuacha wote wapotee. Pengine kwa akili yako utachagua kuwaacha wote wafe. Kwangu mimi ilikuwa ni busara na wala haikupangwa, wengine wapate madhara ili maendeleo kwa wengi yapatikane. Mapinduzi yoyote ya maana lazima yawe na madhara .Hata dawa iwe nzuri namna gani haichi kuwa na side effect. Kama haujaelewa niulize tena nitakusaidia nina uzoefu wa kufundisha wanafunzi wazito kuliko wewe.

Kwanza jifunze kupangilia maandiko yako kwa coma, para, full stop na vidokezo vingine ili usomeke, ulivyoandika unaumiza macho. Siwezi kukusoma na nnadhani kuna wengi pia hawawezi kukusoma.

Ikiwa mfundishaji wenyewe kuandika tu ni namna hiyo, si hasha hata huelewi nnachokufunda na hao wanafunzi wako kwa uchache itakuwa ni majanga.
 
Hivi huyu mzee alipataje huu utajiri alio nao kama hakuwa mwizi?
 
Unasema mengi mabaya kuhusu Nyerere lakini ukweli ni kuwa una chuki ya kidini, ewe shet.wany.

Hata kama asingekuwa analipwa kuna maraisi wangapi wa Afrika waliofanya kufuru, Nyerere angekuwa na roho ya kishetw..any kama yako asingesubiri hata mshahara.

Mkiambiwa kweli mnasema chuki, na umeshaingiza dini. Hata hueleweki.

Nakupa ruksa, rudia post zangu uweke hapa ushahidi wa hiyo chuki, utachokikuta useme kuwa hapa haikuwa hivi ilikuwa hivi, haya anza.

Huwezi kuiongolea taasisi ya Urais bila kumtaja Rais wa awamu hiyo, na Nyerere ndiye anaetajwa hapa, sasa kuonesha makosa yake ndiyo chuki? onesha wewe basi mazuri yake aliyoyafanya na mimi ntakuonesha kuwa Kikwete kafanya mazuri kwa nchi hii kwa miaka 8 zaidi ya Nyerere kwa miaka 24.

Sasa wewe onesha yaliofanywa kwa Tanzania hii na awamu zote zilizopita, ya kwanza, ya pili, ya tatu na mimi ntakuonesha kuwa awamu ya nne imefanya zaidi ya zote hizo kwa pamoja. Kinakushinda nini?
 
Chuki zako ni udini mtupu huna lolote, na hujaanzia hapa muda wote upo hivyo, wala sihitaji kutoa ushahidi wowote coz umeshazibwa macho, masikio na fikra kwa mitazamo yako ya chuki binafsi.

Nyerere was a great man ever lived in Tanzania, na hakuna unachoweza kubadilisha.
 
Great kwa kuwawekesha watu foleni za chakula? kaya moja sukari kilo moja kwa wiki?

Great kwa kuifanya hii nchi na watu wake kuwa masikini wa mwisho duniani ilhali tuna kila mali za duniani?

Great kwa kuifanya hii ya mwisho kwa masomo Afrika Mashariki?

Great kwa kudhulumu mali za watu kwa kutaifisha na kuwalipa aliowaogopa na wengine kuwadhulumu?

Great kwa lipi zaidi?
 
Ile kuhama kwenye hoja na kuanza kujadili koma, vituo na aya inaonyesha tumeanza kuelewana kwa mambo ya msingi ila sasa tunaanza kuangalia mambo madogo madogo pia. Nakushukuru kwa kuelewa. Ushauri wako nitauzingatia nitakapoendelea kuchangia mada nyingine. Jambo la pili la kufurahisha ni hatua ya kuacha lugha ya matusi. Nakupongeza kwa hilo, ni hatua nzuri. Inaelekea ukikazaniwa utakuwa mchangiaji mwenye hoja na lugha nzuri masikioni mwa watu. Pull up.
Kwanza jifunze kupangilia maandiko yako kwa coma, para, full stop na vidokezo vingine ili usomeke, ulivyoandika unaumiza macho. Siwezi kukusoma na nnadhani kuna wengi pia hawawezi kukusoma.

Ikiwa mfundishaji wenyewe kuandika tu ni namna hiyo, si hasha hata huelewi nnachokufunda na hao wanafunzi wako kwa uchache itakuwa ni majanga.
 
Ile kuhama kwenye hoja na kuanza kujadili koma, vituo na aya inaonyesha tumeanza kuelewana kwa mambo ya msingi ila sasa tunaanza kuangalia mambo madogo madogo pia. Nakushukuru kwa kuelewa. Ushauri wako nitauzingatia nitakapoendelea kuchangia mada nyingine. Jambo la pili la kufurahisha ni hatua ya kuacha lugha ya matusi. Nakupongeza kwa hilo, ni hatua nzuri. Inaelekea ukikazaniwa utakuwa mchangiaji mwenye hoja na lugha nzuri masikioni mwa watu. Pull up.

Ewe punguani, hoja ipi hiyo uliyoileta sijaona hoja yako yoyote? kama uliiandika kwenye ile post yako ambayo haisomeki kumbuka kuwa "haisomeki".

Halafu licha ya kujifunza kuandika ipasavyo pia jifunze kuto kusema uongo. Hivi uongo unakusaidia nini?

Onesha tusi nililokutukana na wacha kuzuwa, kubwabwaja na kuhororoja. Na ukishindwa ujuwe wewe ni muongo, mnafik, fataani na mzandik. Unajuwa maana ya mzandik?
 
Nakumbuka humu ndani nilisema kuendelea kujadiliana na wewe ni kujijingisha. Nadhani uoni wangu ule ulikuwa wa busara zaidi kuliko nilivyoendelea kutaka kukuelimisha kumbe hata hufundishiki. Hata matiusi huyajui kwako ni lugha nzuri. Ni ngumu kukusaidia. Kisaikolojia watu wanyonge (inferiors) wanadhani kukubali kosa ni udhaifu wenye nguvu (superiors) hawaoni shida hata wakikosolewa. Wewe nilipokuambia kuwa tumeanza kuelewana umejihisi unyonge ukaona bora uendelee kushikilia kutoelewa na lugha ya matusi ili mradi ujioneshe kuwa hubadiliki. Kwa mwalimu kama mimi, tunajua, hata kama hujakiri kwa kinywa chako lakini kuna kitu umejifunza na umeelewa. Hata kama hujaelewa sasa, lakini naamini utaendelea kuelewa polepole kwa kuwa yawezeka you are a slow learner.

Ewe punguani, ikiwa unashindwa kuonesha tusi ulilotukanwa unakuwa ni nani zaidi ya muongo, fataani, mnafik na mzandik? Unajuwa maana ya mzandik?

Naona darsa limekuingia na sasa unajaribu kuandika kwa kuweka "coma" na "full stop", ingawa unahitaji mazoezi zaidi, pia endelea kujifunza kuweka "paragraphs", kwani andiko lako hilo la juu hapa halina paragraphs, na huko ni kuchosha wanaokusoma na kuchusha kwa andiko lako.

Kumbuka pia "coma" zako unaziweka ndivyo sivyo, soma sentensi kamili kabla hujaweka coma. Pata darsa dogo la matumizi ya "coma" likusaidie wewe na wengine, na ujuwe nguvu ya "coma" inavyoweza kubadili maana ya sentensi au hekaya yako nzima.

Mswahili akipata ------ hulia mbwata.

Mswahili, akipata ------ hulia mbwata.

Mswahili akipata, ------ hulia mbwata.

Mswahili akipata ------, hulia mbwata.

Mswahili akipata ------ hulia, mbwata.

Haya, jifanyishe mazoezi, kwa sentensi hiyo hiyo moja ambayo nimebadili nilipoziweka koma tu, na utaelewa tu nguvu ya koma.

Kumbuka, hapa ndiyo umekumbana na Maalima wa Waalimu, utatia akili ukitaka usitake.
 
mtei+px.gif

Mtei ambaye pia aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha kabla ya kuteuliwa kuwa Gavana wa BoT alisema katika mazingira ya sasa hakuna kiongozi yeyote ambaye anaweza kukubali au kupunguza mshahara wake.PICHA|MAKTABA

KWA UFUPI
Alieleza kuwa ukimwondoa yeye na Mwalimu Nyerere, Serikali iliamua kuwapunguzia mishahara watumishi wengine wa kada nyingine serikalini ili kubana matumizi.

Arusha. Inawezekana likawa jambo nadra kutokea kwa sasa, lakini enzi za uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere lilitokea.

Ni baada ya mwasisi huyo wa Taifa kuamua kwa hiari kupunguza mshahara wake kwa asilimia 10 ili kupunguza pengo baina ya maskini na wale wenye kipato cha juu, uamuzi ambao ulifuatwa na aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) wakati huo, Edwin Mtei.

Mwaka 1968, Mwalimu Nyerere aliyekuwa akilipwa mshahara wa Sh5,000 kwa mwezi alikiona ni kiasi kikubwa ikilinganishwa na wengi wa watumishi na hivyo kuamua kukipunguza.

Mshahara huo wa Mwalimu Nyerere ni sawa na ambao alikuwa akilipwa pia Gavana Mtei. Kutokana na punguzo hilo, mishahara yao ilishuka hadi Sh4,500 kwa mwezi.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili nyumbani kwake Tengeru, nje kidogo ya Mji wa Arusha Jumatatu iliyopita, Mtei alisema alifikia uamuzi huo wa kupunguza mshahara wake baada ya Mwalimu Nyerere kutangaza kupunguza mshahara wake.

Alisema: "Nilipunguza mshahara wangu tena kwa hiari yangu baada ya kuona Mwalimu Nyerere amepunguza wa kwake."

Alisema wakati ule mshahara wa Gavana ulikuwa ukipangwa na Serikali na kwamba ulikuwa na kipengele katika mkataba kikionyesha kuwa hauwezi kupunguzwa na mamlaka yoyote, labda atakapotaka mwenyewe.

Mtei ambaye pia ni mwasisi wa Chadema alisema sababu nyingine iliyomsukuma kupunguza mshahara wake ni kuona kwamba kama asingefanya hivyo, basi angemzidi mshahara Rais (Nyerere), kitu ambacho kwake hakukipenda.

Alisema, ingawa Mwalimu Nyerere alipunguza mshahara, lakini yeye kisheria hakuwa akibanwa kufanya hivyo kutokana na mkataba wake ambao ulikuwa ukiibana Serikali kutokuugusa mshahara wake.

Alieleza kuwa ukimwondoa yeye na Mwalimu Nyerere, Serikali iliamua kuwapunguzia mishahara watumishi wengine wa kada nyingine serikalini ili kubana matumizi.

"Watu wote walipunguziwa mishahara kuanzia vigogo wote (wa wakati ule)," alisema Mtei ambaye Jumamosi iliyopita alitimiza miaka 82 tangu kuzaliwa kwake.

Sababu za punguzo hilo Alisema Serikali ya Mwalimu Nyerere iliamua kuchukua hatua hiyo baada ya kuona kuwa kulikuwa na pengo kubwa la kipato kati ya watumishi wa ngazi za chini na wale wa juu.
Mwanasiasa huyo ambaye aliteuliwa kuwa Gavana wa BoT akiwa na umri wa miaka 32, jambo ambalo ni mara chache kufanyika kwa vijana kuaminiwa na hata kupewa madaraka makubwa kiasi kile, alisema Mwalimu Nyerere alimwamini kwa kiasi kikubwa.

Kuhusu Mwalimu Nyerere, Mtei alisema alikuwa kiongozi mwadilifu, ndiyo maana akafanya uamuzi mgumu kama huo wa kugusa mshahara wake mwenyewe.

Alisema kwa kizazi cha sasa ni watumishi wachache wa kuweza kuwalinganisha naye.

Alisema baada ya Mwalimu Nyerere kuondoka katika uongozi wa nchi, watumishi na hata viongozi walibadilika na kujiingiza katika mambo mengi yakiwamo yale ambayo yanakwenda kinyume na maadili.

Uongozi wa sasa

Mtei ambaye pia aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha kabla ya kuteuliwa kuwa Gavana wa BoT alisema katika mazingira ya sasa hakuna kiongozi yeyote ambaye anaweza kukubali au kupunguza mshahara wake.

"Katika mazingira ya sasa, jambo hilo haliwezekani kabisa," alisema. Aliongeza: "Hivi sasa viongozi wengi wanashindana kupeleka na kuficha fedha Uswisi, wengi wao wanakimbilia kwenye utajiri, si utumishi."

Alisema hivi sasa viongozi wengi wametanguliza mbele masilahi yao na wengine kujiingiza kwenye ufisadi na hivyo kushindwa kuwatumikia wananchi ipasavyo.

Mtei alisema viongozi wote lazima waongozwe na uzalendo na kuwahurumia wananchi wengi ambao ni maskini.

Alisema uamuzi walioufanya yeye na Mwalimu Nyerere hivi sasa unaweza kufanyika katika chama kingine kinachojali wananchi endapo kitaingia madarakani, ambacho hata hivyo alisema siyo CCM. chanzo.Mtei: Nililipwa mshahara sawa na Mwalimu Nyerere - Kitaifa - mwananchi.co.tz

Back
Top Bottom